Naombeni namba ya TAKUKURU_MWANZA

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,328
5,270
Hawa Polisi wamezidi kwa Rushwa,nimesimamishwa kila kitu kwenye gari kiko sawa kasoro reflector moja ndio siioni na nadhani ilipotelea car wash,nimembeleleza zaidi ya saa moja hanielewi anataka nilipe faini 30,000 mfukoni nilikuwa na 13,000 pekee nimelazimika kumpa 5000 ya rushwa na akaniruhusu niende .
wakuu nipeni namba ya TAKUKURU
 
itakusaidia nn hyo number? Ndio uwajibikaji huo na kama ungepata ajali mbele yake kidogo baada ya kukuruhusu alafu ukakosa triangle ya kuweka alafu ukasababisha ajali je situtaanza kuwatukana trafic? Amefanya vyema kukupa adhabu ya kuchukua pesa yako kwa sababu ya uzembe wako....ni bora umshukuru Mungu kakuachia hiyo uliyobakiwa nayo
Ningekuwa ni mimi ningeichukua yote hata usingebakiwa na kitu ili ujifunze kutokana na makosa........byeeeeeeeeeee wasalimu mwanza
 
Jamani tuacheni utani, hawa Trafic wa Mwanza ni balaa kuna jibaba moja jeupe na kijitambi chake limetokea mkoa wa wachaga kabila la wabahiri linapenda sana kusimama barabara ya kuelekea Shinyanga pale Relini kabla ya kufika Mkuyuni...huyu trafic ni balaa jamani anapenda rushwa balaa, ndugu yangu Takukuru utapoteza muda mkubwa wao keshasema kapewa kazi halafu kanyimwa madaraka na uwezo hivyo yeye mwenyewe kaamua kuacha watu wanyake rushwa kama wapendavyo! Natamani kuwe na sheria ya kuwatwanga bakora tu hawa matrafic mi sijui wanatutafuta nini! Vidaladala vyao vibovu kama nini na vinapeta tu kwenda Mwaloni,sie tunabanwa hadi penalti, yaani huyu jamaa akikosa kabisa makosa anaangalia matairi. Na sana sana akiona anayeendesha ni mwanamke ndo utampenda. Traficwa Mwanza wanachangia sana hata kuchelewesha watu makazini. Mkubwa wao aliangalie jeshi lake halifai!
 
itakusaidia nn hyo number? Ndio uwajibikaji huo na kama ungepata ajali mbele yake kidogo baada ya kukuruhusu alafu ukakosa triangle ya kuweka alafu ukasababisha ajali je situtaanza kuwatukana trafic? Amefanya vyema kukupa adhabu ya kuchukua pesa yako kwa sababu ya uzembe wako....ni bora umshukuru Mungu kakuachia hiyo uliyobakiwa nayo
Ningekuwa ni mimi ningeichukua yote hata usingebakiwa na kitu ili ujifunze kutokana na makosa........byeeeeeeeeeee wasalimu mwanza

kwanini wasitoe onyo we gambala rushwa?
 
TAKUKURU Mwanza hawana lolote, Afisa utumishi wa jiji kwa jina Songoma alikamatwa 'akijiandaa' akipokea rushwa ya ngono kutoka kwa mwalimu baada ya huyo mwalimu kuwapa taarifa hao maTAKUKURU hadi kwenye gesti, hadi leo hakuna kesi na huyo afisa utumishi kapanda cheo na kuwa afisa utumishi mkuu wa wilaya ya Ilemela. Maskini mwalimu wangu kabaki na fedhea tu. Mlaaniwe Takukuru!
 
Back
Top Bottom