Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
Nawasalimu wana MMU.
Jamani tuna hawa wadada wanatusaidia kukaa na nyumba zetu.
Kama tujuavyo maisha ya siku hizi bila simu inakuwa patashika kidogo.
Huwa mdada akija kama hana simu huwa nampa simu ambayo nimeinunua kwa ajili ya nyumbani ili niweze kuwasiliana naye naye awasiliane nami ambapo sipo nyumbani.
Na kama inatokea mdada kaja na simu yake basi simlazimishi atumie ile yangu, huwa natumia tu ile namba yake kwa mawasiliano.
Kinachotokea mpaka naomba mwongozo hapa ni kwamba; Huwa nampa sh. 1000 kila wiki kwa ajili ya simu, ili akipata dharura basi aweze kunitaarifu. Mara nyingi mimi huwa napiga simu nyumbani mara kwa mara kwa hiyo inatokea mara nyingi tu ndani ya wiki hajanipigia wala kutuma sms hata moja, na yaweza kuwa hivyo hata mwezi mzima.
Kinachonichosha, siku ikitokea kapata dharura wala hapigi, nikiuliza naambiwa simu haina hela.
Wenzangu pia mnakumbwa na hili tatizo?
Nifanyeje sasa ili hili tatizo liishe?
sababu wakati mwingine ni jambo la maana kabisa linatokea lakini hawezi kuniambia kisa hela kwenye simu kamaliza zoote kupigia watu wake, sasa maana yoooteee ya mimi kumpa hela ya simu inakuwa haipo.
Nimepata mdada mpya sasa nataka nianze naye tangu mwanzo sheria ya hela yangu ya simu iweje........