Naombeni msaada

jack 1

Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
61
Reaction score
63
Habari zenu jamani poleni na majukumu.

Mimi naombeni kuuliza utaratibu wa ustawi wa jamii unakuaje kama unataka baba wa mtoto atunze mtoto je?

1)Vitu gani wanaangalia na inakuwaje?

Samahani kwa anayejua naombeni mnijuze nitashukuru.
 
mkuu ungeenda ofisini kwao watakupa maelezo mazuri zaidi.
 
Nenda ofisini kwao utapata msaada unaouhitaji
 
Habari zenu jamani poleni na majukumu.

Mimi naombeni kuuliza utaratibu wa ustawi wa jamii unakuaje kama unataka baba wa mtoto atunze mtoto je?

1)Vitu gani wanaangalia na inakuwaje?

Samahani kwa anayejua naombeni mnijuze nitashukuru.

nipe nikuaidie kutunza mamaa.... na we uje nae!!!
 
Kwa mtindo huu, 50/50 ngumu sana. Badala ya kukomaa kuingiza kipato unawaza kwenda ustawi wa jamii?? Kwani wewe ni mke wa ndoa? Kama ni mzazi mwenza tu, sh100 kwa mwezi inakuhusu.

Na kama mtoto ana 7yrs+, ndo kabisaaa, akiamua kukukomesha anasema tu apewe akalee mwenyewe.

Ukizaa nje ya ndoa mtoto wako ana haki ndogo sana ya kudai, omba tu mwanamme awe mwelewa na akubali jukumu la kulea.
 
EMTanaweza kutusaidia, labda rate ya gawio la mwezi imepanda. Kuna wakati wanaangalia pato la baba pia, refer kesi ya Mahita na kijana wake.
 
Last edited by a moderator:
Nenda ofisini kwao, watamuita na kumuhoji baadhi ya maswali ili wajilidhishe kama kweli mtoto ni wake na kama ameajiriwa.
Kama atakana mtoto si wake, watakuambia uende mahakamani, huko watatoa amri ya kupima DNA.
Kama atakubali mtoto ni wake na ameajiriwa, watajadili nae ( matumizi ya mtoto kwa mwezi uliyo ambatanisha kwenye fomu) na wewe ukiwepo.
Muafaka wa mjadala huo utapelekwa kwa muajiri wake, atakuwa anakatwa kiasi cha Fedha mlizokubaliana kila mwezi na zitaingizwa katika akaunti yako ya banki, kwa muda wote atakapokuwa kazini mpaka mtoto afikishe miaka 18. Unaweza kuongeza madai zaidi kadri mtoto anavyokua.
Angalizo: hakikisha mtoto kweli ni wake, na huna ajira. Vinginevyo utajikuta unamlipa gharama za mahakamani na fidia za kupotezea muda wake na kumchafulia jina kwa jamii.
 
Habari zenu jamani poleni na majukumu.

Mimi naombeni kuuliza utaratibu wa ustawi wa jamii unakuaje kama unataka baba wa mtoto atunze mtoto je?

1)Vitu gani wanaangalia na inakuwaje?

Samahani kwa anayejua naombeni mnijuze nitashukuru.

kweli no one is above the law yaan mjitu unakuzalishahautumi matumizi? sion raha ya kuolewa bora niishi sigle
 
Mwajiri mara nyingi hushughulika na mke wa ndoa, sasa kama si mke ataendaje kwa mwajiri?

Hasa kama ukute mwanamme huyu ana mke tayari?

 
Kongosho, hujanielewa vema. Nimesema kule kazini kwa baba wa mtoto itapelekwa barua tu, tena na wao wenyewe (ustawi wa jamii) hakuna mahali nimesema mama wa mtoto aende kwa muajiri wa baba wa mtoto.
Pia swala la kumlea mtoto, kisheria haijalishi kama mmeoana au la, hata kama mzazi mmoja kaoa/olewa kwingine. Kinachohitajika ni uthibitisho tu, kama kweli mtoto ni wake.
Pia hata mzazi wa kiume ikiwa hana kazi na anaishi na mtoto, wakati mama wa mtoto ameajiriwa, baba wa mtoto kisheria anaweza kudai fedha za matumizi ya mtoto kutoka kwa mama wa mtoto. Jukumu zima la kumlea mtoto ni la baba na mama.
 
Narudi, tena nitafurahi nikipata vifungu.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…