Naombeni msaada wetu kwa huyu Mgonjwa

Naombeni msaada wetu kwa huyu Mgonjwa

proxy

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
1,481
Reaction score
1,356
Hello ,habari za muda huu wa Jf. Nije moja kwa moja kwenye mada. Nina jilani yangu mwenye umri Karibu kama mama yangu.

Toka mwaka jana mwezi wa 10 alianza kuugua, kwa mala kadhaa alikua anapata matibabu kwenye hospitali ndogo ndogo kama za wilaya na zahanati.

Mwaka huu mwezi wa pili walifanikisha kumpeleka kwenye hospitali kubwa (rufaa) na kugundulika kuwa mama ana kansa ya kizazi ,kwa sasa hali Yale ni kutokwa na maji yenye harufu ukeni na kushindwa kutembea ,na mala nyingine kushindwa hata kuamka.

Hospitali wamempa rufaa ya kwenda Ocean Road kwenye hospitali yenye kitendo mahususi kwa kansa.Kwahiyo baada ya kutoka majibu ndugu( watoto wake) wamechanganyikiwa kwa hali ya mpendwa wao lakini pia namna ya kumfikisha huko Ocean road.

Binafsi niliwashauri wafanye mpango wamfikishe huko kwa kujalibu kuchanga yani sisi majilani na ndugu wengine ,lakini inavyoonekana kama ndugu wamekata tamaa kwa hali aliyokuwanayo mgonjwa lakini pia hali ya kiuchumi waliyokuwanayo hivi sasa.

Nimeandika kwa uchungu kwa sababu mama namfahamu na hali yake kwa sasa sio nzuri kwa kweli. Nimeandika hapa ili kuweza kupata ushauri lakini pia tunaweza kuwashauri hawa ndugu zetu ni kwa namna gani wanaweza kufanya ili kumsaidia mpendwa wao.

Na kama kuna mtu anaweza kuwa na mchango wa mawazo kwa namna anavyoufahamu ugonjwa huu basi itasaidia sana na tutashukuru pia.Natanguliza shukrani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda useme unataka Mchango wa Pesa lakini Mchango wa Mawazo juu ya Ugonjwa huo upo kwa Madaktari Ocean Road, kama amepata Rufaa mnasubiri nini kumfikisha kwa Wataalam?? Mambo ya Pesa mtajua huko huko muhimu Mgonjwa aonane na Matabibu.
 
Labda useme unataka Mchango wa Pesa lakini Mchanga wa Mawazo juu ya Ugonjwa huo upo kwa Madaktari Ocean Road, kama amepata Rufaa mnasubiri nini kumfikisha kwa Wataalam?? Mambo ya Pesa mtajua huko huko muhimu Mgonjwa aonane na Matabibu.
Oky sawa ,mimi ni jalani niliyeguswa na hili tatizo ndugu ,nashukuru kwa mchango wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu, ebu sikilizahii kitu kwa umakini kabisa
 
Attachments

  • VID-20220330-WA0009.mp4
    3.6 MB
Mi kwa ninavyojua, cancer ina stage, kama kafikia stage 4 basi ni suala la muda tu lazima itamchukua kwenda makazi ya milele..
Labda itumike mbinu ingine eg maombi
Ila kama ni stage 4 hata ocean road wataenda kumpa huduma ya kujiandaa na kifo.
Ahsante
 
Mpeleke Ocean road, Ocean road huduma za kuwaona madaktar na vipimo vyote ni bure changamoto ni dawa unalipia. Swala la dawa km Hamna uwezo nayo kuna kitengo hapo mtafikisha Ombi lenu watawasaidia vilevile kuna watoa misaad wengi hapo Ocean road kama mna Nia mgonjwa wenu atapata huduma.

Swala la cancer imefika stage ngapi isiwatishe Kama wadau walivosema hapo juu tambua kila binadamu ni marehemu mtarajiwa unaweza kufa mzima mgonjwa WA cancer ukamuacha na cancer yake anapambania uhai wake. Pambaneni huyo mama apate dawa za kumpunguzia maumivu kila la kheri.
 
Huu ugonjwa acha tu,jana tu kafari jilan yangu
 
Nashukuru kwa mchango wa mawazo yako ndugu ,ubarikiwa

Nakazia

Aende Ocean Road Hospital
Nina Ndugu Yangu Alikuwa KCMC Kwa Huduma Baadaye Aliambiwa Lazima Aende Dar Es Salaam Na Kwasasa Anaendelea Na Tiba Na Mwezi Huu Atamaliza Na Kuambiwa Kinachofuata Iwapo Arejee Home
 
Mpeleke Ocean road, Ocean road huduma za kuwaona madaktar na vipimo vyote ni bure changamoto ni dawa unalipia. Swala la dawa km Hamna uwezo nayo kuna kitengo hapo mtafikisha Ombi lenu watawasaidia vilevile kuna watoa misaad wengi hapo Ocean road kama mna Nia mgonjwa wenu atapata huduma.

Swala la cancer imefika stage ngapi isiwatishe Kama wadau walivosema hapo juu tambua kila binadamu ni marehemu mtarajiwa unaweza kufa mzima mgonjwa WA cancer ukamuacha na cancer yake anapambania uhai wake. Pambaneni huyo mama apate dawa za kumpunguzia maumivu kila la kheri.
Ocean Road wanafanya kazi siku za Jumapili?
 
Back
Top Bottom