Naombeni msaada wenu jamani kwa atakaeguswa ili nipate kumlipa huyu mwenye nyumba hela yake

solanum

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
203
99
Habari zenu wakuu,


Mimi nimepatwa na shida, ni hivi mimi nimelelewa na mama bila baba. Baba yangu alifariki mnamo mwaka 1992 nikiwa bado mdogo sana, mama yangu amejitahidi kunilea huku akijishughulisha na kulima vibarua kwenye mashamba ya watu na kufanikiwa kunisomesha mpaka kidato cha nne, nilipomaliza kidato cha nne nilifanikiwa kufaulu na kuendelea kidato cha tano.

Mama yangu alikuja Dar es Salaam kufanya kazi za ndani kwa wahindi japo alikua akilipwa mshahara mdogo sana lakini alijitahidi kunisomesha mpaka nimemaliza kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu kwenda chuo nashukuru nilipata mkopo kiasi nikajibanabana mpaka nimemaliza chuo mwaka 2015 novemba.

Nikaanza kutafuta kazi sehemu mbalimbali lakini ilipita miezi minne bila kupata kazi, nikapata wazo la kufungua genge kwakua nilikuwa na hela kidogo. Nikafungua genge na kuanza kuuza matunda, viungo mbalimbali na nafaka huku nikiwa nimepanga chumba changu.

Ilipofika mwezi wa tisa mwaka jana niliumwa sana na kushindwa kuendelea na biashara yangu ya genge. Nimetumia muda wangu mwingi kujiuguza na pesa nilizokua nazo zote zimeishia kwenye matibabu na chakula nimebaki sina kitu hela ya kula yenyewe naipata kwa shida.

Sasa huyu mwenye nyumba niliyopanga amenivumilia mpaka sasa ni miezi mitano imepita sijamlipa hela yake sasa ananidai hela yake nimlipe Tsh 150,000/= na mimi sina kitu na nipo njia panda kwakweli.

Naombeni msaada wenu jamani kwa atakaeguswa ili nipate kumlipa huyu mwenye nyumba hela yake. Namba zangu 0758 106 501. Mungu awabariki sana, Ahsanteni!
 
Nadhani ungetaja jinsia yako mkuu..! huenda ungepata msaada wa haraka zaidi..!
Maana naona umepost about 40 min ago, viewers about 40, but no reply..!
 
Habari zenu wakuu,


Mimi nimepatwa na shida, ni hivi mimi nimelelewa na mama bila baba. Baba yangu alifariki mnamo mwaka 1992 nikiwa bado mdogo sana, mama yangu amejitahidi kunilea huku akijishughulisha na kulima vibarua kwenye mashamba ya watu na kufanikiwa kunisomesha mpaka kidato cha nne, nilipomaliza kidato cha nne nilifanikiwa kufaulu na kuendelea kidato cha tano. Mama yangu alikuja Dar es salaam kufanya kazi za ndani kwa wahindi japo alikua akilipwa mshahara mdogo sana lakini alijitahidi kunisomesha mpaka nimemaliza kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu kwenda chuo nashukuru nilipata mkopo kiasi nikajibanabana mpaka nimemaliza chuo mwaka 2015 novemba. Nikaanza kutafuta kazi sehemu mbalimbali lakini ilipita miezi minne bila kupata kazi, nikapata wazo la kufungua genge kwakua nilikuwa na hela kidogo. Nikafungua genge na kuanza kuuza matunda, viungo mbalimbali na nafaka huku nikiwa nimepanga chumba changu. Ilipofika mwezi wa tisa mwaka jana niliumwa sana na kushindwa kuendelea na biashara yangu ya genge. Nimetumia muda wangu mwingi kujiuguza na pesa nilizokua nazo zote zimeishia kwenye matibabu na chakula nimebaki sina kitu hela ya kula yenyewe naipata kwa shida. Sasa huyu mwenye nyumba niliyopanga amenivumilia mpaka sasa ni miezi mitano imepita sijamlipa hela yake sasa ananidai hela yake nimlipe Tsh 150,000/= na mimi sina kitu na nipo njia panda kwakweli. Naombeni msaada wenu jamani kwa atakaeguswa. Namba zangu 0758 106 501. Mungu awabariki sana, Ahsanteni!
 
Haya mambo nilishasema JF tuanzishe mfuko wa kusaidiana ambapo kwa mwezi ni mia tano tu kwa kila member hapa, lakini hakuna mwendelezo, hakuna hata faida ya jukwaa zaidi ya kuchart basi, shilingi mia tano kwa kila member tungeweza hata kuanzisha bank yetu wenyewe na watu wakakopa. Mtaji tunao ambao ni watu lakini hatuna mtu wa kucoordinate.
 
Haya mambo nilishasema JF tuanzishe mfuko wa kusaidiana ambao kwa mwezi ni mia tano tu kwa kila member hapa, lakini hakuna mwendelezo, hakuna hata faida ya jukwaa zaidi ya kuchart basi, shilingi mia tano kwa kila member tungeweza hata kuanzisha bank yetu wenyewe na watu wakakopa. Mtaji tunao ambao ni watu lakini hatuna mtu wa coordinate.
sisemi anadanganya, but can you assure us he isn't?
 
Back
Top Bottom