ZOPPA
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 2,729
- 2,891
Terehe 1/1/2017 saa sita usiku nilipigwa mapanga na jirani yangu sababu tulikuwa tunasherekea mwaka mpya. Mtuumiwa baada ya kunijeruhi alikimbilia kwa mwenyekiti na kuripoti amevamiwa kitu ambacho si cha kweli.
Kwanza mtuhumiwa hakunipigia nyumbani kwake amenipiga mapanga njiani nyumba ya pili kutoka kwake. Mimi baada ya kuumia tulienda kuripoti kwa mwenyekiti kabla yake, baada ta hapo tulienda polisi kuchukua PF3 kwa ajili ya matibabu. Mtuhumiwa alikimbia pasipojulikana, baada ya week mbili alirudi nyumbani kwake kwa kubeep. Tulipoenda na polisi mpelelezi hatukufanikiwa kumuona mtuhumiwa.
Siku inayofuata mtuhumiwa alijipeleka polisi na ndugu zake. Yule polisi mpelelezi akanipigia simu mtuhumiwa amejileta kesho njoo polisi. Siku inayofuata nikaenda, cha ajabu nikagundua mtuhumiwa na polisi ni marafiki. Siku moja baada ya kukamatwa mtuhumiwa tukaambiwa twende mahakamani tukaenda. Mtuhumiwa amekataa na kusema hakunijeruhi, mahakama imenianbia niende na mashahidi.
Je nifanye nini ikiwa mtuhumiwa janja janja. Naombeni mawazo yenu wakuu!