Naombeni msaada: Uso wangu upo rafu sana, nina mba sana na nimeshatumia antifungal creams za kila aina

Kidawa_hiphop

Senior Member
Jul 7, 2018
168
254
Uso wangu upo rafu sana..nina mba sana na nimeshatumia antifungal creams za kila aina ila bado mambo bado,hata za kumeza pia kama fluconazole,itraconazole lakini mba unaisha na uso unakaa vizuri kwa siku chache tu mba wanarudi tena kwa kasi ya ajabu.

Wakuu mwenye experience ya hii shida aliitibu vipi naomba msaada tafadhali.Nakosa kabisa confidence kisa ya uso wangu kuwa rough.Sehemu nyingine sina mba au fangasi wowote.
 
Mods please naomba msiunganishe huu uzi..unganisheni nikishapata suluhu.

Uso wangu upo rafu sana..nina mba sana na nimeshatumia antifungal creams za kila aina ila bado mambo bado,hata za kumeza pia kama fluconazole,itraconazole lakini mba unaisha na uso unakaa vizuri kwa siku chache tu mba wanarudi tena kwa kasi ya ajabu.

Wakuu mwenye experience ya hii shida aliitibu vipi naomba msaada tafadhali.Nakosa kabisa confidence kisa ya uso wangu kuwa rough.Sehemu nyingine sina mba au fangasi wowote.
Mkuu Kidawa_hiphop, tatizo lako yawezekana linalotokana na mchafuko wa damu kwa sababu ya matumizi ya vipodozi na vyakula vinavyochafua damu. Unatakiwa kuchukua majani ya muarobaini na kuyachemsha vizuri kisha kunywa maji yake kikombe cha chai kutwa mara 2 kwa siku 5.

Ili kuondoa mabaka kama chunusi unahitaji kuandaa vitu vifuatavyo:
(i.) Unga wa manjano
(ii.) Aloe vera
(iii.) Mafuta ya nyonyo (castor oil)
(iv.) Mafuta yq mgando (Pure Petroleum Gelly)

Saga kiasi kidogo cha Aloe vera. Kisha weka unga kidogo wa manjano kwenye hiyo aloe vera uliyoisaga na koroga vizuri. Kwenye huo mkorogo weka mafuta ya nyonyo na ukoroge vizuri. Yeyusha mafuta ya mgando na uyamiminie kwenye mchanganyiko wako kisha koroga vizuri kabisa. Uchuje mchanganyiko huo na uweke kwenye kopo la kuhifadhia na uache mafuta yako yagande. Baada ya hapo dawa yako itakuwa tayari kwa ajili ya matumizi. Osha uso wako vizuri kabisa kwa maji ya kwaida kisha pakaza mafuta hayo kutwa mara mbili kwa wiki 2.

Wakati unatumia dawa hiyo huruhusiwi kabisa kula vvyakula vifuatavyo ambavyo husababisha kuchafuka damu:
i. Vyakula ambavyo hujapika wewe au mtu unayemuamini, mfano usile kwa mama ntilie, migahawani, hotel na sehemu nyinginezo kama hizo.
ii. Usile vyakula kutoka kiwandani kama soda, juice, bia, mikate, maandazi, chapati, biscuit, na vingine vingi vinavyotengenezwa viwandani.
iii. Usile vyakula vyote vitokanavyo na wanyama au maziwa
iv. Usitumie dawa za kutuliza maumivu, dawa za presha, au sukari
v. Usile chakula baada ya saa 2 usiku.
vi. Usile virutubisho
vii. Usitumie sukari au glucose.

Nasubiri mrejesho.
 
Umri wako,Jinsia yako,Umeoa au kuolewa? Maswali muhimu kabla ya Tiba.
 
Nenda maduka ya madawa jaribu huko kuulizia dawa za mba au maduka ya urembo pia wanauza dawa za mba. Usichoke jaribu dawa mbali mbali za kupaka utapona tu
 
Unamchafuko wa damu so fanya hivi, chukua mchunga (wild lettuce) ni mboga chemsha na kunywa maji yake kwa siku mara tatu.
Pia chukua majani ya huu mchunga ya kate kate vipande vidogo na yachanganye na maji yako yakuoga yaache kwa mda usiopungua nusu saa kisha oge hayo maji kwa siku saba. KWA NEEMA YA MUNGU UTAPONA
Hii pia ni tiba ugonjwa wa "tetekuwanga"

NB: Ni chungu hivyo vumilia pia waweza kula kama mboga hakikisha unakunywa maji yake ya kwanza sio venginevyo.
 
Back
Top Bottom