Town Hustler
JF-Expert Member
- Oct 25, 2016
- 277
- 367
- Thread starter
-
- #21
Watt 20 ni panel ndogo sana mkuu kwa matumizi ya taa 5, na kuchaji simu, mimi nakumbuka nilipeleka panel ya watt 20, matumizi ni taa moja tu na kuchaji simu wakati wa mchana pekee, mpaka sasa ni mwaka wa tattu halijatokea tatizo. Sana sana ni siku za mvua ndiyo huwa kuna nguvu kidogo
Kwakweli sifahamu bei yake, labda wadau wanaodeal na uuzaji wa solar watatujibu.Bei zake zipoje mkuu
Kwakweli sifahamu bei yake, labda wadau wanaodeal na uuzaji wa solar watatujibu.
Kwa suze ya solar yako itakuwa 25000 mpaka 30,000Bei zake zipoje mkuu
Ahsante mkuu.......Kwa suze ya solar yako itakuwa 25000 mpaka 30,000
Hii inawasha nini au ina uwezo wa kutumia vitu gani kwenye nyumba...?Wapigie namba hii 0800 75 2222. Kupiga ni bure. Huo mtambo kwa mfano kama wangu unalipa 72,000 wanakuja kukufungia iliyobaki unalipa kidogokidogo 29,000 kwa mwezi au 1,000 kila siku kwa mpesa au tigopesa. Ni kama LUKU usipolipa umeme unakatika. Lakini mitambo yao ni imara. Njoo PM ukifanikiwa unipe mrejesho
...Hii inawasha nini au ina uwezo wa kutumia vitu gani kwenye nyumba...?
Shukrani mkuuMimi nina utaalamu wa kudesign mfumo wa solar PV.
Vitu vikubwa katika mfumo wa solar PV ni PV module, solar charge controller, inverter, battery bank, auxiliary energy sources and loads (appliances).
Sasa tuanze step by step (step ziko 5)
Kudesign mfumo wa solar
Step ya 1.Nguvu inayotumika katika mahitaji yako.
Jumla ya matumizi ya vifaa vyako= taa 2 kila moja 3W ukiziwasha masaa 13/siku hapa nime assume umewasha saa 1 jioni hadi kesho yake saa1 au2 asubuhi ndio kuzizima
Taa 2 @3W masaa 5/siku hapa nime assume ukiwasha saa 1 ukazima saa tano usiku maana umesema unazima mbili unaacha mbili na kuchaji simu maximum nguvu inayotumika 5W kwa masaa 3 kwa siku(kwa smartphone)
Sasa
Taa 2 X 3W X13hrs/day =78Wh/day
Taa 2 X 3W X 5hrs/day = 30Wh/day
Kuchaji simu moja X 5W X 3hrs/day = 15Wh/day
Jumla ya matumizi yako= 123Wh/day
Nguvu ya jumla inayohitajika kwenye PV paneli= 123 X 1.3 = 159.9Wh/day say 160Wh/day
Step ya 2. Size ya PV paneli
Jumla ya Wp za uwezo wa PV paneli zinazohitajika= 160/3.4 =47.1Wp
Idadi ya PV paneli zinazohitajika = 47.1Wh/20= 2.4 paneli
Zinazohitajika sahii =3 modules
Kwa io mfumo wako huo unatakiwa upate nguvu kwa kutumia paneli 3 za 20Wp ambapo 3X20Wp = 60 Wp.
hahahaha nimechoka kutype step ya 3 hadi ya 5
tuishie hapo
Kama taa zako au vifaa vyako ni vya DC huna haja ya invetor. Ila kama una vifaa vya AC ndio utahitaji.Shukrani mkuu
Nitafunga betri mpya na controller na taa za nje nitabadili na kuweka za 1W
Inventor ndio kifaa gani
Sawa mkuu hakikisha unafuata yale mahesabu ya kudesign mfumo ili isije kusumbua tenaShukrani mkuu
Nitafunga betri mpya na controller na taa za nje nitabadili na kuweka za 1W
Inventor ndio kifaa gani
Mkuu sijakuelewa vifa vya DC & AC maana yake niniKama taa zako au vifaa vyako ni vya DC huna haja ya invetor. Ila kama una vifaa vya AC ndio utahitaji.
Inverort kazi yake ni kubadili umeme wa DC kwenda AC.
Sawa mkuu nitajitahidi kuwa na nidhamu ya matumiziSawa mkuu hakikisha unafuata yale mahesabu ya kudesign mfumo ili isije kusumbua tena
Kuna vifaa vinavyotumia umeme wa TANESCO hivyo ni AC. Vifaa vinavyounganishwa kwenye betri moja kwa moja hizo ni DCMkuu sijakuelewa vifa vya DC & AC maana yake nini
Ahsante kwa ufafanuziKuna vifaa vinavyotumia umeme wa TANESCO hivyo ni AC. Vifaa vinavyounganishwa kwenye betri moja kwa moja hizo ni DC
kwenye mfumo wetu wa sola kuna Inveta hii inavonvert DC TO AC.
Betri ya N100 ni sawa na 12V ......AH ngapi ?hiyo ni Inveta ya juu.
Ya chini ni betri ya N100.
JUU NINA PANEL YA W200