Naombeni msaada kurudi bongo

Njoo tu mzee ila hayo maisha uliyoenda kuyatafuta usisahau kuyabeba uje nayo hata kama nauli itapungua upunguze uzito wa kilo. Ukija bila bila ukayaacha hayo maisha shauri yako, ukifika bila hayo maisha siku ya kwanza ya pili chali rip.
 
Sikati vitunguu wala maboxi. Naendesha mabasi ya mjini. Kama UDA ya zamani.
Endelea tu kukaa huko huko mkuu ilimradi unakibarua sio mbaya komaa huko huko, huku bongo nyoso hapafai aisee, kwa hiyo pesa yako utatumia kipindi kifupi , Kisha utaanza kujuta nimerudi kufanya nn.
 
Kaa hukohuko umeshiba, haujarudi unaanza kukiponda chakula chetu eti huwezi kula nafaka! Eti huwezi kupanda madaladla! Bora ufie hukohuko utakuja kutusumbua.
 
Ni suala la muda tu!

We unadhani ukila nafaka unapata kisukari hpo hpo?

Ni mchakato wa muda mrefu! Unaweza fikisha miaka 45 then effect za kula nafaka mfulululizo ndyo zinaonekana
Mkuu nimeacha kula ugali na wali mwezi wa tatu sasa kama strategy ya kupunguza uzito kwa hiyo unanishauri nisirudi huko kabisa?
 
We jamaa wewe yaani uje na dolar 1800 sijui hata ni dola za wapi halafu uishi comfortably !!! (eti siyo kula nafaka,kutotumia madaladala. Huku sasa wewe ni babu unapaswa kukaa na kucheza na wajukuu- Ukija na hiyo hela madaladala na nafaka vinakuhusu sana. Ila karibu nyumbani unaweza endesha magari ya mwendo kasi
 
Mziki wa kiume
Mkuu, tulia tu huko huko na hizo dola buku na mianane zako, maisha yamebadilika sana sana mambo yanaenda kasi sana tangu 1992, wewe endelea kukata vitunguu na kubeba mabox huko, game ya TZ ni mziki mwingine.
 
Unarudi bongo na pesa ya kulia mihogo halafu unachagua chakula, eti sili nafaka
 

Akirudi kijijini kule hakuna daladala kutamfaa na maziwa ni mengi sana bila kusahahu mnafaka hakuna atakula vizi na ndizi.
 
Sasa kazi unayo si uendelee na maisha maana kwa masharti yako utaishia kunywa sumu tu,

Eti sitaki kula nafaka, very pathetic.
Huyo anawatania dereva anayeendesha Basi kama UDA analipwa £500 kwa wiki bado overtime. Na nyumba kodi 75 kwa wiki ya serikali na binafsi ni 100 asiwapotezee muda
 
kunywa maziwa, kulala pazuri, kutotumia madaradara kwa usafiri, kula chakula nzuri (siyo kula nafaka).

Mkuu ukiconvert hiyo dollar 1800 kwa exchange ya 2300 utapata kama 4,140,000/= ambayo ni sawa na mishahara ya miezi minne ya watumishi wa kawaida hapa bongo. daladala inakuhusu mkuu kwa pesa hiyo ukinunua bodaboda utashindwa kulipa kodi ya nyumba. Pole sana mkuu jichange angalau uje na dolla elfu kumi
 
Kwa hiyo unakaribia familia sasa unawaacha watoto na nani?
 
Aisee usirudi tena usithubutu njoo na huu Uzi 2021 January tutakwambia maana huku Maskini anafanyakazi kama punda na anakula kama Panya lakini Tajiri anafanyakazi kama Punda hata kula hali..........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…