kiraia
JF-Expert Member
- Nov 20, 2007
- 1,716
- 999
Ndugu zangu wanaJF nimewahi kushikwa mara mbili na Polisi wa usalama barabarani mara ya kwanza kwenye mataa ya Maktaba na mara ya pili katika kituo cha karume, Niliposhikwa mara ya Kwanza nilipelekwa kituo cha Sarrender Bridge nikalipishwa faini ya 20,000 nilipouliza risiti nikapewa kopy ya Karatasi niende central polisi kwa ajili ya kuandikiwa risiti, na hata niliposhikwa mara ya pili pale Karume walifanya hivyo hivyo na kuniambia niende Msimbazi ndio naweza kupewa risiti kwa masharti ya kuacha funguo ya gari, swali langu ni kwa nini wanachukua pesa wakati hawana risiti? Je ni kweli kuwa hawana risiti au ni mchezo mchafu?