Naombeni msaada jinsi ya kumpata mtoto wangu

The patriot man

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
968
1,064
Wakuu habari zenu

Niende direct to the point ilikua ni mwaka 2016 nilikua mkoa wa kilimanjaro nafanya project moja pale moshi mjina nikakutana na binti mmoja mzuri saana nikamtongoza akakubali alaikua anasoma chuo cha ushirika moshi kwa sababu pale mimi nilikaa kwa mda wa miezi 8 akaja akahamia kwangu tukawa tunaishi wote kama mke na mume tulikua tunazini bila kinga siku za kukaribia kurudi zikaisha nikamuambia mimi nakaribia kuondoka ila tutakua pamoja akanisihi sana nikae pale nikamuambia no haiwezekani .

Basi bwana nikikwa dar mwezi wa 4 akanambia ana mimba yangu nikamuambia siko teari kulea akanambia wewe mwanaume ni shetani unakataa kiumbe chako nikajitetea ila hakunielewa akaniblock kila mahali na namba akabadilisha .Mimi nilidhani ananitania.
siku zikaenda miezi ikasogea hee siku moja nikapigiwa cm na Rafiki yake anambia ANNA(fiction name) amejifungua mtoto wa kiume mh nikapiga mahesbu siku ya mwisho mimi kukutana nae kimwili mpka alipokuja kujifungua daah nikawa 100% nahusika na ile mimba nikwa bado natafakari siku moja nimeingia whatsapp zikaingia pic za mtoto mdogo wa miezi kama 5 hivi kuzifungua vizuri daah copy yangu kabisaa.

Nikapiga ile namba akapokea x wangu akanmbia ulimkataa mtoto je huyo mtoto sio wako ikabdidi niwe mpole maana dogo kani copy Kila kitu akanmbia yule mtoto kampa mwanaume mwingine na sitokaa nimuone na nisimzoee akaniblock tena. na Ameolewa na mwanaume mwingine na Anaishi nae na hyo mtoto teari kashapewa jina la baba mwingine naumia sana.

wakuu naombeni msaada jinsi ya kumpata mwanangu
 
Kwa hiyo ulitaka wanaume wenzio walelee mimba kisha wewe ukachukue mtoto kiulaini tu? afadhali kama ungekuwa hujui lolote kumbe ulishaambiwa mapema kuwa anamimba yako ukasema kuwa hauko teyari sasa unakuja hapa kulia nini? ngoja wanaume wenzako wanaojua thamani ya utu walee, tena shukuru mungu huyo mwanamke alikutumia hata picha za mtoto ili akuumize zaidi, ilitakiwa wala usijue jinsia ya mtoto.
 
wee hauko serious kabisa......yanii badala ya kwenda mtafuta physically wewe unamvizia kwenye simu...kama ni wachagga mkuu.....nakushauri ni bora utafute mtoto mwingie huyo sahau kabisa
 
Ee kaka pambana tu na hali yako,sina cha kukusaidia,na Anna alikutumia picha kukuumiza kisaikolojia.
Hongereni wanaume wenye moyo kama mume wake Anna
 
Kwanza wewe si ulikujaga na post hapa kuwa ulikuwa na mpenzi unampenda sana akakusaliti na kapewa mimba juu.(someone tell me if karma has a menu)
Naona yamekukuta unakumbuka kiumbe ulichokikataa tokea tumboni,hivi unajua umemtengenezea mtoto roho ya kukataliwa?
 
Kwanza wewe si ulikujaga na post hapa kuwa ulikuwa na mpenzi unampenda sana akakusaliti na kapewa mimba juu.(someone tell me if karma has a menu)
Naona yamekukuta unakumbuka kiumbe ulichokikataa tokea tumboni,hivi unajua umemtengenezea mtoto roho ya kukataliwa?
yeap ni kweli mkuu ni nilishawahi kulear hii thread ya namna hyoo.
 
We jamaa weewe! kwahiyo hapo shida yako umharibie ndoa yake au? Umeikataa mimba ila mtoto unamtaka!?

Na hapo bila huyo mama wa mtoto kukusamehe mkayamaliza utabaki na maumivu siku zote. Shirikisha wazazi wenu wa pande zote wawasaidie kuyasuluhisha na unatakiwa kuomba radhi haswaaaa
 
Vp kwani watoto kiunoni wameisha ama?km wapo piga moyo konde tafuta mwingine huyo akikua ataujua ukweli
 
wee hauko serious kabisa......yanii badala ya kwenda mtafuta physically wewe unamvizia kwenye simu...kama ni wachagga mkuu.....nakushauri ni bora utafute mtoto mwingie huyo sahau kabisa

Wachaga huwa wanafanyaje Mkuu... Kwa scenario kama hii...fafanua zaidi kidogo Mkuu...

Asante
 
Humekuja humu kufanya nn sasa, tambua hunachako baba si ulikataa mwenyewe alafu sasa nimetoa copy ndo wako! Pu**mba**fuuu kabisa wewe Na bado dunia duara!!Huyu alikuwa wako original.....sasa bas tegemea kuletewa ambao si wako.
 
Back
Top Bottom