Habari zenu wakuu,
Mimi nimepatwa na shida, ni hivi mimi nimelelewa na mama bila baba. Baba yangu alifariki mnamo mwaka 1992 nikiwa bado mdogo sana, mama yangu amejitahidi kunilea huku akijishughulisha na kulima vibarua kwenye mashamba ya watu na kufanikiwa kunisomesha mpaka kidato cha nne, nilipomaliza kidato cha nne nilifanikiwa kufaulu na kuendelea kidato cha tano. Mama yangu alikuja Dar es salaam kufanya kazi za ndani kwa wahindi japo alikua akilipwa mshahara mdogo sana lakini alijitahidi kunisomesha mpaka nimemaliza kidato cha sita mwaka 2012 na kufaulu kwenda chuo nashukuru nilipata mkopo kiasi nikajibanabana mpaka nimemaliza chuo mwaka 2015 novemba. Nikaanza kutafuta kazi sehemu mbalimbali lakini ilipita miezi minne bila kupata kazi, nikapata wazo la kufungua genge kwakua nilikuwa na hela kidogo. Nikafungua genge na kuanza kuuza matunda, viungo mbalimbali na nafaka huku nikiwa nimepanga chumba changu. Ilipofika mwezi wa tisa mwaka jana niliumwa sana na kushindwa kuendelea na biashara yangu ya genge. Nimetumia muda wangu mwingi kujiuguza na pesa nilizokua nazo zote zimeishia kwenye matibabu na chakula nimebaki sina kitu hela ya kula yenyewe naipata kwa shida. Sasa huyu mwenye nyumba niliyopanga amenivumilia mpaka sasa ni miezi mitano imepita sijamlipa hela yake sasa ananidai hela yake nimlipe Tsh 150,000/= na mimi sina kitu na nipo njia panda kwakweli. Naombeni msaada wenu jamani kwa atakaeguswa. Namba zangu 0758 106 501. Mungu awabariki sana, Ahsanteni!