Naombeni mnisaidie mwenzenu naogopa kuoa

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Sijasomea Saikolojia ila naamini hizi ni dalili za "psychological disoder" Tangu nilipokuwa mdogo nilitamani sana siku moja nipate mwanamke atakayenielewa na mimi kumuelewa tuanzishe familia ila kadri umri wangu unavyozidi sogea nazidi poteza interest na ndoa maana nayoyaona kwenye ndoa yanatisha kama nini

Kila kunapoitwa leo najuta kuijua dunia na ulimwengu wa mahusiano maana ni mchungu kuionja na unachoma masikio na moyo.

Kuna X wangu mmoja ameolewa ila huwezi amini jana amenitafuta anasema ati amenikumbuka sana anatamani tukutane lodge fulani kuna kitu anataka nambia. Nimejifikiria sana usiku kucha sijalala nawaza huyu mdada kapata wapi ujasiri wa kutaka kumsaliti mmewe; mwanaume aliyemsomesha na kuwajengea nyumba kwao?

Tuachane na X wangu. Juzi kati nimeenda kumtembelea Soudy rafiki yngu anayefanya kazi lodge flani hapa Magomeni Mapipa. Nilichokishuhudia kimenifanya nichukie wanawake na ndoa.

Nimeshuhudia kwa macho yangu wanawake za watu wanapishana kwenda kuliwa chap na haraka. Kuna wengine wanakuja na vikapu wanaviacha reception. Inasikitisha sana.

Kilichoniuma zaidi nimemuona baba mdgo kaingia na malaya flani hvi huwa anajiuza pub ya jirani. Dunia imefika mbali sana. Kumbukeni baba yangu mdgo ni mchungaji msaidizi kanisani.

Nimeogopa kuoa...maana ntakapooa hizi taswira nilizoziona zitaknitesa sana niwapo ndoani.

Naombeni msaada wa kisaikojia ndugu zangu.

Asanteni
 
Sasa unataka tukusaidie nini? Kukupunguzia huo uoga ulioko akilini mwako, ili uweze sasa kuoa, au!!

Halafu huko lodge ukienda kweli kumtembelea huyo rafiki yaki Soudy, au ulienda kuchunguza maisha ya watu? Binafsi sijawahi kamwe kuwafagilia watu wenye tabia na hulka kama yako.
 
Sasa unataka tukusaidie nini? Kukupunguzia huo uoga ulioko akilini mwako, ili uweze sasa kuoa, au!!

Halafu huko lodge ukienda kweli kumtembelea huyo rafiki yaki Soudy, au ulienda kuchunguza maisha ya watu? Binafsi sijawahi kamwe kuwafagilia watu wenye tabia na hulka kama yako.
Sio kila tatizo unaweza kutatua. Kama hujaelewa tulia. Soma comments utaelewa bdae
 
usikariri wanawake wote hawafanani na ndoa zote hazifanani, kuna watu wana enjoy ndoa mpaka wanaona walichelewa kuoana,amini utapata wa kufanana na wewe
 
Back
Top Bottom