Kwanini hutakiwi kuendeleza mahusiano na mpenzi wako wa zamani kama alikuacha na kuoa mwanamke mwingine?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
Kama mwanaume alikua anakupenda, lakini kwa sababu yoyote ile akakuacha na kwenda kuoa mwanamke mwingine. Dada yangu acha kujidhalilisha kwa kuendelea kutoka na yule mwanaume, iwe ni kwa kumkomoa aliyeolewa au ni kwa kujiambia kua “amekuoa wewe lakini bado ananipenda mimi”. Kujiambia kuwa moyo wake uko kwako, nikuambie tu moyo wake hauko kwako ndiyo maana hajakuoa, kilichobaki kwako ni mazoea tu ambayo anajaribu kuyamalizia.

Ndiyo mwanaume kama anakupenda kama unavyodhani au anakupenda kama alivyosema si ndugu zake wala dini ambavyo vitawatenganisha. Lakini hata tuseme anakupenda kweli kihivyo, unatakiwa kujua mambo makuu matano ambayo nataka usome kwa makini kabla ya kuendelea kujidhalilisha na kuruhusu utumie mwili wako kumfariji wewe, narudia najua bado unampenda, ungetamani mrudiane ila Dada yangu soma kwa makini mambo haya matano.

(1) Kilichobaki Ni Mazoea; Ndiyo kashindwa kukusahau kwakua mlishashea vingi, alikua mtu wako wa kupika na kupakua, kuna utamu anaukosa hivyo kwa huyu mtu mpya ambaye labda kachaguliwa na wazazi wake labda alimpa mimba ‘bahati mbaya’ lakini labda ni dini yake, bado hajakusahau, hajamzoea kama wewe alivyokuzoe hivyo anakua mpweka na anakuhitaji kwa muda ili aendelee kufurahia maisha wakati akimzoea huyu mwingine. Kwamba atajifanya kuwa anakupednda, atakujali na hata wakati mwingine atakua anakusikiliza wewe kuliko mkewe. Yaani utajiona kama wewe ndoiyo mke kabisa lakini anafanya hivyo huku akijifunza kumpenda mkewe, kumzoea na naamini kuwa siku akimzoea, akijifunza kumpenda, hutamuona tena utakua ukimsikia tu kwenye Radio, sasa usiniulize ni lini inaweza kuwa leo, mwakani au hata baada ya miaka kumi ila jua tu utaachwa!

(2) Majukumu Yakimzidi Atamchagua Mkewe; Ndiyo unaweza ona kuwa wewe ndiyo kila kitu kwake, ukaacha maisha yako na kuwa kama mke wake, akakujali kama mkewe. Ila kuna jambo moja ambalo litamkimbiza kwako na hilo ni jamaa mmoja anaitwa Majukumu, siku akiwa na watoto au watoto wakianza shule zile zenyewe, majukumu yakizidi atakukimbia. Ndiyo kama alishindwa kukuchagua wewe kwasababu wazazi wake hawakutaka unafikiri ataacha watoto wake wateseke kisa Mama yako ni mgonjwa. Anaweza kukununulia maua, kadi, underwear na braa za kutosha lakini siku ukihitaji msaada wa maana atachagua wanae na familia yake. Ataenda kumuomba mkewe msamaha atamsamehe na wewe utabaki na tundu la pili katika moyo wako, kwanza la kuachwa kama mpenzi na pili la kuachwa kama mchepuko.

(3) Mwanaume Hakatai Ugali Wa Bure; Najua unajiambia angekua hanipendi mbona anakuja kwangu, mbona nikimuambia namuacha anakasirika, mbona analia kabisa. Dada yangu kama amekuacha kaoa mwingine unatakiwa kujua kuwa mwanaume hawezi kukataa ugali wa bure. Ndiyo analia kwakua wewe ni mchapuko ambao anaupenda lakini pia ni mchepuko wa bei rahisi zaidi kulinganisha na ndoa yake.

Kwanza inawezekana hakuhudumii kitu cha maana, lakini anauhudumia ila sio kama mkewe, una kazi yako, lakini una maisha yako, hahudumii ndugu zako kama ndugu wa mkewe. Lakini anajua hata kama anahudumia anaweza kukuacha wakati wowote hivyo wewe ni kama ugali wa bure, unampa mapenzi tena kwa bei rahisi kabisa kwakua humchuni sana basi unahisi unapendwa, wewe endelea kugawa ugali tu atakula lakini haina uhusiano na mapenzi nikuwa tu mwanaume hakatai ugali wa bure.

(4) Humkomoi Mke Wake Na Mkewe Haondoiki; Moja ya kitu ambacho nimejifunza kutoka kwa wanawake wengi nikua nyie Dada zangu ni wabishi na wagumu kuondoka, mimi mke wangu nikisikia tu bado anaendelea kuchat na X wake anatumiana meseji za mapenzi nitakachofanya ni kumpakia kwenye gari na kwenda kumshusha kwa X wake kisha narudi nyumbani na fundi anabadilisha vitasa halafu naendelea na maisha.

Lakini kwa wanawake kumuacha eti kisa X anasumbua ni ndoto, kwanza likua anajua kua ulikuepo, mlikua manappendana sana na kubwa hata ulikua uolewe wewe hivyo ameingia kwenye ndoa anajua yeye si chaguo lako la kwanza, hivyo usifikiri kaingia kashaolewa, kasharingishia na kijijini kwao kua kaolewa na kuzalishwa kazalishwa halafu eti atoke kwakua wewe umeamua kuwa kahaba na kuendelea kugawa mwili wako bure.

Dada yangu si kwa hawa wanawake ninaowafahamu waliopambania ndoa miaka nenda rudi. Hivyo kama ulishindwa kumpata wakaati hajaoa yuko single basi sidhani kama utampata wakati kashafunga ndoa. Mkewe haondoki hivyo wewe endelea kutumika tu kama mashabiki wa Arsenal ambao wanasubiri kombe la UEFA, ukweli nikua Wenger haondoki na UEFA hamshindi, hivyo hivyo kwako mkewe haondoki na ndoa hupati tena, wewe jigawe tu.

(5) Unajizibia Riziki Nyingine/Unaharibu Maisha Yako; Labda hiki ni kama ushauri tu kwako Dada yangu, humkomoi mtu na unajizibia riziki nyingi, unaharibu maisha yako na hapa nitakuambia mambo matatu. Kwanza wewe mwenyewe unashindwa kupoana maumivu na kutafuta mtu mpya, uanaishi katika maisha ya matumaini labda atamaucha mkewe na miaka inenda hamuachi, hutafuti mwanaume mwingine na hujipi fursa ya kupenda upya. Pili wanaume wanakugopa, kwanza unatembea na mume wa mtu kitu amcho wanaume wengi hawapendi, ni bora uwe kicheche wakawaida ila mwanaume anayetaka kukuoa akijua ukinyumba wa mume wa mtu anakutumia anakimbia.

Ndiyo ilivyo ni kama kalaana flani au tuseme kitu flani kinakera kuwa hujitambui hivyo unawakimbiza wanuame kwani kila wakiuliza wanasikia una mume wa mtu. Tatu unajikuta huwekezi kiuchumi, unapokua na huyu mtu, una kamatumaini kakuolewa moja kwa moja unajikuta unaishi maisha kama mke wa mtu, kumuangalia yeye.

Kuweka mipango kumuangalia yeye anakusaidia vitu vidogovidogo unajiona una msaidizi, unakaa mnashauriana mambo ya maana kumbe unashindwa kufanya yako kwani mwisho wa siku atakaucha na kurudi kwa mkewe. Unajikuta huna kitu cha maana cha maendeleo kwakua tu umeshikilia X ambaye alishakuacha.

Nimalizie kwa kusema kuwa hembu jithamini, hembu hata kama yeye kaakudhauaru kukuona kama dekio lake anakutumia kufuta miguu yake baada ya kumaliza kukuvaa. Yaani kakuvaa kwa miaka mitatu kakuona huna maana anakutupa unakubali kuwa Dekio Lake, kuja kufuta stress za mkewe kwako. Kama kakuona hivyo hembu wewe jithamini na muambia mimi si Dekio naweza kuwa T-Shirt mpya kabis akwa mingine! Unajua nishamaliza, badilika, na soma Kitabu changu!
⁠⁠⁠⁠
 
Ni ujinga kufikiri mwanaume aloko ndani na mkewe anakupenda, ni kwamba anakupotezea muda wako tuu. Akishakuacha akaenda kwa mwingine ni dhahiri kuwa alikuona hufai kwa matumizi ya ndoa!!!
 
Ni ujinga kufikiri mwanaume aloko ndani na mkewe anakupenda, ni kwamba anakupotezea muda wako tuu. Akishakuacha akaenda kwa mwingine ni dhahiri kuwa alikuona hufai kwa matumizi ya ndoa!!!
Sakayo Wa tumosa
 
Mm madem zangu wa zamani hata sijui wapo wapi...maana nkianza kukumbushia wote ntazeeka sijamaliza
 
Mara nyingi inakua ngumu,, kama ulivyosema mazoea n'a vitu kama hivyo.unajaribu mara kadhaa n'a unashindwa. Lakini inafikia Wakati unahitaji Kweli kubadilika,, daima huwa nasema time is à good healer. Muda ukifika inabaki kuwa Story...
 
Haya mapenzi haya... Co kwamba hawaelewi,ila kukubaliana na hali na ku'move on ndo shida inapoanzia
 
Sio kweli kabisa kama ulivyosema kuna facts ambazo hupelekea sisi Me kufanya maamuzi ya ndoa bila kutegemea inaweza kuwa shinikizo fulani.Hali inaweza kupelekea kuendelea kuwa na mahusiano na mpenzi wa zamani japo ulisha owa.Sio kila Ex ni Expired zingine Example

great thinker
 
Haya mapenzi haya... Co kwamba hawaelewi,ila kukubaliana na hali na ku'move on ndo shida inapoanzia
hawajaamua hakuna jambo linaloshindikana kama endapo mtu atadhamiria moyoni yale anayotaraji kuyafanya

ile kukubali kwamba ts over unakua one step ahead kumove on
 
Dah aisee umenikumbusha , nilikuwa na msichana wangu fln binti wa Kilimanjaro, binti nikimpenda sana kwasababu alikuwa na sifa zote za mwanamke wa ndoto zangu. Alikuwa na physical appearance nzuri sana, mguu wa bia , shepu la maana na makalio yasiyopimika. Simply nilimpenda sana, one day nilisema kitu tukiwa faragha basi akachukulia poa ila baadaye alienda akawasimulia marafiki zake basi wakamtia ujinga akaniacha. Dah japo mi ni mwanaume Mwenye roho ngumu ila niliumia sana, nilitumia kila njia kumrudisha, nikaongea na marafiki zangu hadi Mdogo wangu wa kike aisee akapiga chini. Mwisho wa siku nikaaema acha nimove on. Huyu demu naye kama kawaida akawa na wanaume wengine lakini mwisho alikuja kugundua kwamba hakuna asiye na madhaifu, akataka turudiane ila kuniambia akaona ni shida. Kitu kama mwaka hv one day akanitext kunipa hi, namba nikawa nishafuta kitambo nikamuuliza nani akajitambulisha then tukasalimiana. Ukweli ni kwamba bado nilikuwa nampenda ila nilikuwa na demu mwingine so nikampotezea. Baadaye akanifungukia anatamani turudiane ,kwamba amejutia hasira zake. Niliumia sana ila nikamwambia nina mchumba, akasema mchumba unaweza tu kumuacha by the way huyu demu hakuwa mchumba wangu bali demu tu ile bado nawaza cha kufanya huyu demu wangu akapata ujauzito basi nikamwambia hatuwezi kuwa pamoja tena maana yule binti ni mjamzito. Alisikitika sana ila alikuwa tayari kuwa haraka japo roho ilikuwa inamuuma sana.
Basi one day kiutani utani nikamwambia nimekumisi , nakuhitaji , nakupenda imekwenda imeshuka. Akaniambia nakuja maana yule binti aliwenda kwao. Kiutani nikamwambia njoo maana sikuamini kama yuko serious .Aisee baada ya muda mtu huyo, yaani niliumia sana kuona yule niliyempenda akazingua kakubali kuwa hawara. Sure nilipiga bao moja nikashimdwa kuendelea ghafla akaanza kulia kwa kujuatia maamuzi yake. Kwasasa anaishi na mwanaume ila bado ananiambia eti ananiwaza sana na kwamba kuona wakati mawazo yake yanakuwa mbali sana, kwa kifupi tumekubaliana tuache kuwasiliana ili aweze kusahau.....ILA DAH NAUMIA YALE MAKALIO YAMEONDOKA ila namshukuru Mungu nilipata ujasiri wa kuacha makalio na shepu na kuchukua kimbaombao changu ambaye sasa kanizalia mama yangu, Mungu anaweza kukunyima unachokipenda akakupa wa kukufaa maishani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Interesting

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom