Naombeni mawazo juu ya hili

Barackachess

Senior Member
Sep 1, 2018
156
121
Ndugu zangu, Nawasalimu kwa jina la jamuhuri ya muungano wa Tanzania,

tokana na ukuwaji wa teknolojia ulivyo hivi sasa , Mimi pamoja na walimu kutoka katika shule mbalimbali bora Tanzania (Top 50 Schools) tumeshirikiana kwa pamoja na tumeanzisha mfumo muhimu/maalumu unao wawezesha wanafunzi wa kidato cha 1 mpaka cha 6 (Kwa secondary) Pamoja na Darasa la 4 mpaka la 7 kwa Primary (English Medium) kufanya mitihani online popote walipo.

Mfumo huu ni rafiki, Na Utamuwezesha Mwanafunzi kufanya mtihani online (NECTA FORMAT) akasahishiwa Kisha akapewa report yake (Baada ya kumaliza mitihani yote ) Mara baada ya mtihani kuisha atafanyiwa correction mtandaoni kwa njia ya LiveVideo pamoja na kurudishiwa softcopy ya answersheet yake iliyo sahishwa (IN DIGITAL WAY). Vifaa vya kuzingatia katika Huduma hii ni internet pamoja na simu janja (Smart Phone) au Computer.


Pia mwanafunzi ataweza kuingia E-class yani Darasa la mtandaoni na akafundishwa kwa njia ya Livevideo na akauliza maswali mtandaoni na kujibiwa na mwalimu live
Mfumo wa majibu ni kama ule utolewao na balaza la mitihani yani NECTA, Kwani mara baada ya mwanafunzi kumaliza kufanya mitihani yake na kusahishwa, Matokeo yake yatatoka na matokeo yake yatapangwa kulingana na marks zake na nafasi aliyoshika kimkoa, wilaya na kitaifa, Pamoja na Daraja lake yani Division.

Wanafunzi watakao fanyaa vizuri kitaifa na kufanikiwa kuingia Top 10 watapata zawadi ikiwemo kulipiwa Ada za shule (Mwaka 1), Computer, Pesa Taslimu, Simu janja (Smartphone), Safari za Mbugani (Serengeti) pamoja Safari za kimataifa kwenye nchi zenye vivutio

Naombeni Ndugu Zangu mpitie tovuti yangu hii www.taifaexam.net na kama kutakuwa na chochote cha kuongeza naomba msisite kunishauri hapa au kupitia naba yanguu hii ya simu 0718220206
 
Back
Top Bottom