Naombeni kufundishwa kuendesha Pikipiki

Naombeni kufundishwa kuendesha Pikipiki

mleta mada pikipiki unayo na ni yako mbona utaijuaa tu hakuna kinachishindikana mkuu....nenda uwanjani jifunze mwenyewe.....kikubwa jua kuiwasha na kuchochea moto kidogo na ujue break ilipo basi
jifunze kuoangilia gia pia...mfano anza na gia namba moja kuondokea ukizoea unaingia ktk gia zingine
 
Unaiwasha, alaf unabana cruch ( ipo kushoto) alaf unaweka gear, utavuta mafuta taratibu wakat unaachia cruch slowly itaanza kwenda yenyewe
😂😂😂😂😂😂
Mkuu siyo rahisi kwa mtu ambaye hajawahi kuendesha pikipiki au gari. Timing ya crachi ya mafuta siyo rahisi kihivyo, kama hujui lazima chombo kizime
 
Nimenunua Pikipiki lakini sijui jinsi ya kuendesha, naomba mtu anifundishe jinsi ya kuendesha nitamlipa, napatikana Dar.
Unaweza ukafundishika kwa mtandao wa simu nikuelekeze hatua za mwanzo kabisa za muhimu za kufuata?

Kifupi kama unajua kuendesha baiskeli, ni rahisi sana kuelewa.
Hatua ngumu kwa mwanafunzi ni kuondoka na kusimama.

Ukiweza hayo, mengine yatafuata.

Mi sihitaji hela yako, pia nipo mbali na Dar.
 
Back
Top Bottom