Royal Warrior
JF-Expert Member
- Nov 19, 2015
- 1,166
- 2,144
Kuna watu 4. tuwaite A, B, C na D. wamefukiwa chini ya ardhi kasoro vichwa vyao tu. wakafunikwa macho kisha wakavishwa kofia ( za rangi nyeupe na wengine rangi nyeusi). A na B wametenganishwa na ukuta (yaani A hamuoni B wala B hamuoni A). Sasa wameambiwa njia peke ya wao kupona ni mmoja wao (yaani yeyote kati yao) aseme rangi ya kofia yake aliovaa kama ni nyeupe au nyeusi. akiipatia basi wote wataachiwa huru. akiikosea basi wote watauliwa. wamepewa dakika 10 watafakari.
hawaruhusiwi kuongea. na wanajijua kama wapo wa 4. na wawili wamevalishwa kofia nyeusi na wawili wengine wamevishwa nyeupe ila hawajui ni rangi ipi waliovaa wao.
C anamuona B.
D anawaona wote C na B.
hawawezi kugeuka nyuma kuangalia wa nyuma kavaa rangi ipi.
Baada ya dakika 1
swali: nani kati yao atatoa jibu?
swali: kwa nini atakua 100% sahihi?