...mgao wa umeme uwe saa moja mara moja kwa wiki. Kusiwe na madawa hospitali hata haya yasiyotosha sasa yawe machache zaidi, waalimu na manesi wapigike zaidi na wakulima wapigike zaidi. Labda hapo ndipo wenye imani bado na magamba watatia akili
mkuu umesema ambacho hua nataka kusema kila siku ila nasita,...
kiukweli ni kauli ambayo mtu anaweza kudhani wewe sio mtanzania,ila binafsi naomba
tupate gharika kali kweli kweli,ndipo watanzania tutakua na upendo!
Hatuna upendo ule tulio ambiwa tupendane,leo hii mtanzania nyumba ile anaweza kua analala njaa
lakini jirani yake anampikia mbwa chakula maalum,jirani anaumwa lakini hasaidiwi na jirani yake,...
mtoto wa jirani anaweza hata kuingia kwenye moto lakini jirani mwingine akakimbia kwenda kuchungulia
dirishani kama ataungua ili aanze kupiga kelele,...
wengine wanalia maisha magumu,wengine wanawaita "wavivu nyie",....
natamani,natamani kweli kweli,
1.petrol,diesel,mafuta ya taa viwe 10,000/= @ lita
2.chakula kipande bei mara mia zaidi,
3.magonjwa yatokee
na mengine mengi,naimani kabisa kabisa kabisa,haya yakitokea yatatuunganisha watanzania
na tutapendana,tunahitaji kitu kimoja cha kutuunganisha wote,nacho ni DHIKI KUU,....
lakini,mapenzi ya Mungu na yatimizwe