Naomba wimbo "Tazama ramani"

Naomba wimbo "Tazama ramani"

Joined
Feb 26, 2017
Posts
49
Reaction score
67
Wakuu habari zenu,,, natumai mu wazima na mnaendelea na shughuli za kulijenga Taifa.

Naomba mwenye Audio ya huu wimbo anisaidie kuipata.

"Tazama ramani utaona nchi nzuri,
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaaaaaaaaa....
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa,
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha.

Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania. Majira yetu haya, yangekuwaje sasa,
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha.

Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa,
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha".

Ahsanteni...
 
Dah... yaan mkuu umekuwa na mawazo kama yangu.. hv soon tu nikitaka nianzishe thread kama hii ya kuomba huu wimbo... yaani naupenda sana.. nausikilizaga TBC taifa.. Ila ni adimu sana..
Wakuu tunaomba mtusaidie huu wimbo
 
Kuna Clip moja ya JKT nahisi ni KANEMBWA au MLALE JKT, OP KIKWETE wakati wanamaliza mafunzo kabla ya gwaride kuanza(ile intro') wanaupiga. Ingia YouTube utafute gwaride zote za JKT utaupata mkuu.
 
Kuna Clip moja ya JKT nahisi ni KANEMBWA au MLALE JKT, OP KIKWETE wakati wanamaliza mafunzo kabla ya gwaride kuanza(ile intro') wanaupiga. Ingia YouTube utafute gwaride zote za JKT utaupata mkuu.
heshima yako afande,tusaidie direct link ,pengine ww ukienda u tube unaweza ona jila la hlo gwaride la kutoa heshima kuliaaa na ukatupa linki kuliko sis kwenye kutafuta moja moja mpka tuipate.....
 
f7e21a67ca881b97e27423b0a32756e0.jpg
Wakuu habari zenu,,, natumai mu wazima na mnaendelea na shughuli za kulijenga Taifa.

Naomba mwenye Audio ya huu wimbo anisaidie kuipata.

"Tazama ramani utaona nchi nzuri,
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaaaaaaaaa....
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa,
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha.

Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania. Majira yetu haya, yangekuwaje sasa,
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha.

Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde name nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya, yangekuwaje sasa,
Utumwa wa nchi, Nyerere ameukomesha".

Ahsanteni...
Audio jaribu hiyo
 
Attachments

heshima yako afande,tusaidie direct link ,pengine ww ukienda u tube unaweza ona jila la hlo gwaride la kutoa heshima kuliaaa na ukatupa linki kuliko sis kwenye kutafuta moja moja mpka tuipate.....
Hahah mimi sio afande, we cheki YouTube lile gwaride la kuanzia dakika 45 kuendelea(zipo gwaride mbili tofauti, ya Part I & II zinajitegemea) achana na vile vya dakika 2-15 kiongozi. Andika KANEMBWA JKT
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom