Naomba Ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba Ushauri

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kasheshe, Mar 11, 2010.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mimi ni Mtanzania-Mzanzibar, ila nina asili ya Bara.

  Natamani sana nikakitumikie kijiji changu au kata yangu ya asili, kwa maana niwe mjumbe wa zile halmashauri za vijiji au Ward Committees ili nilete changamoto za maendeleo na pia kuzuia ufisadi maana ufisadi wa levo ile ndio balaa zaidi, unaua watu wengi wasio na hatia.

  Lakini nimeajiriwa huku Unguja, sasa nitawezaji kushiriki maendeleo ya kule kijijini wakati huo nikifanya kazi huku Unguja?

  Nia yangu sio kuwa Mbunge wala nini, na wala sio kuwa active politician nataka kufanya mabadiliko na kuondoa ile dhana kwamba sisi tulioenda shule kidogo twataka vyeo vya juu tu... yaani kuanzia ubunge etc.

  "I'm only interested to make/influence significant positive change in my society... before I die"

  Nijuavyo mimi tukienda wengi vijijini ndio tutaleta mageuzi ya kweli...

  Naombeni ushauri nifanye je? Kazi naipenda na Napenda pia kusaidia kijiji/kata yangu!

  Natamani kama wananchi wangekuwa kwenye levo ya information age lakini hawako huko bado... watahitaji kuniona kwa macho yao ...sio kwa simu, email au vyovyote vile.
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,153
  Trophy Points: 280
  ..kwani taratibu za kuchaguliwa na sheria za kutumikia nafasi hizo zikoje?

  ..je, huna njia nyingine za kuleta mabadiliko ktk kijiji na tarafa yako bila kutumikia ktk nyadhifa hizo?

  ..kama umekaa muda mrefu nje ya tarafa yako inabidi kwanza uanze kushiriki ktk shughuli za maendeleo la eneo lako kabla ya kuomba nafasi yoyote ile ya uongozi.
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hivi vikao ndivyo vinavyopanga miradi yote ya maendelea... ndivyo vina-set priorities etc.

  Kwa kweli sina njia nyingine... maana si unajua mishahara yetu ndugu... nilitaka kusaidia kwa mawazo na brain... njia ile ya fedha sina mkuu...

  Nina uhakika kwa level hiyo ya kijiji/kata nikiwa na nia watanipatia maana huwa narudigi nyumbani mara kwa mara na kuongea na wazee... lakini mimi sitaki kuwa wale wanasiasa wanaosema wameambiwa na wananchi wagombee yetu ukweli ni kwamba wameongea na watu wasiozidi 50, na wapiga kura ni zaidi ya laki moja.

  Naomba msaada.
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,815
  Likes Received: 5,153
  Trophy Points: 280
  Kasheshe,

  ..naogopa usije ukapachikwa jina la MJUMBE MTORO wa vikao vya kamati za maendeleo ya kata na tarafa. je una uhakika kwamba utaweza kuzingatia mahudhurio na ushiriki ktk vikao na shughuli za maendeleo huko kijijini?

  ..wazo lako ni zuri kwasababu inawezekana kabisa ushiriki wako ktk hivyo vikao unaweza kuwapa mwanga wajumbe wengine kuhusu njia za kisasa za kusukuma maendeleo ya eneo lenu
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hili lingewezekana tu kama vikao vingine vingeruhusiwa kuendeshwa ki-teknohama lakini wataona haka kajamaa kanaringa sana.
   
 6. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mkuu kama wewe una nia ya kubadili japo kidogo kwa nini usifanye hiyo contribution yako hapo hapo Zenji? Then baada ya kustaafu tuseme miaka 65 unaweza kwenda kijijini kwako na kuanza kuwasogeza walalahoi walipa kodi wa hili taifa.

  Kwa kuanzia unaweza kujitolea kuanzisha Library kijijini kwako na kuanza kuwasogeza kwa kuwapa computers kama mbili hivi na wakaanza kuzitumia pamoja na connection ya Internet hivi na kuifanya kwa fee kwa kuanzia then baadaye ikawa bure kwa wananchi.
   
 7. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wacha1,

  Yakheee ishakuwa mambo ya kutoa hela hayo tenaaa, mi sinaa mapesaaa ati, lakini nina maushauri.

  Ukinona kwenye mtandao hapa, basi ujue wa mwajiri!
   
 8. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Mkuu computer mbili hazizidi Millioni moja unawapanga wanakijiji wanakopa na kajengo kadogo. Kwa kuanzia wananchi watalipa gharama kidogo baadaye inakuwa free, sio lazima wewe uchange kwa sababu hata vijijini ni ushauri mzuri wakiuwapa fweza itapatikana watajipanga tu hilo ni wazo kuna njia nyingine unaweza kutumia sio lazima hilo la kupashana habari na kujua nini kinatokea katika ulimwengu huu.

  Unaweza hata kuanzisha mradi wa kufyatua matofali ya kuchoma na kuanza kujenga nyumba madhubuti kijijini kwako kwa kushirikiana na wakandarasi na kuwa na ramani pamoja na vitu kama hivyo. Tatizo kubwa la wananchi siyo fweza ni mbinu jinsi ya kufanya na kuwa na mtu ambaye atawaongoza ambaye wanamuamini anafahamu anachofanya.

  Miradi mingine ni ya kielimu nk
  BTW umeshafanya feasibility study ukagundua ni kitu gani ambacho unaweza kufanya kijijini kwako?
   
Loading...