Nimekuwa na Msichana kwa miaka mitatu tangu chuo hadi 2namaliza. Nikapata kazi Mkoani, nimefanya kazi kwa Miezi 5 nikiwa mbali na Mchumba wang lakin 2mekuwa 2kifanya Mawasiliano kwa kipind chote. Nilitokea kumwamini rafiki yangu (kazn) kupitiliza hadi nikampa Namba ya Shemeji yake. Sikujua kumbe jamaa anapeleka Maneno yakunigombanisha na Mchumba wang, kweli 2likolofishana. Ikabidi nimwombe Mama yangu Mzazi aniombee Msamaha. Yakaisha. Sasa kumbe wakati hoo 2megombana, akaamua Kulala na Mtu mwingine. Nilivyopata rikizo nikaenda Dar kwaajili yake ili 2weze kupanga Mipango ya Harusi. Kwani nilisha mtambulisha Nyumbani. Nilienda nikamkuta anaujauzito wa Wiki 3. Kweli iliniuma ikabidi nimwache na mie nikarud kazin. Bt aliitoa Mimba na Sasa ananiomba Msamaha 2rudiane. Kumpenda bado nampenda lakin nifikiria kilicho tokea Naumia sana. Jaman nifanyeje.?