Naomba ushauri

chen

Member
Feb 12, 2012
64
7
kuna mdada mmoja nimetokea kumpenda tena sana ila ana mimba ya miezi 5 co yangu nimemkuta nayo.kwao ni moro nami niko dar maisha yake ni magumu sana kwani anamtegemea mama yake kwa kila kitu na ina tokea muda mwingine anakosa mlo wa cku,tatizo anataka nimpatie hela atoe hiyo mimba ila uwezo wa kumpatia hela sina,sasa anataka atumie njia ya kienyeji kuitoa na kwa sasa nikimpigia cm hapokei.nifanye nn wana jf
 
kama kweli wampenda nakushauri msitoe hiyo mimba.
ukipenda boga penda na ua lake.
Msiue kiumbe kisicho na hatia kwa tamaa zenu.
OTIS
 
kama kweli wampenda nakushauri msitoe hiyo mimba.
ukipenda boga penda na ua lake.
Msiue kiumbe kisicho na hatia kwa tamaa zenu.
OTIS
Mwambie huyo mu uwaji mana wanadhani mimba sio kiumbe, kuna watu wanaogopa kumua sisimizi wao wanaua binadamu.
 
Mwambie huyo mu uwaji mana wanadhani mimba sio kiumbe, kuna watu wanaogopa kumua sisimizi wao wanaua binadamu.

Wajua kuna watu huwa wanakuja na mawazo ya ajabu sana.
Kuna raia wana roho za kikatili sana
OTIS
 
Wajua kuna watu huwa wanakuja na mawazo ya ajabu sana.
Kuna raia wana roho za kikatili sana
OTIS
Kweli kabisa sijui wamepewa roho gani hao, yani wao kutoa mimba wanadhani ni kitu cha kawaida tu, hawajui kama yule kiumbe ataenda wadai roho yao kule mbele ya safari...wamesahau kama safari sio kifo watafika tu, kule tunapo enda.

Ndo mana wengine ukiwauliza ulikwa wapi, na sasa uko wapi, na unaelekea wapi...wanasema tuilikuwa kigoma na sasa tuko dodoma na tunaelekea dar...Kumbe swali lao bado sana kulijibu.
 
unanafasi yakumfanya afurahie maisha...hata kama huna fedha jalibu kumpa ujasiri kuwa anaweza akalea mimba ktk mazingira hayo kwani mungu huwatendea miujiza wanao tubu au wanaojutia makosa yao!
 
Kabla hujamhukumu kwamba ana roho mbaya kwa wazo lake la kutoa hiyo mimba hebu vaa viatu vyake, msimuliaji anasema huyo binti ana maisha magumu sana, hujui hiyo mimba kama itaendelea kuwa tulivu au kutakuwa na complications na itahitajika fedha.

Naomba kufahamishwa kipi bora kutoa mimba au kuzaa na kumtupa mtoto, au kuzaa kumlea mtoto katika mazingira hatarishi na mwishowe mtoto awe mtoto wa mitaani.

KWA MTIZAMO WANGU KWA SASA NI HATARI ZAIDI KUITOA HIYO MIMBA KWA SABABU IMESHAKUWA KUBWA, ANAHITAJI USHAURI WA KARIBU NA USHIRIKIANO ILI ASIJE WAZA VINGINEVYO(KUZAA NA KUTUPA N.K)
 
kama anashindwa kuwa jasiri ktk hilo je mbele yakitokea tena atakuwa wa kunyofoa mimba mpaka lini.manake binadamu tunasahau haraka ataitoa na atajisahau tena yeye avumilie kama ameweza kufika miezi mitano minne anashindwa nini.
 
kuna mdada mmoja nimetokea kumpenda tena sana ila ana mimba ya miezi 5 co yangu nimemkuta nayo.kwao ni moro nami niko dar maisha yake ni magumu sana kwani anamtegemea mama yake kwa kila kitu na ina tokea muda mwingine anakosa mlo wa cku,tatizo anataka nimpatie hela atoe hiyo mimba ila uwezo wa kumpatia hela sina,sasa anataka atumie njia ya kienyeji kuitoa na kwa sasa nikimpigia cm hapokei.nifanye nn wana jf[/QUO we,kama unampend mshauli mimba hasitoe.maana nidhambi.pia mpeukweli k.m utampend na mtoto pia...
 
jikakamue umpe hela one off ya mtaji,hata kama ni biashara ndogo ndogo....kama kuuza genge:A S-heart-2: kama umempenda muoe mtoto atakuwa wako....mbona sie wanawake tunaletewa watoto daily na tunalea....:A S-cry:
 
Kutoa mimba ya miezi 5 sio utu unaua kiumbe bali pia ni hatari kwa maisha ya aliyebeba hiyo mimba. kama kweli unampenda utamjali na utatunza hicho kiumbe kitakachokuja duniani, huwezi jua labda unashushiwa baraka kutoka mbinguni.
 
kuna mdada mmoja nimetokea kumpenda tena sana ila ana mimba ya miezi 5 co yangu nimemkuta nayo.kwao ni moro nami niko dar maisha yake ni magumu sana kwani anamtegemea mama yake kwa kila kitu na ina tokea muda mwingine anakosa mlo wa cku,tatizo anataka nimpatie hela atoe hiyo mimba ila uwezo wa kumpatia hela sina,sasa anataka atumie njia ya kienyeji kuitoa na kwa sasa nikimpigia cm hapokei.nifanye nn wana jf
mimba miezi mitano mtoto ameshaanza kucheza tumboni, kama ameweza kuvumilia miezi hiyo mitano huyo dada anashindwa nini kuvumilia miezi minne iliyobaki.
kuna watu wanatafuta watoto wewe umejaliwa kupata bila kuhangaika unataka kutoa, unamtaka kumuua bila hata hatia.
mwambie wewe umempendea hiyo mimba yake na akitoa basi ndo mwisho wenu na mwambie kutoa mimba ni DHAMBI.
 
Kabla hujamhukumu kwamba ana roho mbaya kwa wazo lake la kutoa hiyo mimba hebu vaa viatu vyake, msimuliaji anasema huyo binti ana maisha magumu sana, hujui hiyo mimba kama itaendelea kuwa tulivu au kutakuwa na complications na itahitajika fedha.

Naomba kufahamishwa kipi bora kutoa mimba au kuzaa na kumtupa mtoto, au kuzaa kumlea mtoto katika mazingira hatarishi na mwishowe mtoto awe mtoto wa mitaani.

KWA MTIZAMO WANGU KWA SASA NI HATARI ZAIDI KUITOA HIYO MIMBA KWA SABABU IMESHAKUWA KUBWA, ANAHITAJI USHAURI WA KARIBU NA USHIRIKIANO ILI ASIJE WAZA VINGINEVYO(KUZAA NA KUTUPA N.K)
viatu vyake mbona vinavalika tu, kama maisha ni magumu basi wakijijini wangekuwa hawazai mana wale wanamaisha magumu zaidi ndo mana wanakimbilia mjini. ina maana wanaozaa ni wenye uwezo tu wa kulea, ukiwa unajua kuua ni vibaya basi ugumu wa maisha siyo kigezo cha kutoa mimba. ningemwelewa endapo angesema mimba imetungwa nje ya kizazi na doctor kasema no way out lazima itolewe hapo sawa otherwise simwelewi mtu anayetoa mimba kwa sababu nyinginezo na mtu kama huyo uwa namfananisha na jambazi anayevamia nyumba na lengo lake ni roho ya mtu tu(kuua).
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom