KBD... Inatakiwa uongee na huyo mama... kama huyo baba imeshindikana...
Yeye atacho amua ndio itakua msingi sababu waweza enda mbele na huyo mama akakukana.
mkuu...kaa mbali na maisha ya watu.
kama huyo mama anapigwa na hachukui hatua zozote basi ujue kuna jambo.
1. Wakati unatafakari njia ya kumsaidia huyo mama pia ufikirie namna ya kupata nyumba nyingine kwani huyo baba akikustukia unakula "notice."
2. Uwe mwangalifu huyo jamaa anaweza kukuzulia jambo ukashangaa.
3. Muelimishe huyo mama achukue hatua huyo bwana awekwe kikao ama na wazazi wa pande zote 2 kabla ya kulifikisha swala hilo kwenye vyombo vya sheria. Polisi unaweza kwenda mkamwekea mtego ila kwa polisi wetu sidhani kama utapata ushirikiano wa kutosha....
Unajua huyu dada aliolewa kijijini akaletwa kwa mume........sasa inawezekana hajui aanzie wapi na aishie wapi.
Jambo la kwanza, jaribu kuongea na muathrika namaanisha mkewake...haingii akilini kwenda polisi wakati mlengwa hujamshirikisha...na kwa sbb umesema inatokea anapolewa nadhani mngejaribu/wajaribu jinsi ya kumfanya aache pombe.....Lakini mkitaka kulichukulia the way unavyotaka liende kaka unageuziwa kesi sasa hv na nyumba utaiona chungu...
Wanajukwaa nawasalimu wote kwa heshima na taadhima. Mimi Ninaishi kwenye nyumba ya kupanga mahali fulani na baba na mama mwenye nyumba wanaishi hapo hapo. Sasa huyu baba mwenye nyumba anatabia ya kumpiga mke wake sana esp anapolewa. Hiyo tabia imekuwa ikiniudhi sana sana na nilishawahi kuongea nae kuhusu hiyo tabia akaahidi kujirekebisha. Alijirekebisha kwa muda lakini naona sasa imeanza upya.................. Yaani ni mkorofi sana, anambonda mkewe na matusi na maneno ya kashfa mengi mno mpaka aibu. Huyu mdada kipindi fulani aliondaka kwao, na huyu mume akaomba samahani kwa wazee na kuwaahidi kuwa kitendo hicho hakitajirudia lakini naona mambo ni yale yale................................................................................................................................................................................................................... Sasa nilikuwa nauliza mimi kama raia mwema, naweza kwenda polisi kumshtaki huyu baba au nikaenda japo kwa tamwa kupata uongozi wa kisheria...........................mimi niko kinyume na talaka lakini ningetamani kumfundisha huyu mwanaume kitu ili asirudie kitendo kama hiki tena. Naomba kuwasilisha.
Asante sana dia.........huyo dada kwa kweli anateseka sana. Ila nilifikiria labda wakati wa pulukushani mi ndio niwaite polisi.
Wanajukwaa nawasalimu wote kwa heshima na taadhima. Mimi Ninaishi kwenye nyumba ya kupanga mahali fulani na baba na mama mwenye nyumba wanaishi hapo hapo. Sasa huyu baba mwenye nyumba anatabia ya kumpiga mke wake sana esp anapolewa. Hiyo tabia imekuwa ikiniudhi sana sana na nilishawahi kuongea nae kuhusu hiyo tabia akaahidi kujirekebisha. Alijirekebisha kwa muda lakini naona sasa imeanza upya.................. Yaani ni mkorofi sana, anambonda mkewe na matusi na maneno ya kashfa mengi mno mpaka aibu. Huyu mdada kipindi fulani aliondaka kwao, na huyu mume akaomba samahani kwa wazee na kuwaahidi kuwa kitendo hicho hakitajirudia lakini naona mambo ni yale yale................................................................................................................................................................................................................... Sasa nilikuwa nauliza mimi kama raia mwema, naweza kwenda polisi kumshtaki huyu baba au nikaenda japo kwa tamwa kupata uongozi wa kisheria...........................mimi niko kinyume na talaka lakini ningetamani kumfundisha huyu mwanaume kitu ili asirudie kitendo kama hiki tena. Naomba kuwasilisha.
Hicho kituo cha polisi kipo mbali kiasi gani na unapoishi? Manake hizi nyumba zetu za Uswazi bana.....mpaka polisi wafike...kwanza sijui watafikaje. Nyumba ina address?