naomba ushauri wenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

naomba ushauri wenu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mtanzania in exile, Jul 13, 2012.

 1. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Katika mwaka mmoja tu (june 2011 hadi July 2012) wake za watu watatu wamenifata kunitaka kimapenzi. Ninachotaka kujua ni kwa nini? ni kosa gani nifanyalo kiasi kuwa wake za watu wafikiri nawataka?
  Wote nimewakwepa, lakini kinachonishangaza ni kwa nini hasa waache waume zao na kunifuata mimi? Wakati huo huo kuna mwanamke ambae yuko single na ananivutia mno lakini ananipiga chenga mwaka na nusu sasa na anasingizia eti ananihisi mimi ni player, jambo ambalo sio kweli kabisa!
  Mmoja kati ya hawa wake za watu amefika hadi kudai kuwa anajua hasa kuwa ninamzimia, na ni woga tu ndio unaonizuia mimi kumfuata, na kwa sababu hiyo ndiyo yeye kaamua ku make the first move. Wote wamedai kuwa ucheshi wangu na tabasamu zangu niwaonapo njiani na sehemu za mikusanyiko ni ishara ya kuwa niko interested. Hilo sio kweli kwani hiyo ni hulka yangu kuwa mcheshi kwa kila nimjuae sio kwao wao tu, tabasamu kwangu ni jambo la kawaida. Daima huwa na dakika chache za kusimama kusalimiana na kuzungumza na niwajuao nikutanapo pahali popote pale.
  Hivi ndugu zangu kuwa mcheshi na mchangamfu ni kosa? Huku ugenini ukianza kutokusalimia au kutotaka kujuana na watanzania wenzako ni hatari, kwani mbali ya wao kukuona kuwa unajipenda na kuwadharau wenzako pia nao watakutenga, jambo amablo sio jema hasa ukizingatia kuwa tuko mbali na familia zetu, binaadam mzima leo hujui kesho utaamkaje.
  Hebu niambieni nifanyaje ili kuepukana na matatizo haya. Imeanza wake wa watu kuhisi nawataka, isije ikaja kufika waume zao kufikiria nawaibia wake zao.
   
 2. Meljons

  Meljons JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 2,591
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Huyo ni roho inakuandama ya kutembea na wake za watu. Muombe Mungu akuepushe na hilo liroho akupe mchumba ambaye mtaoana.
   
 3. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama hufanyi makosa unawasi wasi gani.

  Huyo anaye kuitwa player ungeomba kamchezo naye basi :violin:
   
 4. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Moyo wa binaadamu ni dhaifu, nimekataa watatu and i hope nitakuwa na moyo huo huo kama akitokea mwengine, lakini ningelipenda isiwe hivyo na ndio nikataka kujua ni lipi nifanyalo ambalo limewafanya wake za watu kunitaka.

  Sasa wewe unasema nini hapo, nimekwambia aniitae player hanitaki kwa sababu anaamini kuwa mimi ni player na ndio maana hanitaki sasa kamchezo hapo nitapata vipi? vipi mshikaji ushaanza week end nini :A S 465:
   
 5. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #5
  Jul 13, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mimi nakupa njia za kumpata mana yeye anasema wewe ni player, sa mwambie twende tukacheze mana huwezi kunijua player kama hujacheza na mimi....Akijidai sijui sitaki mwambie nilidhani we ni experiance wa mchezo kuliko mimi ukanifundishe kumbe mimi na wewe wote si wachezaji....Afu utaona kama humpati.

  Weekend hapa watatoto wa ki Australians mapaja wazi tu mpaa unalia wasizidi kuzikamua.
   
 6. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pole kijana na hongera kwa kutupa clue ambazo labda zinaweza kutufanya kujaribu kukusaidia.
  - Kwanza huko ugenini uliko inaonyesha jamii yenu Watanzania) mnapenda kutanua. Sijui kitu gani kinakufanyeni hivyo, sijui uhuru wa kuwa mko mbali,au hamu ya kutaka kuchanganyika na wenzako, au labda ni njia ya kupata kipato cha ziada kwa kuhongwa au sababu nyengine zozote. Kwako wewe ni kuwa muangalifu na kujaribu mahusiano ya karibu na wale wachache utakaowaona wana muelekeo wako, yaani wa kutafuta maisha ya sasa na baadae.
  -Hulka yako ya kuchangamkia kila mtu inatafsiriwa vibaya na kuonekana kuwa wewe ni mmoja wa hao watanuaji (na ndio maana yule alie na msimamo kama wako pia anakutafsiri kuwa uko katika kundi). Jiangalie na jaribu kuchangamka na watu pale tu inapowajibika, nikikusudia kuepuka michanganyiko isiyo na maana.
  Tahadhari: Waswahili wana msemo; "Papo kwa papo kamba hukata jiwe" nikimaanisha kuwa mazowea yatakufanya uingie mtegoni na utaserebuka nao hao wake za watu.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Pole kwa kuwa mcheshi na mwenye tabasamu. Anza kuwanunia sasa!
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuna watu watafikiri unatania
  but mimi naamini ulichokisema
  huwa inatokea kwa baadhi ya watu kuwa na mvuto na kundi fulani la jamii
  mfano wapo ambao wanatongozwa na ma suger mammy tu sana
  wapo wengine gays ndo wanawataka hata kama wao hawashiriki
  wapo wanaopendwa na walimu wao tu
  kuanzia secondary mpaka chuo mtu anatembea na walimu wake tu
  mradi dunia hii haishi vituko...

  na hilo la waume zao kuku mind trust me...linakuja....
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  yaani mie haya mambo ya kila kitu imekuwa roho anakuandama jamani?

  Hivi ukae mkao wa kutongozwa napo usingizie roho?

   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  labda una mvuto wa kimahaba? Au wanataka kukuchuna? Encelea kuwakataa na kuwa serious zaidi....kama ulikuwa na ukaribu nao punguza.....kama ulijenga mazingira hatarishi acha....
   
 11. B

  Bosco massawe Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu hayo ni yakawaida cha msingi kua na msimamo mmoja. Kisha tafuta unaempenda nae akupende asiekupenda achana nae. Ukishaoa utulie na mke wako. Huo ndio ushauri wangu
   
 12. MWAMUNU

  MWAMUNU JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 661
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mi ushauri wangu jitahidi kucheza mbali na hao mamanzi wa watu !!
  na kama ni suala la uchangamfu basi changamka na wanaume wenzio.Usikute wanakutegea mtego ili wakushike ugoni then wakugonge ****, uku kwetu zipo sanaa hizo.Take care hakuna cha kuzimikiwa wala nini fatilia ushauri aliokupa
  THE BOSS utu uzima dawa !!!
   
 13. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #13
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  ahsante kwa ushauri wako ndugu, lakini napenda nikukosowe kidogo kuhusu hapo uliposema kuwa watu huku nje tunatanuwa sana. Hilo sio kweli na ni mawazo ya wengi wa waliopo nyumbani. Ukweli hutokea baadhi ya siku kukawepo na mikusanyiko ya hapa na pale na sio kila mwisho wa week end, mara nyingi hukuntana kwa sababu kuna jambo iwe harusi, msiba n.k hivyo ndivyo ilivyo pande hizi niliko, sijui kwengine though
   
 14. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  kwa maana hiyo unataka nimwambie kuwa nilidhani anapigisha kwa wengine, halafu unafikiri atapendezwa na kauli kama hiyo? No way, nipe ushauri mwengine
   
 15. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #15
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 797
  Trophy Points: 280
  The Boss wewe unashobokewa na kundi lipi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #16
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  hapo ndio unapopachikwa title ya mtu wa maringo. Nikimnununia kila mtu nitaongea na nani huku?
   
 17. N

  Neylu JF-Expert Member

  #17
  Jul 13, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 2,650
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kaka kuna ka msemo kanasema, Fanya kila kitu kwa kiasi... Hata kama kuwachangamkia hebu wachangamkie kidogo then endelea na mambo yako na uonyeshe wazi kwamba unachokimaanisha ni salamu tuu na si vinginevyo.. Siajabu wewe unawasabahi huku unatabasamu halafu unawatizama kwa mahaba vifuani .. Sasa hapo unategemea nin?
   
 18. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #18
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hujakosea nimeshaanza kuhisi machale ya mmoja wao.
   
 19. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #19
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  The only solution ni kuacha kuchekea chekea wake za watu maana kifuatacho waume zao nao wataanza kukuchekea wewe!:evil:
   
 20. mtanzania in exile

  mtanzania in exile JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 245
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  ucheshi ni tabia yangu, natabasamu kwa yeyote nikutane nae awe mwanamme au mwanamke. kwa nini nibadili tabia njema kwa kuwa tu baadhi ya watu hawaridhiki na walio nao?
   
Loading...