RedDevil
JF-Expert Member
- Apr 30, 2009
- 2,367
- 1,519
WanaJF, nimeona niwashirikishe kuhusu hili linalonisumbua muda kidogo kwani muda unaelekea ukingoni sasa. Mimi mwanaJF mwenzenu nimefanya application nyingi kwa ajili ya admission vyuo mbalimbali vya nje lakini application nyingi zinishis njiani ikiwa na maanisha huwa nashindwa kuzimalizia kutokana na gharama ama kushindwa kukamilisha malipo ya application fees. Nimejitahidi kufuatilia namna ya kulipa lakini kwa njia ya ama credit card au bank draft lakini shida ni kuwa nashindwa kutokana na kuongezeka kwa gharama. Kama kuna mtu au mwanaJF yeyote anaweza kunipa njia au kunishauri namna yeyote rahisi ya kufanya hayo malipo nitashukuru. Ahsanteni, naomba kuwasilisha hoja.