Naomba ushauri wenu wana JF

Too general DA, wa2 wa namna hiyo wapo na huko CTC anako chukua dawa huyo dada huduma ya ushauri wa namna ya kuishi wenza wenye HIV status walonazo ipo, hivo wai2mie, kizuri zaidi ni kuwa hata mwenzie kaacha kujinyanyapaa amini wakizingatia wataish maisha ya amani!.KUNA IMPROVEMENT KUBWA MNO KTK HIV MANAGEMENT TOFAUTI NA HAPO AWALI SEMA TU JAMII NDO HAIJAELIMIKA VYA KUTOSHA NDO MAANA INAKUWA NGUMU KU2MIA HIZO HUDUMA ZILIZO TAYARI. Kwakifupi waende wote ctc kuna msaada mkubwa tu.

Naona sijaeleweka mie nimesema swala la mwanaume kukubali kiulani bila kuhoji ndo issue iliyonichanganya.

Hizo ndoa za positive na negative mbona nyingi tu na tunawapa ushauri jinsi ya kuishi bila kuambukizana???

VCT au CTC???
 
Habari ya muda wana JF
Kama nilivyowaambia kabla kuwa huyu mume wangu ana kigeugeu sasa hivi kaja na mpya tena anasema hana tena imani na mimi kama naweza kumlinda hivyo ni bora tuachane. Ila alichonichanganya zaidi anasema nyumba inabidi iuzwe. hayao aaliyasema jana, leo asubuhi kabadilisha tena anasema hapana tusiachane tutengane tu. Mpaka naondoka sikupata kujua ni nini anataka kuachana au kutengana? Habari ndo hiyo ndugu zangu
 
Pole sana dada,just kno that God loves u, he listen talk to him, ur his child anointed empowered and eqqiped. Simply be incouraged.wengi wamekushauri vizuri ila mimi nakukumbusha tu kuwa nothing is impossible to God,unaweza kupona kabisa. Faith moves mt. I love u sister.
 
Pole sana barak, kwa fikra zangu mimi, nahisi kabisa mumeo pia ni muathirika pia ukute ndo alie kuambukiza.

Pili yawezakua analijua hilo tokea zamani sana ila hakuthubutu kukwambia. kwakua angekuvunja moyo .

Kitu kingine hakupenda kukwambia kwa kuogopa utawambia watu kua nyinyi ni waathrika.

Sidhani kama ni upendo tu, upendo wa agape huo ndugu yangu. cha kufanya usimuache endelea kuishi nae, muombe mkapime wote pia na mtoto

Ili muhakikishe, akiwa mbishi usilazimishe cha muhimu amekubali muendelee. kwa wewe pia niwakati wako wakua karibu na mungu kupita kawaida naku msihi mumeo pia kurudia mungu.

pole sana dada kwa wakat mgumu ulionao kwa sasa.
ila kuna vitu me vinanifanya niwe na waswas kidogo....

kwanza hii thread umejaribu kueleza juujuu sana mpaka unaona wachangiaji wanamponda sana mmeo.

pili kuna sehem nimeona umesema huo ugonjwa uliupata labda kutoka kwake au kabla ya ndoa sabab hujawah saliti ndoa. ebu fikiria mmeo ndo angekuwa wa kwanza kukupa hayo maelezo kwamba ni muathirika hivi ungelimuelewa kirahisi kama ulivyoandika, hapo najua ungetokea ugomvi wa ajabu sababu ww unauhakika haujasaliti ndoa sasa yeye kasaliti na sahv ni mgonjwa. apo najua ungedai taraka na kivumbi cha ajabu....check n think then use brain.
wengi wamekushauri vizuri sana, ila ninawaswasi kama utaendelea kuwa nae apo ndani na mambo yakawa safi kama mwanzo kabla hamjapima.
kuhusu jamaa kwa ninavyojua wanaume tulivyo atakuwa keshapima na kakuta anao naye kanyamaza sababu naye ana mchezo mchafu nje ya ndoa na anaamini yeye ndo kakupa so anajaribu kuona upo vip.
 
Dada, kwanza mm nakukaribisha sn ktk mtandao wetu wa sema usikike ktk jamii yetu, ila usivunje sheri, kwa mtu yeyote aliyeko humu kwenye mtandao au nje ya mtandao kwa kudhalilisha kwa namn yoyote ile, ili uwanja na carpet let au jamvi letu liweze kuwahabarish maelfu ya watu,
kuhusu jambo hili, dada nakupa pole kidogo tu, kwa hili lililotokea kwani hata mm limenikuta japo sijawahi kusema kuwa limenikuta llkn kwa ujasiri wako namm napenda kuwa wazi kwa hili, mm nilisafiri nje ya nchi nikiwa huku, nikasikia mke wangu anaumwa sn, tulikuwa tumeachana kama miezi mitano hivi alipopima akagundua kaathirika, lkn hakusema, niliporudi hakuwa wazi lkn alijikinga ili nisiambukizwe, lkn namshukuru sn Mungu nilipopimwa nikwa mzima, lkn mbele ya nesi mke wangu akawa analia, nikamwambia usihofu mke wangu, nitakuwa na ww kwa kila hali wala sifikirii kukuacha naposema mpaka ss niponae tunaishi maisha mazuri tu, watoto wetu wapo sekondari wengine wako primary school, napendakusema kuwa si lazima unisikilize mm au dada anaesema wanaume waongo sn atakubwaga sikumoja, c kweli sn mbona mm sijambwaga mke wangu tunakula tunda kivingine ci lazima liwe kama mwanzo,
jipe moyo mkuu sn, usiwaze wala kumfikiria sn mumeo kuwa ss anakula tunda kwa kumenya maganda wakati kwako ala kwa maganda, jitulize sn, ondoa gubu kabisa mbembeleze sn umlee zaidi ya mwanzo ili akupende zaidi ya mwanzo, usisikie la mtu maadam akubali kuwa atakuwa na ww kama mm nilipokubali mpende sn, leo toka alipoumwa mke wangu ni mwaka wanne, tupo woe na watoto wetu hawajui km mama aanumwa hiv.
Ubarikiwe sn.

Oooh brother mungu akubariki sana kwa moyo wako mkuu.
 
Habari ya muda wana JF
Kama nilivyowaambia kabla kuwa huyu mume wangu ana kigeugeu sasa hivi kaja na mpya tena anasema hana tena imani na mimi kama naweza kumlinda hivyo ni bora tuachane. Ila alichonichanganya zaidi anasema nyumba inabidi iuzwe. hayao aaliyasema jana, leo asubuhi kabadilisha tena anasema hapana tusiachane tutengane tu. Mpaka naondoka sikupata kujua ni nini anataka kuachana au kutengana? Habari ndo hiyo ndugu zangu
Pole sana, we tulia muache yeye achague anachopenda, kwasababu yeye ndo anasema hivi mara vile.
tulia endelea nakazi kama kawaida mpaka atakapojua anataka nini ndo mtaelewana sasa.
 
Huyo mumeo ni muongo sana tena wa kutupwa..........................iko siku utakuja kusema hapa.................wanaume walivyo wakali eti akubali hali uliyonayo ha ha ha ha ha wewe unacheza na kusikia kwenye redio akubali eti yeye mzima sio kweli nikwambie..........................

Dena Amsi kama umesoma mawazo yangu vile. Alikuwa anajua kwamba ameathirika ndiyo maana akawa anajibaraguza na kujidai. Kwa nini amekwenda kupima mwenyewe na hawakufuatana kwenye hilo? Samahani lakini inawezekana anajua sana hali yake ya kiafya alikuwa anakuzuga tu.

Hebu jaribu kufuatilia huyo mama wa mtoto wake bado yuko hai?

Pole sana lakini madamu amekubali mwenyewe wewe endelea nae tu.
 
loliondooooooooooooo!!!!!!!!! Nendeni tu wala msisikilize mameno ya watu ninao ushahidi wa2 wanne na mtoo wa miaka 6 walioenda na wako freshi sasa wanasubiri vipimo vya mara ya pili mwezi wa saba
 
My dear sister, mbona wapo ninawajua wanawake wameathirika na wanaume hawajaathirika or lets say virusi havijaonekana na wanaishi??? cases kama hizi zipo....wanaume hawafanani kwenye hili....labda tu tumshauri Baraka wakapime na mumewe ahakiki hali ya mumewe lakini najua kama anampenda atampenda tu hata kwenye hali hiyo!
Michelle mambo?
nahisi DA na wengineo wanaompinga mume huyu kwa vile namna ambavyo story imekaa ni vigumu kuamini reaction hii ya mumewe.
1. Kwanza alikuwa anakataa kupima afya yake kwa madai kuwa anaogopa na siku akijua ameathirika atakufa: Ujasiri wa kwenda kupima pasipo kupanick baada ya kuona cheti cha mkewe ameupata wapi? tena kenda pima kimya kimya kisha aja ASEMA (si kuonyesha cheti!!) kuwa hajaathirika???
2. Na kwa uwoga wa kuathirika (kama alivyoonyesha mwanzo) sidhani kama angewezakukubali kuendelea na mkewe unless wifey aseme kuwa makubaliano hayo hayahusishi kushiriki tena tendo la ndoa)
3. Lakini kikubwa nilichonote ni kuwa huyu bwana alizaa nje ya ndoa (huyo bintiye mwenye miaka 10 wakati first born ana miaka 12) ina maana wakati ndoa yake ina miaka 2/3 yeye tayari alishakuwa 'mzoefu wa nje'.....sasa miaka kumi ya mazoea na upungufu wa mapenzi unataka kunambia alitulia na kuwa saint?? Labda!! kama ni kweli nini kilikuwa kinamfanya awe anagoma kwenda kucheck afya??
4. Hii hadithi haijakamilika...........kuna missing/omitted parts nyingi tu
 
Habari ya muda wana JF
Kama nilivyowaambia kabla kuwa huyu mume wangu ana kigeugeu sasa hivi kaja na mpya tena anasema hana tena imani na mimi kama naweza kumlinda hivyo ni bora tuachane. Ila alichonichanganya zaidi anasema nyumba inabidi iuzwe. hayao aaliyasema jana, leo asubuhi kabadilisha tena anasema hapana tusiachane tutengane tu. Mpaka naondoka sikupata kujua ni nini anataka kuachana au kutengana? Habari ndo hiyo ndugu zangu

Baraka huyo ni mumeo kwa hioli unalolieleza hapa hebu jaribu kumshawishi mwende tena wote mkapime upya kisha baada ya kuhjakikisha nawe umeviona vipimo vyake naye kaona vyako au mmepewa majibu pamoja ndipo uje hapa tujadiliane hayo ya kuuza au kutouza nyumba...........mbona kama kachanganyikiwa sasa??
 
Nashukuru sana wote kwa ushauri wenu, ila mimi wasiwasi wangu ni kuwa je ni kweli anamaanisha anachokisema?
Maana kwa jinsi ninavyomuelewa anaweza kusema hivyo lakini bado hajawa na maamuzi kamili. Na wasiwasi wangu umenidhihirishia baada ya sasa kuanza vituko,
Mfano jumamosi nilimuuliza kama ataenda na watoto kumuona babu yao anaeumwa akasema hajajua, baada ya mimi kuondoka kwenda kazini alikwenda nao na akawaacha walale huko bila kunitaarifu, na hapo yule mtoto wa kwetu wote naumwa na kuna dawa anatumia na ameziacha nyumbani, baada ya mimi kurudi nyumbani na kugundua kuwa mtoto hatarudi na dawa ameziacha nikampigia kumuuliza sasa tunafanyaje maana dose itaharibika, akasema subiri nakuja tena kwa hasira, na aliporudi alikuwa kimya wala hakulizungumzia na likuwa amelewa, asubuhi pia akawa kimya, sasa ni visa tu na juzi amempeleka mtoto kwa aunt yake bila mimi kujua pia mpaka leo hajarudi, yaani kama mtu mwenye bifu fulani hivi na maelewano hakuna, na jana amelala kwenye chumba cha watoto.

Hio ndioo hali halisi ndugu zangu haya naendelea kusikiliza ushauri wenu.

Duh nina wasiwasi na anayoyaeleza kwa hao ndugu zake. Pole sana Baraka but jipe moyo MUNGU atakupigania.

Reaction ninayoiona hapa ni KUCHANGANYIKIWA...........na si kuwa amechanganyikiwa kwa kuwa wewe umeathirika la hasha wanaume wengi hawako hivyo hawako tayari maisha yao yafanywe magumu na mtu mwingine let alone mwanamke (Man's Ego). Yaani ingekuwa hivyo angekwisha kutangazia uchafu ili tu akuondoe kwenye maisha yake. Huyo amechanganyikiwa baada ya kugundua kuwa naye si salama (kama kweli alikwenda kupima na alikuwa hajaathirika tangu zamani) au baada ya kugundua matunda ya 'mambo' yake aliyokuwa akiyafanya gizani.... amechanganyikiwa kwa kile alichokisababisha kwenye familia yake.

Wewe tulia kimya ila vituko vikizidi mama ita wazee liwekeni jambo sawa kisha mkapime wote..........askufrustrate wanao bado wadogo ati
 
Habari wana jamii wote,ni mara yangu ya kwanza kuingia huku kwenye forum hii
Naomba sana mnipe ushauri wenu kwa haya nitakayoyaeleza hapa

Mimi nimeolewa nina miaka 13 katika ndoa, nina mtoto mmoja wa kiume mwenye miaka 12, mume wangu ana mtoto wa kike mwenye miaka 10 aliezaa na mwanamke mwingine.

tatizo langu ni kuwa miaka mitatu iliyopita niligundua kuwa nimeathirika na sasa natumia dawa za kupunguza makali(ARV)
Nilishindwa kumweleza mume wangu kuhusu hali yangu kwa kuwa kila nilipomshauri kuhusu kupima afya alikuwa hataki akidai kuwa siku akigundua kuwa ameathirika atakufa. Ila mimi nilipogundua kuwa nimeathirika nikawa sikubali kufanya mapenzi bila kutumia kinga, ingawa wakati mwingine alikuwa analazimisha lakini sikuwa tayari.

Hivi karibuni akanieleza kuwa amegundua kuhusu hali yangu baada ya kuona kadi yangu ya clinic, na yeye ameenda kupima na amesema yeye hajaathirika, hivyo kasema tuendelee kuishi bila watu kujua.

Mimi nikampa option kuwa kwa kuwa yeye ni mzima basi nisimbane kama atahitaji awe na mwenza mwingine basi tunaweza kuachana na yeye akaanza maisha mapya, lakini kasema kuwa haiwezekani tuachane kwa kuwa tumeishi muda mrefu na tumesaidiana mengi.

sasa naomba ushauri wenu je hili linawezekana? Au mna ushauri gani?

Ahasanteni

Nashukuru sana wote kwa ushauri wenu, ila mimi wasiwasi wangu ni kuwa je ni kweli anamaanisha anachokisema?
Maana kwa jinsi ninavyomuelewa anaweza kusema hivyo lakini bado hajawa na maamuzi kamili. Na wasiwasi wangu umenidhihirishia baada ya sasa kuanza vituko,
Mfano jumamosi nilimuuliza kama ataenda na watoto kumuona babu yao anaeumwa akasema hajajua, baada ya mimi kuondoka kwenda kazini alikwenda nao na akawaacha walale huko bila kunitaarifu, na hapo yule mtoto wa kwetu wote naumwa na kuna dawa anatumia na ameziacha nyumbani, baada ya mimi kurudi nyumbani na kugundua kuwa mtoto hatarudi na dawa ameziacha nikampigia kumuuliza sasa tunafanyaje maana dose itaharibika, akasema subiri nakuja tena kwa hasira, na aliporudi alikuwa kimya wala hakulizungumzia na likuwa amelewa, asubuhi pia akawa kimya, sasa ni visa tu na juzi amempeleka mtoto kwa aunt yake bila mimi kujua pia mpaka leo hajarudi, yaani kama mtu mwenye bifu fulani hivi na maelewano hakuna, na jana amelala kwenye chumba cha watoto.

Hio ndioo hali halisi ndugu zangu haya naendelea kusikiliza ushauri wenu.

Ahasante (Pihu)
Mimi kama sijapata kwake basi nitakuwa nilipata kabla ya kuolewa
Huo ndio ukweli wangu ndugu yangu.

Habari ya muda wana JF
Kama nilivyowaambia kabla kuwa huyu mume wangu ana kigeugeu sasa hivi kaja na mpya tena anasema hana tena imani na mimi kama naweza kumlinda hivyo ni bora tuachane. Ila alichonichanganya zaidi anasema nyumba inabidi iuzwe. hayao aaliyasema jana, leo asubuhi kabadilisha tena anasema hapana tusiachane tutengane tu. Mpaka naondoka sikupata kujua ni nini anataka kuachana au kutengana? Habari ndo hiyo ndugu zangu

Baraka_41 mpendwa.

Sikiliza kwa makini ushauri wa babu.

Nime quote posts zako zote ili kuunganisha mtiririko wa matukio ya kisanga hiki.

Nazungumza hapa kama mwanaume ambaye nazijua vema tabia zetu wanaume. Nazungumza pia kama mme wa bibi yenu ambaye ni mdau mkubwa katika masuala haya ya HIV/AIDS.. Huwa ananiambiaga visa vya kushangaza na kusikitisha sana.

Kama ulichokiandika hapa na kukiri kwa nafsi na mbele za Mungu kuwa ni ukweli mtupu basi:
1. Mume wako ameathirika na VVU ala anakuficha
2. Ndiye aliyekuambukiza VVU, ila anajaribu kukimbia kivuli chake
3. Anakutafutia sababu akufanyie kitu kibaya

Babu anakushauri, chukua tahadhari. Usikubali kuwa anakupenda kivile. Kwa mtu kama huyu, best option anayoiona babu ni kutengana naye. Kama anadiriki kukuficha ukweli na kukufanyia visa kama hivyo, iko siku atakushangaza kwa kubwa zaidi. ...Unarudi toka kazini unakuta nyumba ina watu wengine kabisaaaaa! Imeshauzwa.

Anywa, pole sana ndugu yangu. Ila maisha lazima yasonge mbele. Ishi kwa matumaini, zingatia masharti ya madaktari, mwombe Mungu akusaidie kuukabili huu mtihani....

Amini amini nakuambia, muda si mrefu dawa itapatikana.

Mungu akubariki sana.

Babu anarudi kitandani.
 
Aksante sana babu.
 
Babu nashukuru sana kwa ushauri wako , leo tena maekuja na uamuzi mwingine kuwa hatatoa talaka ila tutatengana na yeye takuwa na chumba chake na baadae ataondoka ila pale nyumbani ataacha chumba chake ambapo atakuja wakati wowowte atakapotaka.

Vile vile alisisistiza nikampime mtoto na namshukuru mwenyezi mungu nilikuwa naogopa sana kwenda kumpima mtoto lakini nimeenda kumpima na majibu ni Negative Nilishukuru sana kwa hilo.

Sasa jana anasema amemwambia mtoto kuwa yeye ataondoka pale nyumbani nasikia mtoto alilia sana.
 
inaonyesha anamshaur mbaya sana au jana wakat anaongea na wewe inaonyesha alikuwa anadubai kichwan na alipo amka asubuhi akakumbuka akawa bado anahang over hvyo alikuwa hajijui ila pia na wewe kuwa na msimamo utamuona mwenyewe anarud kwenye mstari usiyumbishwe na tena kama mmezaa na kama mnachangia maisha yan ninamaana wewe unaudumia familia pia acha jifanye hunapesa na hulet pesa uone atasemaje huyo mumeo ni limbuken na anaemshaur itakuwaje
 
Back
Top Bottom