Naomba ushauri wenu niolewe au? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba ushauri wenu niolewe au?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kanjunju, Jan 3, 2012.

 1. K

  Kanjunju Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina mchumba yapata miaka minne sasa,mwaka huu ndio tulipanga tufunge ndoa.lakini alipokwenda kwao kutoa taarifa kwao wamemkatalia.mama yake amemwambia kwamba kila anapomuomba mungu wake anaona giza mbele hivyo haitaji mwanae anioe mie.na akasema anatupatia miaka mitatu hiyo ndoa itakuwa imeshavunjika.kutokana na msimamo alioonesha mchumba wangu kwa wazazi wake nimeamua tufunge ndoa lakini nikifikiria upande wa wazazi wake napata hofu.nifanyaje wapendwa?karibuni kwa maoni.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Una tabia mbaya?
  Unaiba mboga jikoni?
  Dini ni tofauti?
  Kwa nini mama mkwe hakutaki?
  Kuna jambo hapo....

  Wewe unaona future ya ndoa yako?
  Umeridhika naye?
  Jiulize hayo, then uendelee
  Huolewi na mama mkwe anyway
   
 3. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Watu wengi bado tunahofu na vitu visivyo na ulazima. Kama mnapendana na kila mmoja anamfurahia mwenzake, kwa nini mtake kuishi kwa kufuata amri ya mtu mwingine? Its your life, the chance you have might be very difficult to get after. Kwa hiyo ushauri wangu, oaeni na mpendane zaidi.
   
 4. M

  Mamaa Kigogo Senior Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shoga huwezi jua na wewe umuombe mungu sana smtms wazazi wanaguvu sana mtashangaa mkioana mambo hayaendi jaribuni kuwashirikisha watumishi they will help you kwa mawazo na maamuzi
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Olewa ndugu, mama wakwe huwa hawaishiwi na visa, kwani unategemea kuishi na huyo mama mkwe?, kama nyie mwapendana yatosha.
   
 6. n

  ngwana ongwa doi Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  la! mama mkwe wako alipoomba anaona giza! je wewe ulipoomba uliona nini? giza au nuru?,je unaamini katika maombi?kama unaamini muombe Mungu akuthibitishie,kama kweli kuna giza mbele achana naye au kama kuna nuru uendelee naye,ni kweli Mungu hujibu maombi.

  Kama huamini katika maombi subiri wadau wataanza kukujuza sasa hivyi then utapima mwenyewe.
   
 7. P

  Pure nomaa JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 1,050
  Likes Received: 1,076
  Trophy Points: 280
  Kaa chini na mama mkwe na umuulize kinaga ubaga kwa nini hataki mwanae akuoe so baada yahapo i hope utakuwa nala kufanya.good lucky
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  nakushaur usiolewe, maisha ya ndoa ni ya hatari sana. Hilo giza analoona mama mkwe mtarajiwa iwe ishara kwako kuwa hilo ni jambo la kuliepuka
   
 9. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Siku hizi ndoa zinapigiwa "ramli"! shame!
   
 10. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tazama mimi navyo fikiria, mfano na kusudia mfano kwa upande wangu, kama napendana na mwanamke na mama yangu akasema nisimuoe huyo mwanamke....Inabidi niwachane naye, kwa sababu na mheshimu mama yangu.

  Narudi kwenye swali lako vipi na view upande wa huyo mchumba wako, kama mama yake hataki akuoe ni bora uwachane naye....Kama huyo mchumba wako ataamua kukuoa, ina mana si mwanaume mzuri kwako mana hana heshima kwa wazazi wake vipi atakuheshimu wewe.

  BTW, sikushauri uwachane naye ni bora kwanza apate green light kutoka kwa wazazi wake, kama wazazi wake hawataki...Wachumba wako wengi tu, usifanye haraka wako wachumba wazuri tu utawapata....Wewe bana kimyaaaaaaaa.
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Afadhali umeliona hili mkuu... tunajaribiwa sana hama mwaka huu
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kwa nini msiishi tu bila ndoa kwa muda?
  muone inakuwaje?
  wachaga wana kitu inaitwa 'kubariki ndoa'

  hutokea hata baada ya miaka kumi na tano kupita ndo wanaingia church...
   
 13. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kanjunju watu weengi saana husema mapenzi ni kati ya wawili wengine ni wakuwapotezea.... Siamini hio kauli wala sikubaliani nayo... Huyo mamake katia ngumu alafu muoane kwa kulazimisha hata kama mwapendana... Mie noana it is not advisable kwa kweli. Ilitakiwa wewe ufunge safari kwenda kwa mamake na umueleze kwa unaga ubaga kabisa kua wampenda mwanae na kua huna nia nae mbaya, na umuambie ukweli kua pamoja na kusema mwnae yupo tayari kwenda kinyume na wafunge ndo hivo hivo - wewe haupo tayari wala comfortable for watambua uwepo wake kama mama yake na kwamba waomba saana baraka toka kwake aweze kubali aoana na mwanae.

  Kwa upande mwingine huo uchumba ni wa mda mrefu mno. Haipendezi kama hamko tayari kuoana karibuni kuanza tambulisha ndugu wa karibu saana hasa wazazi... hakuna mwanadamu hana kasoro (hivo watakujua saana na sababu wanadamu hujisahau wataku judge kwa kasoro zako wakisahau hata nao wanazo); Hivo yawezekana kabisa kuna tabia labda mbaya ambazo unazo na zimejulikana... Ama tu yawezekana huna tabia mbaya lakini kwa mda ambao wamekufahamu huajaonesha ushirikiano kwa famiia ya huyo mchumba toka akutambulishe kwao.... Hivo mama mkwe kisha ona wee ni kimeo kwa mwanae...
   
 14. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  olewa olewa olewa
  eva/hawa was the luckiest woman; she had no mother-in-law."And all the people shall say, Amen."
   
 15. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Oh' Kid sis.... So having a mother in Law is Unlucky? Kumbuka ni mzaa chema.....
   
 16. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndio sababu akamfukuzisha Adam kwenye pepo...Angekuwa ana mother in law labda angemshauri asifanye haraka ya kumpotezea Adam pepo.

  Mungu atanisamehe mana kuna wakati mwingine inabidi tujibu vile hata kama dhambi.
   
 17. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mother Son Relationship

  [TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  A mother has undying love for her children. Her presence itself deeply affects the entire life of her little one. Our mother is the first woman in our life and cannot be replaced by anyone. A mother's love always makes her son stronger as well as balanced in his life. While a father makes his son strong enough to fight with the world, it is the mother who teaches him when and where to think from his heart.

  The most delicate aspect of mother and son relationship comes, when another woman enters into his life, either as a girlfriend or as a wife. This is the time, when almost every mother starts feeling insecure and becomes apprehensive. From being the only woman in her son's life, she has to share the affection with someone, who is as important in her son's life as she is. This is the time for the son to make his mother understand that she has and will always be the most special person in his life and that someone else can never take her place. On the other hand, a mother should also understand that she has to stop holding on to her son all the time and let go of him.
  hope umeelewa
   
 18. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mimi sijui kama ni unlucky au vp ila wewe ni mtu mzima na unajua case nyingi za mother in law unaweza chagua kuwaweka group gani.ila mimi wengi naona ni disaster kwa wake za watoto wao utadhani wao hawakuolewa kwa watu
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Yaani mie mtu akishaanza stori za 'kuonyeshwa' simsikilizi tena! Huyo Mungu wake anamuonesha giza tu la ndoa yenu, hakumuonesha mafuriko akaokoa maisha ya watu 30+? Tena nyie mngefunga ndoa wawili tu na rafiki zenu 2 kama mashahidi, akimaliza kuomba giza likiondoka awafanyie sherehe kubwa muunganishe na ubatizo kama sio other religious rituals!
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  wakwe wengine bwana, wanaanza vitimbi mapeeeeeeemaaaa, hajakupenda tu hamna kuona giza ,nyotanyota wala maruweruwe
   
Loading...