Naomba ushauri wenu ,age difference

Naomba ushauri wenu ,age difference

RAISI MPYA

Member
Joined
Jan 30, 2014
Posts
76
Reaction score
14
Habari zenu wana Jamvi

Leo nimekuja hapa kwa ajili ya kupata ushauri wenu,mi ni kijana wa miaka 22 lakini Mungu amenijalia nimepata ajira ya kudumu serikalini na yenye maslai mazuri,kwa sasa nimeanza kujitegemea na sina mpango wa kuoa 7bu nina mpango wa kuoa nikiwa na miaka 25 au zaidi.daima cjawa tayari kuwa kwenye mahusiano na mpaka sasa nipo single.

Linapokuja swala la kuoa naona kama naanza kutafuta Maisha upya jinsi swala hili ninavyo liona zito,wengi wananishauri ni vyema kuwa na mchumba mapema ili kujuana tabia lakini point ya age difference ndio imekuwa tatizo maana wengi wanasema age difference ifike miaka 5 na kuendelea.

Kwa mahesabu hayo kwa harakaharaka natakiwa nikatafute mtoto wa form 3 or 4.kitu ambacho sidhani kama kimekaa sawa,kwa kutambua kuwa humu ndani mpo watu wenye umri sawa na wazazi wangu najua mtanipa ushauri ambao either uta boresha ule tunaopatiana vijana mitaani au kubadirisha kabisa.

Nawasilisha.
 
Ninakushauri uongeze kiwango cha elimu yako kwa sasa kabla hujafikia maamuzi ya kuoa, baada ya kuoa utakuwa na majukumu ya ziada. Umri wa kuoa kwakweli hakuna formula, ninashauri uoe yule ambae roho yako imempenda kwa dhati kwani ni rahisi kuvumiliana kwenye ndoa.
 
Angalia zaidi vigezo vingine.issue ya age sio tatizo sana sana itakuletea matatizo ukitilia mkazo zaidi.unaweza kukutana na mwanamke kafanya 'mtemvulism'
.
 
Angalia zaidi vigezo vingine.issue ya age sio tatizo sana sana itakuletea matatizo ukitilia mkazo zaidi.unaweza kukutana na mwanamke kafanya 'mtemvulism'
.

nimekuelewa mkuu,sema kwenye kipengeke cha tabia naona pia kuna tatizo,unawezaje kutambua tabia ya m2 ucye ishi nae
 
Usikariri maisha....
usioe kwa sababu umesema uoe ukifika miaka 25..
utajipa pressure za kuoa sababu umri umefika hata kama hujapata mtu sahihi...

oa ukiwa tayari..na kuwa tayari ni pamoja na kumpata mtu sahihi....
 
vijiweni umeshauriwa nini? ili tujue pa kuanzia
 
dogo fikiri maisha kwanza mapenzi yatakuchanganya kwanza hata kaakili kako kenyewe hakajakomaa
umejenga..?.yaan unaacha kufikiria mambo ya maaanaa we....unakitanda kwanza..?
 
Miaka 25 kuoa ? Noma at least miaka 30 ukioa mapema utaki sa mengi Dunia hii . Una bahati umepata kazi ukiwa na umri mdogo fanya kazi na wekeza kisha chapa kitabu hadi igonge 30 na uanze wazo la kuoa ni ushauri tu
 
habari zenu wana jamvi,leo nimekuja hapa kwa minajili ya kupata ushauri wenu,mi ni kijana wa miaka 22 lakini mungu amenijalia nimepata ajira ya kudumu serikalini na yenye maslai mazuri,kwa sasa nimeanza kujitegemea na sina mpango wa kuoa 7bu nina mpango wa kuoa nikiwa na miaka 25 au zaidi.daima cjawa tayari kuwa kwenye mahusiano na mpaka sasa nipo cngo.
linapokuja swala la kuoa naona kama naanza kutafuta maisha upya jinsi swala hili ninavyo liona zito,wengi wananishauri n vyema kuwa na mchumba mapema ili kujuana tabia lakini point ya age difference ndo imekuwa tatizo maana wengi wanasema age difference ifike miaka 5 na kuendelea,kwa maesabu hayo kwa harakaharaka natakiwa nikatafute mtoto wa form 3 or 4.kitu ambacho czani kama kimekaa sawa,kwa kutambua kuwa humu ndani mpo watu wenye umri sawa na wazazi wangu najua mtanipa ushauri ambao either uta boresha ule tunaopatiana vijana mitaani au kubadirisha kabisa.
NAWASILISHA

Anza kutafuta vitu vya kuzalisha pesa na ujijenge kimaisha.nenda hivyo mpaka ufikie umri wa miaka 25,kisha hapo tafuta mchumba utakaesikia ndani yako kua anafaa,ukimpata kua nae ktk mahusiano mpaka miaka 28 au 30,kama atakua ametulia na anafaa utajua,hapo utaweza kufunga ndoa na kuendelea na maisha,TAHADHARI:katika kipindi hicho ukimpata huyo binti hakikisha na yeye ana umri wa kujua ni mume yupi anaemfaa kumuoa,maana hapo ukichukua binti mwenye uchu wa kuolewa kesho au ameshapiga mitaa mingi na wanaume alafu wewe ukamuweke miaka mitano ya kumjua na kusubili akili yako ikomae unaweza stuka kakuponyoka ghafla.kimsingi wewe bado ni mdogo sana.karibu kwenye maisha.
 
Kijana mleta mada hebu soma ushauri wa huyu ndugu kwa uzuri...

Ni ushauri mzuri...

Usikariri maisha....
usioe kwa sababu umesema uoe ukifika miaka 25..
utajipa pressure za kuoa sababu umri umefika hata kama hujapata mtu sahihi...

oa ukiwa tayari..na kuwa tayari ni pamoja na kumpata mtu sahihi....
 
dogo fikiri maisha kwanza mapenzi yatakuchanganya kwanza hata kaakili kako kenyewe hakajakomaa
umejenga..?.yaan unaacha kufikiria mambo ya maaanaa we....unakitanda kwanza..?

kitanda nnacho,
 
hicho si kiatu kusema cha mtoto mkubwa havai au cha
mkubwa mtoto havai. wee jali inapita basi .
 
Baada ya kuajiriwa ndiyo unaona swala la kuoa zito. Na vibinti vya fomu 3 na 4 hapo hutafuti mke bali unatafuta starehe. Kama unaoa wewe oa tu, kama unaona bado fanya starehe kwanza.
 
Ninakushauri uongeze kiwango cha elimu yako kwa sasa kabla hujafikia maamuzi ya kuoa, baada ya kuoa utakuwa na majukumu ya ziada. Umri wa kuoa kwakweli hakuna formula, ninashauri uoe yule ambae roho yako imempenda kwa dhati kwani ni rahisi kuvumiliana kwenye ndoa.

Inawezekana hapo ana Masters unataka aendelee kusoma mpaka wapi mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom