Naomba ushauri wakuuu..Najua huku kila kitu kina majibu

ketone

JF-Expert Member
Jan 22, 2016
510
655
Mimi niliwahi kuwa na leseni class C mwaka 2001 ila baada ya hapo niliamua kupiga kazi za udereva na ufundi magari chini nikaenda kusoma mambo mengine baada ya kumaliza chuo kikuu ninaona uhitaji wa kuwa na leseni ili siku hali ikiwa tete nirudi barabarani kutafuta ugali..
je nikitaka kupata lesseni ingine nifanyeje maana hii naona sitoeza irudisha tena maana sikuwahi kuilipia pale mda uliopoisha....
na je kuna sehemu wanasomea mafunzo ya leseni mda wa jioni kwa huku dar..es..salamu...
Na nikitaka kupata experience ya kuendesha mabasi makubwa nifanyeje..maana niliwahi kuendesha fuso...double coaster lakini basi sijawahi kuendesha..natamani sana kuendesha midude hiyooo...
pls naomba ushauri wako hapo..ila uwe unaelewa nilichouliza
 
Mkuu Kuhusu Leseni Yako Hiyo Huenda Ni Ile Ya Mfumo Wa Kitabu Ambao Kwasasa Hautumiki Tena Hapa Nchini.
Daraja C Uliyokuwa Nayo Ama Ukiitaka Kwasasa Lazima Uende Chuo Cha Usafirishaji/VETA Ikumbukwe Kwasasa Kuna Madaraja Mengi.

C Ni Kwaajili Ya Kuendesha Mabasi Ya Abiria Tu Unatakiwa Uende Chuo Kupata Hiyo Elimu Ndiyo Utaweza Kupata Daraja Hilo

Ikiwa Yoyote Utakavyoamua Nina Hakika Ukienda Chuo Ndiyo Njia Rahisi Ya Kupata Leseni Uitakayo Maana Coaster Utatakiwa Kuwa Na C1 Ambayo Shule Lazima

Kwa Dar VyuoVinavyotambuliwa Na Serikali Nadhani Wajuzi Watakuja Kukutajia Japo Ninavyojua Mimi Darasa La Jioni Sina Hakika Nalo
 
safi sana ndugu..ilikuwa ya vitabu kweliii...hata kumbukumbu zake naona hawana tena
 
Kwakuwa unajua Udereva tayari usipasue kichwa,
wahi VETA , jisajili kama Mwanafunzi wa awali.

-Ni kozi ya mwezi mmoja tu.
Unamaliza fasta unachukuwa Daraja 'D' lako baada ya mwaka unaomba Daraja lingine na kuendelea.

Kumbuka cheti Chao nacho kinaweza kukubeba mbele ya safari.

Kumbuka wao wanayo madarasa ya jioni.
La pili la msingi kwakuwa wewe unajua hutalazimika sana kuhunduria kila Darasa.

Short cut zama hizi Sio.
 
VETA Chang'ombe Ukienda Utaelekezwa Utaratibu Maana Wana Vituo Vyao Vingi Sana Tena Huenda Unapoishi Wakawa Na Huduma
 
Back
Top Bottom