Naomba ushauri wako rafiki....

Naomba ushauri wako rafiki....

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,614
True story iliyonitokea jana.
Soma na toa ushauri wako mwanaJF
Nikiwa nimejituliza kuvulini huku nikiongea na marafiki zangu; alinijia binti mrembo akavuka kiti na kukaa karibu yangu kama vile ananifahamu. Tulikatisha maongezi na kumtazama. Binti aliuliza hivi “Samahani nimeambiwa kwenye meza hii kuna mtu anaitwa Muggy” Rafiki yangu akamuuliza kama anamfahamu, binti akajibu kuwa simfahamu, rafiki yangu akamuuliza ulikuwa na shida gani naye? Binti akajibu kuwa ni kwa wema tu. Nikamweleza kuwa ndo mimi, binti akaniomba niongee nay eye pembeni. Nikamwambia kuwa aongelee hapo mezani kwani hawa ni marafiki zangu na chochote atakachonieleza nitawaeleza na wao.. haya ndo yalikuwa maneno ya binti huyo.
“Samahani kama nitakukwaza, naomba umkataze mke wako ahachane na mume wangu, amekuwa akitembea naye kwa muda mrefu, nimemfata na kumkanya akanijibu kuwa mume wangu alimfata mwenyewe hivyo wa kuthibiti ni mume wangu”
Nikamuuliza nataka mimi nimsaidieje; akasema ananiomba nitumie busara kubwa kusuruhisha hali hiyo.
Nikamuaga;
Angekuwa wewe ungechukua hatua gani?
 
Ngoja kwanza...yaani mkeo anamegwa na mume wa huyo binti? Kwa maneno mengine mkeo anachiti na mume wa huyo dada?

If that's the case I'd have puckered for a smooch.....
 
Ngoja kwanza...yaani mkeo anamegwa na mume wa huyo binti? Kwa maneno mengine mkeo anachiti na mume wa huyo dada?

If that's the case I'd have puckered for a smooch.....
Naamini umenipata vyema!
Maswali mengi yaligonga kichwani mwangu na sijapata majibu!

Je huyo binti alitaka na mimi nilianzishe kwake?
Je! kuna mtu anataka kuharibu ndoa yangu kwa uzushi huo?
Je! ni kweli mke wangu anatembea na huyo bwana?
 
mmmh yaani hata hukuhamaki kuwa mkeo anatarasuriwa na ndume la jamaa huyo.......................!:high5:
 
Usiwe na papara, usimchukie Mkeo, na wala usivuruge amani ya nyumba yako. Mwanaume ameumbwa akawekewa koromeo, Mungu alikuwa na maksudi yake kwamba hicho ni kizibo yaingiayo ndani yasitoke, so weka moyoni na anza uchunguzi wa kina kuhusu nyendo za mkeo. kama ni kweli utabaini na kama si kweli pia utabaini ukishapata majibu yaliyo sahihi halafu Tafakari chukua hatua.
N;B ANGALIA HATUA UTAKAYOCHUKUA HAITAHATHIRI FAMILIA NA WEWE MWENYEWE KWA UJUMLA.
 
  • Thanks
Reactions: Kop
Naamini umenipata vyema!
Maswali mengi yaligonga kichwani mwangu na sijapata majibu!

Je huyo binti alitaka na mimi nilianzishe kwake?
Je! kuna mtu anataka kuharibu ndoa yangu kwa uzushi huo?
Je! ni kweli mke wangu anatembea na huyo bwana?

Nadhani binti ametumia busara kubwa kuja kukueleza yaliyomsibu(yanayo wasibu ninyi), ila chakufanya sasa na wewe kuwa mdadisi ili uweze kujua mbivu na mbichi.
Kumbuka maamuzi ya haraka baadae yaweza kuwa na majuto.
 
"Nikiona mwenzangu anaibiwa nahisi kama naibiwa mimi, so miaka kadhaa ijayo ndo mniulize ntaoa lini..."
 
Anayechukuliwa mke/mume anajulikana kwa maongezi yake!
 
Pole, nakushauri hayo maneno usiyapuuuzie yafanyie kazi kama ni kweli utagundua tu,
 
Usiwe na papara, usimchukie Mkeo, na wala usivuruge amani ya nyumba yako. Mwanaume ameumbwa akawekewa koromeo, Mungu alikuwa na maksudi yake kwamba hicho ni kizibo yaingiayo ndani yasitoke, so weka moyoni na anza uchunguzi wa kina kuhusu nyendo za mkeo. kama ni kweli utabaini na kama si kweli pia utabaini ukishapata majibu yaliyo sahihi halafu Tafakari chukua hatua.
N;B ANGALIA HATUA UTAKAYOCHUKUA HAITAHATHIRI FAMILIA NA WEWE MWENYEWE KWA UJUMLA.

ni kweli kabisa Lisa kwasababu ni taarifa za kuletewa hatakiwi kuchukua maamuzi ya haraka, afanye uchunguzi kwanza ili aweze kubaini ukweli wa taarifa hiyo.
 
jenga ukaribu na huyo dada ili upate taarifa zaidi, usianze kuhisi eti na yeye anakutaka, pia huyo mkeo wewe unamuonaje? pia ulimpataje? kama hajatulia utajua tu haihitaji king'amuzi, nb.mke mwema anapatikana kwa Bwana.
 
Ya kuambiwa changanya na za kwako, kwangu mimi hapo naona kengere ya tahadhari inagonga kwa mbaaaaaaaaaaaaali
 
Mtafute tena huyo sister akupe details kuwa aligunduaje hilo na alikutana wapi na mkeo akampa onyo,atakayokueleza ndo utaanza nayo ktk upelelezi wako,bt usimwoneshee shaka yeyote wife huenda ni uzushi,moyo wa mwenzio ni kiza kinene.
 
Fanya urafiki na huyo dada mwambie unahitaji ushirikiano kuthibitisha je ni kweli unamegewa!?, then utaamua sasa utamfanyaje wife! Ametoa ofa tunda lako!!
 
Kuna mambo ya muhimu ulitakiwa kumuuliza huyo binti ( Mwanamke).
1. Mume wake ni nani (Jina) na anafanya kazi wapi.
2. Aligunduaje uhusiano huo.
3. Alijuaje kuwa wewe ni mme wa huyo mwanamke anaye mchukulia mume.
4. Je namba za simu za huyo mwanamke( anaye muibia mume) anazo, ili kuhakikisha na namba za mkeo.

Mwisho ulitakiwa ujue jina na namba ya simu ya huyo dada anayeibiwa mume. Baada ya hapo uchunguzi rahisi kabisa
 
"Nikiona mwenzangu anaibiwa nahisi kama naibiwa mimi, so miaka kadhaa ijayo ndo mniulize ntaoa lini..."

Hata ukitaka kuoa jiulize utamuoa nani, ukiambiwa we ni boyfrend haimaanishi upo peke yako,hahahahaha
 
Usimpuuze wala usimfatishe, ungemwambia asante kwa taarifa then fanyia kazi taratibu bila presha ukigundua muokoe mkeo humo shimoni umtoe maana anaweza fanyiwa kitu mbaya bure ukaja mkosa
 
Habari za saa hii. Kila hadithi au kisa kinapande mbili za maelezo huyo dada kasema yake lakini mkeo ujafahamu yake pia.
Kikubwa kama alivyokuambia huyo dada wewe usizidishe wala kupunguza muite wife kwa upole ambao hajawahi ona kwako kisha msimulie najua yeye atakuwa anamengi ya kusema kama uwongo au ukweli hilo anajua yeye ila tu wewe uwe jasiri usipayuke kisha umwachie yeye atatoa jibu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hata ukitaka kuoa jiulize utamuoa nani, ukiambiwa we ni boyfrend haimaanishi upo peke yako,hahahahaha

Heri nikate mgomba tu niufiche najua hautagombaniwa na wala sitaibiwa...!
Suprise umeamua kuniumiza moyo kabisa sio...!??
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom