Naomba ushauri wako rafiki....

Naomba ushauri wako rafiki....

Naamini umenipata vyema!
Maswali mengi yaligonga kichwani mwangu na sijapata majibu!

Je huyo binti alitaka na mimi nilianzishe kwake?
Je! kuna mtu anataka kuharibu ndoa yangu kwa uzushi huo?
Je! ni kweli mke wangu anatembea na huyo bwana?

hahahhahahhahah! watoto wa mujini bana kaaaz kweli kweli.
uspate hofu na mkeo wala hakucheat ila hiyo ni stail ya mjini kwamba BORA TUKOSE SOTE KWA NINI BANA??
tena kama unajitahd kutoka na mkeo, ukampiga pamba akanoga, home kwako amani full mkeo tabasamu kila uchwao basi jua VIJOKA VYA MDIMU HAVIKOSEKANI, yaani wao ingawa hawali ndimu lkn sharti na mchumaji asiile. hawa ni ndo MAFISADI KIWEMBE, kutwa kuchwa kufisadisha penzi la wenzao.

my take: ongea na mkeo mpe caution kwamba anawindwa and that kama anamarafiki ambao hawaaminiki awapotezee, istoshe mwambie asigombane na watu kama ni mtu mgomvi. abadilishe saluni anakotengeneza nywele na eneo analopenda kutoka kupata moja baridi.
 
jenga ukaribu na huyo dada ili upate taarifa zaidi, usianze kuhisi eti na yeye anakutaka, pia huyo mkeo wewe unamuonaje? pia ulimpataje? kama hajatulia utajua tu haihitaji king'amuzi, nb.mke mwema anapatikana kwa Bwana.
kwa taarifa yako mwanamke ambaye anacukuliwa mumewe na mwanamke mwingine hana courage hata ya kumsogelea mume wa huyo mwanamke kumwambia. yaani akimjua mwaamke watatukanana wao wenyewe but hawez kuake trouble kumtafuta huyo mwanaume kisha akaja eti smjui ila nataka kumwambia kitu.

funguka akili hii hapa mjini inaitwa staili ya FISADI PAPA'' msome mzee Yusufu utamuelewa.huu ni mchezo a unachezwa na watu kati ya hawa, ndugu wa mume(dada+mma mkwe ) kama hawampendi mkewe, mashoga wa bishomvu kia anawaringia na mumewe, majirani wao na mwanamke anayemtaka huyu mume ( yaani @tutoe b)
 
Hivi mtu humjui tu akukurupukie eti mkeo amuache mume wangu!!
'
Kama ni mimi naambiwa eti mke wangu anafanya ufedhuli huu wala siwazi
'
Ningemwambia tu huyo mwanamke nimesikia halafu aende!
'
Kwanza amejuaje niko pale?
'
Huyo aliyemuambia kwenye meza ile kuna fulani ni nani?
'
Amenijuaje?
'
Mambo mengine kuyapa nafasi ni kujisumbua tu!
 
dah! Unamoyo waujasiri sana Lisa Mungu akusaidie mumeo asije akatoka nje tena coz i know how it hurts.
Niliumia sana nipokuta ni kweli,nililia sana , maana sikuamini kabisa kama angeweza kufanya hilo. Ila nimemsamehe na nampenda Mumewangu ndiyo maana bado tupo .
 
ukitaka kufanikiwa kitu usiwe na papara, lazima uwe na subira, na umuombe sana Mungu akuondoshee maumivu ya Moyo , na akupe hekima ili uweze kulikabili jambo kama hilo. Mimi niliambiwa Mr wangu ana mwanamke na wamezaa, basi sikuwa na papara, nilimtafuta mpk nikampata, nikahakikisha nimemchukua mtoto, Mr anarudi home anamkuta yule mtoto yupo home anacheza nawenzie, kidogo azimie, alishindwa kuuliza wala kusema chochote akaishia kubwaga mizigo na kuondoka, mm sijui alienda wapi aliporudi akataka kuanza kunihadithia nikamkatiza kuwa sitaki maelezo. mpk leo namlea mm na kama atakwenda tena nitaomba talaka. maana ujinga wakati wa kwenda tu kurudi huulizi njia.

Duh! hii nayo kali, sasa mama yake alikubali vipi umchukue mtoto wake wakati yeye yupo? Ulitumia lugha ipi hadi mke mwenzako akakuamini?
 
huyo binti mjanja sana nadhani alikuwa anataka kukutongoza pembeni sasa ulivyojifanya kauzu eti aseme mbele ya rafiki zako kwani hata mkienda pembeni utawaambia ndio kaamua kukukomesha kwa huo uongo ili ujutie uamuzi wako. angekuwa mkweli angekupa vithibitisho vyote ili mtatue tatizo pamoja.

Darubini kali mkuu; hata wale niliokuwa nao mmojawao alinambia hivyohivyo! Ahsante sana kwa mawazo yako mazuri sana.
 
Hapo kaka kuwa mwangalifu si kila taarifa unayopewa ni kweli, nakushauri uchunguze kwanza kabla ya kuchukua hatua . Uchunguzi wako utabaini kama hiyo message ni ya kweli au la. Pia kwanini haukumuuliza huyo mdada maswali ambayo yangekusaidia kubaini mbivu na mbichi mapema. Kwanini yeye akuambie na kutoweka. Pengine nae huyo mdada ni adui wa ndoa yako , watu bwana wanapenda sana kuingilia ndoa za watu hasa yao yanapokua yamewashinda. Usiliache jambo hili hewani , chunguza na usibadilike tu hapo home kabla hujajua mbivu na mbichi.

Kwa kweli sikuwa na maswali zaidi ya kumuomba namba yake yasimu na ya mume mtuhumiwa! Ila kwa sasa sijisikii kufuatilia kwani nahisi kama ni mchezo wa kupangwa ili amani nyumbani kwangu itoweke!
Na nisipofuatilia nahisi alo-enginer huo mpango itam-pain zaidi.
 
Piga kimya, fanya uchunguzi kwanza, kama kweli anatemea na mume wa huyo dada.
Ukitoka hapo kapime,hiv, kabla haujafanya uamuzi mwingine
Ahsante sana kwa ushauri wako Somoe
 
Jamani mie sielewi watu, mtukatoka home kwake roho inamuuma anakuja kukupa habari na ulikubali mwenyewe iwe mbele y wenzako.

sasa unadhani yeye kuja kumtaja mumewe na mkeo itamtajirisha?

wengi huwa mnakosea mtu akikutonya hivi sio unaenda eti mnywesha mtu pombe aongee kumbuka mtu mwizi huwa mjanja na hata kama iweje mwizi na mjanja huwa hawakubali labda uwakamate papo hapo katika tendo.

mimi ningekuwa wewe pale pale ningemwita huyo dda/mama aliyechukua muda wake kunitafuta na kuja na kuongea nae kujua why anasema haya ameona nini maana utakuta namba ya mkeo inamsumbulia nyumba yake,

jamani nasema haya maana najua Tanzania wengi wanawake wanaiba nje na uwezi kuamini wana tabia hizo my friends wengine waume zao hata walale waote walie hawatakaa kamwe huhisi wanaiba.

Eti umesikia wanataka kukuvunjia ndoa ili iweje, kwani wanakufata kukutaka wakuvunjie uwe nao? maneno hayo I guess mkeo ndio anakuambia maana anajua utakuja kuanza kusikia maneno anajipanga vilivyo haswa kama sasa hivi unavyodhani anasingiziwa.

sasa ungeongea na dada huyo ungejua uanzie wapi, sasa mke kashajua na njia zao zitabadilika, kuweni wajanja jamani kukimbilia kuuliza kwa pombe eti hotelini ulidhani ndio jibu? mmh

mie ni ushauri tu kwa sie wanawake na wanaume. ulimuomba namba unajua mumewe anaishi nae vipi huko home si angeenda kumtwanga huko hadi basi,

ila nimeshaona wanawake wanaenda kwa wanaume wanasema mkeo analala au amelal ana mume wangu sasa na mimi nataka kulala na wewe ili nilipize, ndio maisha haya.

Good luck

Duh! sasa Dada Mzuri umekuja kivingine; kama nimeishawabumburua nifanyeje? Umeliangalia suala hili kwa mapana sana; ushauri hujanipa lakini. Nakushukuru na ninaaamini utanipa ushauri nifanyeje ili niweze kubaini ukweli uko wapi.

Na je nikigundua kwamba huyo mdada alichokiongea ni kweli; huoni kwamba ndoa yangu itasambaratika?
Watoto wangu wataishije kwa kulelewa na mzazi mmoja?
 
hahahhahahhahah! watoto wa mujini bana kaaaz kweli kweli.
uspate hofu na mkeo wala hakucheat ila hiyo ni stail ya mjini kwamba BORA TUKOSE SOTE KWA NINI BANA??
tena kama unajitahd kutoka na mkeo, ukampiga pamba akanoga, home kwako amani full mkeo tabasamu kila uchwao basi jua VIJOKA VYA MDIMU HAVIKOSEKANI, yaani wao ingawa hawali ndimu lkn sharti na mchumaji asiile. hawa ni ndo MAFISADI KIWEMBE, kutwa kuchwa kufisadisha penzi la wenzao.

my take: ongea na mkeo mpe caution kwamba anawindwa and that kama anamarafiki ambao hawaaminiki awapotezee, istoshe mwambie asigombane na watu kama ni mtu mgomvi. abadilishe saluni anakotengeneza nywele na eneo analopenda kutoka kupata moja baridi.

Nimekupata vyema tena sana! Ubarikiwe kwa busara zako.
 
Nimekupata vyema rafiki mwema. Ahsante.
 
Hivi mtu humjui tu akukurupukie eti mkeo amuache mume wangu!!
'
Kama ni mimi naambiwa eti mke wangu anafanya ufedhuli huu wala siwazi
'
Ningemwambia tu huyo mwanamke nimesikia halafu aende!
'
Kwanza amejuaje niko pale?
'
Huyo aliyemuambia kwenye meza ile kuna fulani ni nani?
'
Amenijuaje?
'
Mambo mengine kuyapa nafasi ni kujisumbua tu!
Ahsante sana kiongozi!
 
kwa taarifa yako mwanamke ambaye anacukuliwa mumewe na mwanamke mwingine hana courage hata ya kumsogelea mume wa huyo mwanamke kumwambia. yaani akimjua mwaamke watatukanana wao wenyewe but hawez kuake trouble kumtafuta huyo mwanaume kisha akaja eti smjui ila nataka kumwambia kitu.

funguka akili hii hapa mjini inaitwa staili ya FISADI PAPA'' msome mzee Yusufu utamuelewa.huu ni mchezo a unachezwa na watu kati ya hawa, ndugu wa mume(dada+mma mkwe ) kama hawampendi mkewe, mashoga wa bishomvu kia anawaringia na mumewe, majirani wao na mwanamke anayemtaka huyu mume ( yaani @tutoe b)

Ahsante sana!
 
Duh! hii nayo kali, sasa mama yake alikubali vipi umchukue mtoto wake wakati yeye yupo? Ulitumia lugha ipi hadi mke mwenzako akakuamini?
Mimi nilijidai mume wangu kanituma pale nikamtizame mtoto, kuwa ni damu yetu, akaniuliza jina nikamtajia la wifi yangu ambaye tulikuwa naye, basi yule dada akampigia mume wangu kumuuliza kama anamfahamu, akaambiwa ni kweli, basi akawa huru kuongea na sisi na tukamchimba akasema yooote kwa kujua sisi wote ni wifi zake. baada ya siku tukaenda sasa kumchukua ili akashinde home ndiyo ikawa moja kwa moja.wakamalizana huko wenyewe. anaruhusa ya kuja kumsalimia .Ila kwa sasa yule dada ananiheshimu sana.
 
Hakika we ni Kamanda; nimekukubali!
 
Fuatilia ndugu usione shida . Hii itakusaidia kuujua ukweli na pia utajua kwanini yote hayo yanafanyika then utawasaidia wengine watakaopatwa na mkasa kama wako. Usiogope , ukiujua ukweli utakuweka huru even in future hautatumia hili tukio kama reference endapo utamkuta mkeo na kosa la jinsi hii otherwise utageneralize tu na kusema ndio maana kipindi fulani ulisemwa hivi , wakati huenda tukio unalo refer halikua la kweli.
 
Ushauri wenu ni mzuri;
Baadhi ya majibu ya maswali hayo ni kama ifuatavyo:-
Binti nilimuomba namba ya mumewe akasema hana simu.
Nikamuomba namba ya kwake akadai hajaikalili kichwani; akaniomba niongozane naye hadi saloon ili anipe hiyo namba ya kwake - nikamkatalia.
Wife nilimuita hotelini - nikakaa naye - baada ya bia 2/3 hivi nikamuuliza - akadai hajui chochote kuhusiana na hilo.
Kuhusu utulivu wa wife wangu namwamini sana na ni mtu ambaye yuko bize na shughuli zake, ni mcha Mungu, hana makuu; n.k
Ila kulikuwa na tetesi mtaani kwamba kuna kundi la wanawake wanataka kuvuruga ndoa yangu. Kwa kukumbuka tetesi hizo ndo maana nilipoelezwa maneno hayo sikupanick wala kuwa na mawazo.
Hizi tetesi ulizisikia toka kwa nani? kwa mke wako au?
 
wengi huwa mnakosea mtu akikutonya hivi sio unaenda eti mnywesha mtu pombe aongee kumbuka mtu mwizi huwa mjanja na hata kama iweje mwizi na mjanja huwa hawakubali labda uwakamate papo hapo katika tendo.

Hata uwakamate hapo, bado hawatakubali.
 
Hizi tetesi ulizisikia toka kwa nani? kwa mke wako au?

Kuna mwanamke tunaheshimiana sana kwa sababu nilimsaidia mme wake kupata kazi nzuri. Majirani wakaanza kumwambia mme wa huyo mwanamke kwamba nina mahusiano naye ya kimwili. Uvumi huo uliposhindikana (kwa kuwa mume wa huyo mwanamke tulikuwa tunaheshimiana sana) ndo wakamwambia huyo mwanamke kuwa tunajifanya wajanja sasa wataamia upande wa pili (wakimaanisha kwangu). Sijui nimeeleweka au?
 
Back
Top Bottom