Jiamini mdogo wangu, usipoweza kujiamini hutoweza kufanya lolote.
Usisikilize ya watu wewe jikubali kwa vile ulivyo, hao wanaokughasi na maneno fanya yanaingilia sikio la kushoto kisha yanachomozea sikio la upande wa kulia.
Hata ungekuwa nazo hizo sifa wanazozitaka wao bado wasingekosa cha kusema kwa jinsi watu wanavopenda kusema. Mfano ukiwa mnene watasema, mwembamba watasema, mrefu watasema, mfupi watasema, usipopenda kula watasema, ukiwa unapenda kula watasema.
Hakuna utakachofanya hapa ulimwenguni ukakubalika na watu wote, kuna wataokukubali na kuna ambao hawatokukubali ambapo kwa mimi hapo nasema ni kawaida kwa sisi binadamu(tunayo kasoro hiyo).
Cha kufanya jiangalie wewe kama wewe achana na watu waseme, watasema itafikia muda watakuwa hawana cha zaidi watatulia