Nokla
JF-Expert Member
- Aug 12, 2012
- 3,169
- 1,711
Habari zenu wandugu,
Direct to the point. Mimi ni mgonjwa wa heartburn/ gerd kwa jina lingine ambayo imeshakuwa sugu. Kiukweli nasumbuliwa sana ni muda sasa wa miaka takriban 6 hivi nimejaribu tiba za aina tofauti hospitali na kienyeji lakini tatizo liko palepale.
Mwaka 2015 nilienda regency pale wakanipima kipimo kina OGD wakadai kwamba mishipa ya esophagus imelegea, na kunianzishia dozi ya miezi 3 ambapo baada ya kumaliza dozi tu nilikaa kama mwaka hivi hali ikaanza kurudi tena.
Nimejaribu kufuatilia ratiba za vyakula, vinywaji muda wa kula kulala etc lakini hali inazidi kuwa mbaya. Kwa sasa ni shida zaidi maana muda wote mimi mdogo wangu mchungu tu kama nimekunywa acid, meno yanasagika tu mdomoni bila kuuma, nina gesi nyingi sana tumboni muda wote mimi najamba tu iwe nimekula au sijala ni kujamba haiwezi pita dakika 10 nisijambe.
Kooni kuna kama ute mzito ambao mara nyingi lazima niteme hii hali imepelekea sauti yangu kuwa na mkwaruzo mzito. Yaani siwezi kuongea dakika 3 lazima nikwaruze koo ili liwe sawa au niteme ute mzito mdomoni.
Sasa naombeni mwenye kujua hospital nzuri inayofanya utafiti zaidi kwenye mfumo wa chakula na koo na esophagus ili nikafanyiwe vipimo nijue shida ni nini hasa? Kiukweli sihitaji mtu anipe dawa kwanza maana hospitali hizi ukienda wananipa anti acid kiukweli nimekunywa hadi yamekuwa kama maji sihitaji tena bali nahitaji kwanza nipate kujua tatizo ni nini na hali hii inatibikaje?
Natanguliza shukrani