Jumapili iliyopita nilijisikia kizunguzungu na kichwa kuwa kizito.Nikaenda hospitali wakanipima pressure wakaona 123/75.Wakapima damu na kuona sina maleria bali nina Typhoip.Nikapewa dawa za kunywa kwa siku kumi na bado naendela nazo na leo ni siku ya 4.Lakini bado najisikia kizunguzungu na joto kali mara moja moja na hali nilitegemea nipate ahueni.Sasa sijui kuna tatizo jingine au la.Na je kweli kizunguzungu ni dalili ya Typhoid?.Tafadhali naomba ushauri?
typhoid dalili zake huwa ni ngumu kuzitabiri,zinaweza kuja katika forms tofauti.maliza dose kwanza utapata ahueni,kunywa maji mengi,kula ushibe na upate muda wa kupumzika.
Ale bela.Nashukuru Mungu naendela vizuri sasa baada ya kunywa maji mengi kila wakati.Tatizo ni kuchimba dawa kila wakati.Ila ni bora kuliko kizunguzungu na tumbo kukaa ovyo.Kipindi wanachukua vipimo walipima uwingi wa damu wakasema iko sawa.Sijajua sukari kama iko sawa.