Naomba ushauri wa kibiashara nafilisika

bintishomvi

JF-Expert Member
Mar 21, 2015
1,164
831
Mimi ni mjasiliamali ninae shugulika na biashara za takarejea kwa mfano Machupa na Plastic chakavu nimejitahidi nimenunua mota na machine ya kuchakata na kutoa vipandevipande.

Nguvu yangu imeishia hapo nimezunguka kwenye kuomba mikopo wanadai mpaka waone eneo la biashara na mpaka ifike miezi 6 na dhamana ninayo zaidi ya machine sasa nimekwama nifanyeje ikiwa pakupata bidhaa napajua, masoko nayajua machine inaharibika muda unapotea biashara naijua vizuri maana nilianza Siku nyingi japo haikuwa aina hii nina mzigo nilinunuaga wa aina nyingine amboo nilikuwa nategemea kupata pesa nianzie biashara hii mzigo umekwama.

Nishaurini nifanyeje, nakufa njaa nyenzo ninazo.
 
eleza kwa kina yaani unanunua chupa unasaga kwa Mashine maalum then.....
eleza kwa kina au ni- inbox tuongee zaidi.
 
Ebu elezea kwa mapana jinsi unavyofanya hiyo kaxi baina yako wewe na wateja wako. Alafu ntakuambia cha kufanya mdau.
 
Nitanunua plastic chakavu kwenye vijiwe na kusaga kutoa vipande vipande na kuuza kwenye masoko ya hapa hapa au Kenya maana kote nilishafika kulinganisha bei kwa hiyo nilichokosa pesa ya godauni na malighafi lakini nina uzoefu wa biashara ya takarejea. Hata kwa dhamana nitaweka eneo langu ilimradi uaminifu tu maana napoteza muda wa biashara au mnanishauri nini?
 
Naitaji pesa ya kuendeleza biashara nipate eneo la biashara na mtajj wa kununua bidhaa yaani hesabu yake kama ml 7. Niko tayari kuweka rehani nyumba yangu ambayo haijaisha ipo maeneo ya Kimara mwisho hata kwa makubaliano yoyote ilimradi yawe ya khaki kwa pande zote mbili ninamaanisha tunaenda kwa mwanasheria Niko tayari kulipa riba.
 
fanya haya
1.Ondoa mawazo ya kushindwa kwenye fikra zako.
2.ili kupata mahali pa kufanyia kwanini usifanyie hapo hapo nyumbani kwako.
3.Anza kidogo kidogo usiharakie kwenda haraka utapata hasara.
4.Weka tabia ya kuweka akiba hii itakusaidia sana maana kanuni ya mikopo siku zote ni kuwa unakopa kuongezea mtaji tu yaani 75% ya fedha ni zako na 25% ni za mkopo
 
Nashukuru kwa ushauri wako .kunachangamoto ilinikuta ndani ya biashara na nje ya biashara , lakini niliitatua ndiomaana niliyumba kiuchumi na kibiashara .
 
Leo ukikopeshwa hiyo m7 utarudisha baada ya muda gani na riba sh ngapi?
Je, hiyo pesa itakidhi mzunguko wa hiyo biashara yako?
Vipi kuhusu joint venture ili ufanye biashara ukiwa stress free?
 
Nikikopeswa m7 nitarudisha mkopo pamoja na riba m 10 nitarudisha kila mwezi m 1.7 ilikupunguza deni na riba. Ili swala la kusheha sio mbaya tutawajibika kwa pamoja na kukubariana kisheria.
 
Vp kama mshirika mpya akiamua ku inject 5m kwenye hiyo biashara, je utaweza kuingia nae mkataba wa kuwa shareholder na mkaanza biashara au ni mpaka itimie hiyo 7m?
Kwa uzoefu wako na hii biashara sales turnover ya mwezi ni sh ngapi?
 
Tutahanzia tatizo maeneo ya kusagia wanatoza pesa nyingi na hiibiashara inachukua eneo kubwa kidogo na isiwe maeneo ya watu maana machine inatoa kelele sana .
 
Tutahanzia tatizo maeneo ya kusagia wanatoza pesa nyingi na hiibiashara inachukua eneo kubwa kidogo na isiwe maeneo ya watu maana machine inatoa kelele sana .
Kwa mwezi mauzo yako ni kiasi gani?
Umesahau kujibu swali hili mkuu.
 
Kwa mwezi mauzo yako ni kiasi gani?
Umesahau kujibu swali hili mkuu.
Wastani wa kila siku 2 kupata tani moja na kusaga zaidi ya hapo ni juhudi yako tu kujituma kutafuta mzigo na kuhalakisha kununua na kupeleka eneo la kusagia kwa haraka na mengine Mengi ukiwa eneo la tukio na ukionyesha nia ya kuitaji tufanye kazi imladi usiwe mnyanya wakuchezea uchafu .
 
Naitaji pesa ya kuendeleza biashara nipate eneo la biashara na mtajj wa kununua bidhaa yaani hesabu yake kama ml 7. Niko tayari kuweka rehani nyumba yangu ambayo haijaisha ipo maeneo ya Kimara mwisho hata kwa makubaliano yoyote ilimradi yawe ya khaki kwa pande zote mbili ninamaanisha tunaenda kwa mwanasheria Niko tayari kulipa riba.
Basi mkuu, ktk safar yako hiyo ya kukopeshwa hela ni ngekushuri huende benk Plc Kabisa maana wengine wakikopesha hela hutoweza kurudisha kamwe pesa zao ni za mazingara!
Kuwa makini. Hito hela isije ikawa Adhabu kwako.
Kitu kingine punguza Mhemko!!!
 
Back
Top Bottom