Biashara ya mashine ya kusaga na kukoboa nafaka- Fahamu bei zake, uendeshaji wa biashara hii pamoja na faida na hasara zake
ureni
JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,261
526
kusaga 3.jpg
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WANA JF
Wana JF wataalamu wa biashara na wale walioshawahi kuifanya biashara ya mashine ya kusaga naomba mnijuze inalipa?au itakua ni kupaka hewa rangi? Na mashine ya kusaga na kukoboa zinapatikana wapi na bei yake ni shilingi ngapi? Na umeme wake ni wa phase ngapi?
Nina kasehemu kangu Goba nimejenga fremu za biashara kwa mbele nataka niweke mashine ya kusaga nyuma, naomba mnijuze kwa mwenye experience au idea.
Natanguliza thanks.
Habari za jioni wakuu
Ninaombeni mawazo yenu. Niko kwenye mchakato wa kuanzisha kiwanda rasmi cha kusaga na kufungangasha unga wa nafaka mbalimbali. Nina mashine ya kusaga mahindi mkoani Dodoma na nilikua nafunga na kuuza unga kienyeji vijijini. Sasa nimeamua kuifanya iwe rasmi kabisa na Mungu akisaidia January 2016 bidhaa zangu zitakua sokoni. Niliyofanya mpaka sasa?
1. Mashine ya kukoboa na kusaga
Tayari ninayo na inatoa huduma
2. Mashine ya kupima, kufungasha na kufunga niliagiza kutoka China na iko kwenye hatua za mwisho za kuwa installed
3.Nimeshaanza mchakato wa kupata vifungashio kwenye kiwanda kimoja Bagamoyo. Mifuko ya kilo 5, 10 na 25 yenye nembo.
4.Stock ya mahindi ninayo karibia tani 10
5.Niko kwenye hatua za mwisho za kupata kibali cha tbs.
Kwa wazoefu wa biashara hii naomba kama kuna mwenye mchango wa ziada tushauriane mpaka hapo nilipofikia. Na kama kuna kitu kingine chochote kinahitajika.Tunaweza wasiliana hapa kwa michango au anymore business ideas/patnership na masoko zaidi.Au hata kwa PM
Shukran.
Mjasiriamali
Habari wapendwa,
Naombeni mnisaidie mwongozo nataka kuanzisha mradi wa mashine ya kusaga nakukoboa nafaka, gharama zake nizipi? uendeshaji wake?
Je, biashara hii inaweza kunitoa kimaisha? nimetenga chumba kimoja nyumbani kwangu ndo nitawekeza humo mradi huo, natanguliza shukrani wapendwa
kusaga 1.jpg
UFAFANUZI NA MICHANGO ILIYOTOLKEWA NA WADAU
Mimi sina experience illa nafikiria something similar huko mkoani. So far ninajua costs of the machines at University of Dar es Salaam Technology Development and Transfer Center (TDTC) ni as follows:
A) MAIZE MILLER
Model mm 500/18.5
Capacity (kg/hr) 500
Power Input 18.5 kW 3 phases
Dimension (mm) 1400*1000*900
Weight (kg) 290
Price: Tshs.2,100,000/=B). MORTAR HP 25 USED FROM UK.
Price: Tshs.1,500,000/=
TOTAL TSHS. 3,600,000/=
C). MAIZE HULLER/DE-HUSKING MAIZE
Model HL 500
Capacity (kg/hr) 500
Power Input 11 kW 3 phases
Price: Tshs.1,560,000/=
D). MORTAR HP 15-20 USED FROM UK.
Price: Tshs. 900,000/=
TOTAL TSHS.2,460,000/=
GRAND TOTAL FOR A, B, C, AND D: TSHS. 6,060,000/=
Kila ka kheri... I would also like to hear from others wenye experience na hili zoezi.
Nina uzoefu kidogo na ninazo mbili katika location tofauti vijijini na si mjini.
Nakuomba uchunguze sana upatikanaji wa mahindi katika sehemu unayotaka kuweka.Ikiwa upatikanaji sio reliable nakushauri uachane na mradi huo na uweke mashine ya kuranda mbao,construction industry inakuwa kwa kasi mijini.
Kuhusu upatikanaji,maduka yako mengi sana na mojawapo maarufu lipo Morogoro road karibu na jengo moja jipya (sikumbuki jina) ambapo wanauza vifaa vya umeme (tronic).Motor ya hp 20 ex China ni around 70000/- na kinu cha kusaga na kukoboa ni almost same price,500000/- kila kimoja ingawa kila baada ya miaka miwili itabidi ubadili,sio imara kabisa!!!
Naamini itakusaidia na achana na huyo mchangiaji ambaye anwaza naniiiiiiiiiiiiiiiiiii
Mashine zangu zinaleta at least shillings mia nane kwa unit moja ya umeme na umeme unaohitajika ni three phase.
Kwanza wewe unaye tafuta kuwekeza kwenye mashine ya kusaga, hiyo lugha ya kupaka rangi upepo itakukosesha watu wa kukusaidia. Labda niseme hivi mimi ninao uzoefu wa mashine ya kusaga.
Kusema ina faida ni kweli ina faida saana tu!!!!!!!! Maelekezo ya msaada:-
1. Jenga banda imara na store ya kuweka mahindi na pumba, safe storege kwa mazao ya mud mrefu.
2. Funga umeme wa three phase watu wa umeme watakuelewesha.
3. Nunua mashine yaani kinu cha kusaga size 75 kama uwezo ndogo anza na size 50.
4. Nunua motor size HP 25 au HP30 iwe china siemens Germany au Borch au England bora matunzo mazuri.
5. Nunua kinu cha kukoboa size 50 na motor HP 15. Tangaza biashara yako kwa majirani na watu wa mbali.
Pata kijana au vijana waaminifu wa kufanya kazi vinginevyo utafanyia upepo kama ulivyo tangulia kusema, uwajalibu kwanza.
Faida kubwa ya machine iko kwenye pumba.Jiandae ubarikiwe.
Nina uzoefu kiasi na biashara hiyo. Pia nimewahi kufanya kazi SIDO kwa muda mrefu kama Mhandisi na nimetengeneza sana mashine za kusaga na kukoboa. Basically ni biashara nzuri kama una capital ya kutosha kwa maana kwamba uwe na storage facility ya mahindi.
Usisubira mahindi toka kwa madalali. Uwe na wazo la packaging na sio usubiri watu wanye kusaga kwenye viroba. Nakushauri pia nunua mashine toka Workshop ya SIDO moshi au Arusha wana mashine imara sana.
UDSM mashine zao sio nzuri sana!!!!!. Nunua kinu cha kusaga namba 75 au 100 na cha kukoboa rola 3 na funga Mota za Horse power 25 au 30. Muhimu pia ni kuwa uaminifu wa wasagaji ni asset kubwa sana ingawa unaweza kuntrol wizi kwa kulinganisha unit zilizotumika na kiasi cha mifuko kilichozalishwa.
Kwa matumiza mazuri gunia moja kusaga na kukoboa usitumia umeme zaidi ya unit 7(kwh) kwa mota ya Hoers power 25.It is a good and lucrative business if you have capital and markeing strategy. Try now.
Pamoja na kutokuwa na uzoefu wa biashara aina hiyo, lakini nimeshuhudia uendeshwaji wa biashara hii nikiwa katika kampuni inafaa sana tu.
Jaribu kubadili kidogo mtazamo na matarajio ya biashara yakio na geukia upande wa pili kwa kujenga dhamira ya kujiamini zaidi ili ufanye makubwa.
Usifikirie watu wakuletee mahindi ili ukoboe na kusaga, ila hilo liwe second target.
• Kwanza fikiria kuwa na chanzo cha uhakika cha kupata mahindi na ikiwezekana kulima shamba lako mwenyewe na ya kununua iwe nyongeza tu.
• Pili fungua macho yako kwenye taasisi na vyuo na fanya utafiti utaona wanaweza kuwa soko lako ya uhakika ukiingia mkataba nao
• Tatu buni packaging ambayo itakuwa labeled na shirika la viwango ili kurudufu ubora wa bidhaa yako unaweza kuwa na soko hata kwenye supermarkets
• Nne wateja wengine wawe extra income baada ya kujiridhisha kuwa na uhakika wa kuendesha biashara yako hata kama unakuwa na upungufu wa wanaokuja kutumia vinu vyako.
Nikuhakikishie tena jiamini na jenga moyo wa kufanya makubwa, Kama Mungu yuko upande wako hakuna lisilowezekana, ila uwe tayari kuruka vihunzi kabla hujafikia mafanikio.
Penye nia pana njia
1. Mashine ya kusaga unga wako wewe ili uweke kwenye mifuko uuze au unasagia watu wanalipia huduma hiyo?!!
2. Angalia soko na wanunuzi endelevu au hapo unapoiweka tabia ya watu unaoishi nao je ni wa kipato cha kati au vipi, watu wengi kwa sasa wananunua unga dukani kuliko kubeba mahindi kwenda kusaga,angalia sehemu unayokaa na wateja unaowalenga.
3. Kukutoa au kutokukutoa inategemea na malengo yako, mtaji, mipango kazi, uelewa wako wa soko, timu yako utayofanya nayo kazi, aina za mashine utazotumia, usimamizi wako n.k. . . .Biashara inataka nidhamu ya hali ya juu sana nabkubadilika kutokana na soko na washindani wako.
4. Umeamua kuweka chumba katika nyumba hiyo hiyo au unapoishi umejenga vhumba pembeni maalum kwa kazi hiyo??!!. Kusaga ni kazi ya vumbi na ina kelele, sio salama sana kuweka katika nyumba hiyohiyo nadhani hata maandalizi ya msingi wa mashine ni tofauti na nyumba ya kuishi
Kila la kheri. . .
Naomba nikuelekeze gharama za uendeshaji, gharama si kubwa maana gharama zote zinaingia kwa mlaji mfano umeme,usafiri,mifuko,maji n.k
Unachotakiwa kuzingatia ni mahindi
Mahindi mazuri yatatoa wastan mzuri yakitoa wastani mzuri ndio yayakupa faida nzuri
Mahindi mazuri yanayotoa wastani mzuri ni ya Kibaigwa haya yanatoa wastani kuanzia 68 mpaka 75.
Maana yake asilimia 75 ni makande(unga) alisimia 25 ni pumba. Ukipata mahindi ambayo ni chini ya wastani wa 65 achana nayo vinginevyo ununue bei ya chini sana ili isikukate ukala hasara
Maana hapo utapanda pumba nyingi kuliko unga.
Pia kuna swala la bei inabidi ucheze nalo sana kama unavyoona kwenye maduka ya kubadilisha pesa na soko la mahindi liko hivyo hivyo.
Tena hapa ndio kuna kasheshe kwelikweli maana unaweza ukanunua mzigo wako Leo kwa bei ya sh 450 (mfano) kesho ukasikia bei ni 430 Mara nyingine huwa inapanda kwahiyo ikipanda faida kwako ikishuka itakupa stress maana ww utauza unga wako kwa bei ya juu kidogo kuliko wenzako ambao wamenunua kwa bei ya chini hivyo bei yao itakuwa chin kidogo.
Kwamaana hiyo tahadhar ni muhimu sana kwa nunua mahindi kwa bei ya chin kidogo ili hata yakipanda usiathirike.
Na hapa pia itategemea sana usukumaji wako was mzigo sokoni (hapa kuna mambo mengi ya kujua). Utatengeneza faida nzuri sana ukienda kununua mzigo mwenyewe mkoani badala ya kununua kwa madalali Manzese.
Niishie hapa kwanza
Mimi sina experience illa nafikiria something similar huko mkoani. So far ninajua costs of the machines at University of Dar es Salaam Technology Development and Transfer Center (TDTC) ni as follows:
A) MAIZE MILLER
Model mm 500/18.5
Capacity (kg/hr) 500
Power Input 18.5 kW 3 phases
Dimension (mm) 1400*1000*900
Weight (kg) 290
Price: Tshs.2,100,000/=B). MORTAR HP 25 USED FROM UK.
Price: Tshs.1,500,000/=
TOTAL TSHS. 3,600,000/=
C). MAIZE HULLER/DE-HUSKING MAIZE
Model HL 500
Capacity (kg/hr) 500
Power Input 11 kW 3 phases
Price: Tshs.1,560,000/=
D). MORTAR HP 15-20 USED FROM UK.
Price: Tshs. 900,000/=
TOTAL TSHS.2,460,000/=
GRAND TOTAL FOR A, B, C, AND D: TSHS. 6,060,000/=
Kila ka kheri... I would also like to hear from others wenye experience na hili zoezi.
Wana JF wataalamu wa biashara na wale walioshawahi kuifanya biashara ya mashine ya kusaga naomba mnijuze inalipa?au itakua ni kupaka hewa rangi?na mashine ya kusaga na kukoboa zinapatikana wapi na bei yake ni shilingi ngapi?
Na umeme wake ni wa phase ngapi? Nina kasehemu kangu Goba nimejenga fremu za biashara kwa mbele nataka niweke mashine ya kusaga nyuma,naomba mnijuze kwa mwenye experience au idea.Natanguliza thanks.
hapo knye rangi sijakupata ndio bness gani hiyo?
Nina uzoefu kidogo na ninazo mbili katika location tofauti vijijini na si mjini. Nakuomba uchunguze sana upatikanaji wa mahindi katika sehemu unayotaka kuweka.Ikiwa upatikanaji sio reliable nakushauri uachane na mradi huo na uweke mashine ya kuranda mbao, construction industry inakuwa kwa kasi mijini.
Kuhusu upatikanaji, maduka yako mengi sana na mojawapo maarufu lipo Morogoro road karibu na jengo moja jipya (sikumbuki jina) ambapo wanauza vifaa vya umeme (tronic).
Motor ya hp 20 ex China ni around 70000/- na kinu cha kusaga na kukoboa ni almost same price,500000/- kila kimoja ingawa kila baada ya miaka miwili itabidi ubadili, sio imara kabisa!!!
Naamini itakusaidia na achana na huyo mchangiaji ambaye anwaza nani. Mashine zangu zinaleta at least shillings mia nane kwa unit moja ya umeme na umeme unaohitajika ni three phase.
Kwanza wewe unaye tafuta kuwekeza kwenye mashine ya kusaga, hiyo lugha ya kupaka rangi upepo itakukosesha watu wa kukusaidia. Labda niseme hivi mimi ninao uzoefu wa mashine ya kusaga.
Kusema ina faida ni kweli ina faida saana tu! Maelekezo ya msaada:-
1. Jenga banda imara na store ya kuweka mahindi na pumba, safe storege kwa mazao ya mud mrefu.
2. Funga umeme wa three phase watu wa umeme watakuelewesha.
3. Nunua mashine yaani kinu cha kusaga size 75 kama uwezo ndogo anza na size 50.
4. Nunua motor size HP 25 au HP30 iwe china siemens Germany au Borch au England bora matunzo mazuri.
5. Nunua kinu cha kukoboa size 50 na motor HP 15. Tangaza biashara yako kwa majirani na watu wa mbali.
Pata kijana au vijana waaminifu wa kufanya kazi vinginevyo utafanyia upepo kama ulivyo tangulia kusema, uwajalibu kwanza.
Faida kubwa ya machine iko kwenye pumba.Jiandae ubarikiwe.
Wana JF wataalamu wa biashara na wale walioshawahi kuifanya biashara ya mashine ya kusaga naomba mnijuze inalipa?au itakua ni kupaka hewa rangi?na mashine ya kusaga na kukoboa zinapatikana wapi na bei yake ni shilingi ngapi?Na umeme wake ni wa phase ngapi?...
Huyu jamaa ureni yupo au alipitia tu, ana mambo yake?
Usijaribu kununua kinu cha udsm,nunua kwa mafundi wazoefu mtaani!pia jiandae kuchakachua umeme bila kufanya hivyo faida yote wataila tanesco
Nina uzoefu kidogo na ninazo mbili katika location tofauti vijijini na si mjini.
Nakuomba uchunguze sana upatikanaji wa mahindi katika sehemu unayotaka kuweka.Ikiwa upatikanaji sio reliable nakushauri uachane na mradi huo na uweke mashine ya kuranda mbao,construction industry inakuwa kwa kasi mijini...
mkuu umeelezea vizuri sana naona hii bness haihitaji mtaji mkubwa ukiwa na M4 unaweza kuanza natakanifungue yangu maeneo ya Manzese ya kusaga na kukoboa pale bness ipo!
Nina uzoefu kiasi na biashara hiyo. Pia nimewahi kufanya kazi SIDO kwa muda mrefu kama Mhandisi na nimetengeneza sana mashine za kusaga na kukoboa. Basically ni biashara nzuri kama una capital ya kutosha kwa maana kwamba uwe na storage facility ya mahindi.
Usisubira mahindi toka kwa madalali. Uwe na wazo la packaging na sio usubiri watu wanye kusaga kwenye viroba. Nakushauri pia nunua mashine toka Workshop ya SIDO moshi au Arusha wana mashine imara sana.
UDSM mashine zao sio nzuri sana!!!!!. Nunua kinu cha kusaga namba 75 au 100 na cha kukoboa rola 3 na funga Mota za Horse power 25 au 30. Muhimu pia ni kuwa uaminifu wa wasagaji ni asset kubwa sana ingawa unaweza kuntrol wizi kwa kulinganisha unit zilizotumika na kiasi cha mifuko kilichozalishwa.
Kwa matumiza mazuri gunia moja kusaga na kukoboa usitumia umeme zaidi ya unit 7(kwh) kwa mota ya Hoers power 25.It is a good and lucrative business if you have capital and markeing strategy. Try now.
Nina uzoefu kiasi na biashara hiyo. Pia nimewahi kufanya kazi SIDO kwa muda mrefu kama Mhandisi na nimetengeneza sana mashine za kusaga na kukoboa. Basically ni biashara nzuri kama una capital ya kutosha kwa maana kwamba uwe na storage facility ya mahindi. usisubira mahindi toka kwa madalali...
Mkuu maeleo mazuri ntapata mchanganuo wa makadirio ya bei! ubarikiwe sana nataka nitie maguu kyenye hii bness
Nina uzoefu kidogo na ninazo mbili katika location tofauti vijijini na si mjini.
Nakuomba uchunguze sana upatikanaji wa mahindi katika sehemu unayotaka kuweka.Ikiwa upatikanaji sio reliable nakushauri uachane na mradi huo na uweke mashine ya kuranda mbao,construction industry inakuwa kwa kasi mijini.
MIGNON nimepata mawazo hapa nafikiri itakua bora ni nunue hii mashine ya bei poa itakayodumu kwa two years nisikilizie biashara itakuaje kwanza, ndipo baada ya miaka miwili nikiona mwelekeo unalipa niupgrade,lakini mia 8 kwa unit ya umeme imenitisha tena manake inaonekana kama nitakua nafanyia kazi umeme tu,bila faida.
Asante sana kwa ushauri hapo nimekuelewa vizuri kwa maana nyingine kwenye hii biashara kupata hasara sio rahisi, mie kitu ambacho nawasiwasi nacho hapa sasa hivi ni umeme,labda garama za umeme zinaweza kuwa kubwa sana.
Nina uzoefu kiasi na biashara hiyo. Pia nimewahi kufanya kazi SIDO kwa muda mrefu kama Mhandisi na nimetengeneza sana mashine za kusaga na kukoboa. Basically ni biashara nzuri kama una capital ya kutosha kwa maana kwamba uwe na storage facility ya mahindi. usisubira mahindi toka kwa madalali. Uwe na wazo la packaging na sio usubiri watu wanye kusaga kwenye viroba. Nakushauri pia nunua mashine toka Workshop ya SIDO moshi au Arusha wana mashine imara sana. UDSM mashine zao sio nzuri sana!!!!!. Nunua kinu cha kusaga namba 75 au 100 na cha kukoboa rola 3 na funga Mota za Horse power 25 au 30. Muhimu pia ni kuwa uaminifu wa wasagaji ni asset kubwa sana ingawa unaweza kuntrol wizi kwa kulinganisha unit zilizotumika na kiasi cha mifuko kilichozalishwa. Kwa matumiza mazuri gunia moja kusaga na kukoboa usitumia umeme zaidi ya unit 7(kwh) kwa mota ya Hoers power 25.It is a good and lucrative business if you have capital and markeing strategy. Try now.
Kweli JF nimeikubali kuna wataalamu,hapo kwenye packaging nimeipenda sana,kwa idea hiyo naweza kupata sana manake naweza kusaga nikaweka kwenye package nikasambaza,mambo yakawa safi,asante sana mkuu,nikishaanza hii biashara nitarudi kuwapa feedback ya progress.Nashukuru sana,Je mambo ya leseni yanakuaje? Na ni kiasi gani?
Asante sana kwa ushauri hapo nimekuelewa vizuri kwa maana nyingine kwenye hii biashara kupata hasara sio rahisi,mie kitu ambacho nawasiwasi nacho hapa sasa hivi ni umeme,labda garama za umeme zinaweza kuwa kubwa sana.
TANESCO watakufungia mita mpya ambayo readings zake ni kule HQ yao, hivyo you will get the bills from HQ no kuchakachua, ni kama LUKU. Ongea na TANESCO!!!!!!!!!
Nina uzoefu kiasi na biashara hiyo. Pia nimewahi kufanya kazi SIDO kwa muda mrefu kama Mhandisi na nimetengeneza sana mashine za kusaga na kukoboa. Basically ni biashara nzuri kama una capital ya kutosha kwa maana kwamba uwe na storage facility ya mahindi...
Pamoja na kutokuwa na uzoefu wa biashara aina hiyo, lakini nimeshuhudia uendeshwaji wa biashara hii nikiwa katika kampuni inafaa sana tu.
Jaribu kubadili kidogo mtazamo na matarajio ya biashara yakio na geukia upande wa pili kwa kujenga dhamira ya kujiamini zaidi ili ufanye makubwa.
Usifikirie watu wakuletee mahindi ili ukoboe na kusaga, ila hilo liwe second target.
• Kwanza fikiria kuwa na chanzo cha uhakika cha kupata mahindi na ikiwezekana kulima shamba lako mwenyewe na ya kununua iwe nyongeza tu.
• Pili fungua macho yako kwenye taasisi na vyuo na fanya utafiti utaona wanaweza kuwa soko lako ya uhakika ukiingia mkataba nao
• Tatu buni packaging ambayo itakuwa labeled na shirika la viwango ili kurudufu ubora wa bidhaa yako unaweza kuwa na soko hata kwenye supermarkets
• Nne wateja wengine wawe extra income baada ya kujiridhisha kuwa na uhakika wa kuendesha biashara yako hata kama unakuwa na upungufu wa wanaokuja kutumia vinu vyako.
Nikuhakikishie tena jiamini na jenga moyo wa kufanya makubwa, Kama Mungu yuko upande wako hakuna lisilowezekana, ila uwe tayari kuruka vihunzi kabla hujafikia mafanikio.
Penye nia pana njia
Na kuchakachua ni nzuri lakini ubaya wake wakikustukia faini yake ni kubwa sana kuna mama mmoja boss wa Tanesco nilimgusiaga kuhusu kuchakachua akaniambia niachane nayo manake wakishtukua faini ni kubwa,inaweza fikia milioni tano.
Pamoja na kutokuwa na uzoefu wa biashara aina hiyo, lakini nimeshuhudia uendeshwaji wa biashara hii nikiwa katika kampuni inafaa sana tu.l
Jaribu kubadili kidogo mtazamo na matarajio ya biashara yakio na geukia upande wa pili kwa kujenga dhamira ya kujiamini zaidi ili ufanye makubwa.
Asante sana wana JF nazidi kupata mawazo mazuri sana la kampuni ni lamaana sana,kwa hiyo nitaweza kuwa na packaging zenye nembo ya kampuni yangu na kusambaza sehemu mbalimbali mjini,hapo nimekupata.
Suala la kutafuta masoko kwenye taasisi na mavyuo nalikubali na kushukuru kwa ushauri mzuri sana ntaufanyia kazi.Lakini kwenye kulima naogopa sana manake kuna mjomba wangu mmoja alikopaga fedha nyingi benk kwa ajili ya kilimo,
akachukua hecta kama 100 kwa ajili ya kilimo alikua anajiitaga mkulima bora,akalima mahindi shamba lote kwa kweli majirani wote walimkubali wakawa wanamwita investor,ikaja kitu moja inaitwa mvua ya alninyo mbona alikuwa mdogo kama piriton na pressure juu hakupata hata ya ushaidi,kwa hiyo toka enzi hizo ukiniambia suala la kulima linaniwia gumu.
Nafikiri fanya research ya kutosha kabla ya kujiingiza kwenye biashara hii ikiwa ni pmj kuangalia eneo ambalo unahitaji kuinvest,upatikanaji wa raw material(mahindi), wateja,idadi ya washidani kama wapo, bei yao,uwezo wa wateja(economic base) sifa ya mjasiriamal ni kutake risk ,usiogope hasara la sivyo utakufa presha bure once unapopata hasara.mkuu ubarikiwe sönga mbele.
Back
Top Bottom