Naomba ushauri wa biashara

lil pablo

Senior Member
Jan 6, 2018
108
51
Hadi sasa nimepata 4.6M
Je ni mkoa gani kwa sasa naeza fanya biashara sioo kilimo
Hioo pesa inatosha kuinvest kwenye biashara gani?
 
1. Biashara ya ununuzi mazao.

2. Mradi wa kufyatua matofali, paving blocks hasa kwenye miji kama Dodoma.

3. Simple Car wash: hapa mchawi ni location

4. Biashara ya mgahawa, hasa kwa mkoani
Hakikisha unakuwa classic, unapika chakula kitamu wahudumu wa safi kwenye kauli na mvuto utapiga pesa maana sehemu nyingi za mikoani migahawa ni sufiri watu wanaanzisha kwa mazoea hawapo serious.

5. Kata leseni ya biashara mifugo ya mifugo ni kama laki sita, nenda Dodoma kwenye minada ya kigwe na singida ukachukue mbuzi kwa bei ya (40K_60K) unaweza ukawa unawauza kwenye minada ya ruvu, loliondo kibaha ama mahakama ya mbuzi kiembe mbuzi vingweta. Au waweza kuwa unafanya delivery mwenyewe kwenye ma bar ya dar.

6. Shinyanga nilivoenda nilimkuta mama mmoja anatengeza ice cream. Ana vijana kama ishirini 10 kawapa vile vibaiskeli vya bakharesa 10 wengine baiskeli za kawaida na bei za askirimu zake ni 200 na 300 nawe waeza enda wilaya ama mkoa ambao bado ukaanzisha hii biashara, mashine yake ni 1.2m

pamoja na mashauri haya; za kuambiwa changanya na zako. Mwisho usiwe muoga Ku jaribu kitu chochote. Mfanyabiashara siku zote ni risk taker.

Nyingine watakuongezea wadau.
 
Umemshauri vizuri sana na sisi wengine tumetambua jambo hap. lkn ktk mazao nafikili kwa hela aliyonayo itamsumbua, angalau ingekua 8m.
 
Back
Top Bottom