Kwa tsh 50,000 naweza fanya biashara gani Zanzibar?

Nipo Zanzibar maisha huku sio kama bara Dar na mikoani,kwahiyo pesa inabidi ukubali kujitoa hasa.
Nenda soko la darajani kanunue mifuko Ile ya miatano uuze ,rejareja Kwa wateja hapo TOBO LA PILI.Pia unaweza kuuza machungwa kwenye toroli(vijana wa Tanga wanafanya sana hii hapa znz)
Pia unaweza kuuza pweza,ngisi,kachori na utumbo wa kukaanga wa ng'ombe sokoni Jumbi asubuhi.
Biashara ya kutembeza kahawa zanzibar sijaona sana ila ukiweza unaweza kufanya nahofia vifaa na mtaji wako mdogo.
Ahsante
 
Fanya biashara ya chakula wauzie watalii wa ndani
Huduma ya chakula zenji ni adimu
 
biashara ya uji wa mchele weka nazi na hiliki
kuwa msafi kikombe ni buku hukosi faida ya 20k kwa siku maana chupa moja faida ni 5k

Mchele agiza huku bara
 
Nipo Zanzibar maisha huku sio kama bara Dar na mikoani,kwahiyo pesa inabidi ukubali kujitoa hasa.
Nenda soko la darajani kanunue mifuko Ile ya miatano uuze ,rejareja Kwa wateja hapo TOBO LA PILI.Pia unaweza kuuza machungwa kwenye toroli(vijana wa Tanga wanafanya sana hii hapa znz)
Pia unaweza kuuza pweza,ngisi,kachori na utumbo wa kukaanga wa ng'ombe sokoni Jumbi asubuhi.
Biashara ya kutembeza kahawa zanzibar sijaona sana ila ukiweza unaweza kufanya nahofia vifaa na mtaji wako mdogo.
Ahsante
nakubaliana na wewe, nilikuja nikataka nikae huko wiki mbili ila nikakaa siku sita tu nikageuza, maisha yapo juu sana
 
Zanzibar maisha ni ghali sana hasa Bidhaa za vyakula ukitoa sukari kidogo.lakini vingine vyote vilivyobaki ni ghali sana,huku electronics na vyombo vya moto kama magari na pikipiki bei Chee.
 
Back
Top Bottom