Naomba ushauri tafadhali....

Huyu utakuta anasababu zingine za kuolewa na huyo bwana na si mapenzi. Mapenzi yana wivu ati. Mapenzi sio unyonge vile. Aombaye msamaha hubadilika. Huyo mwanaume anajua amekukamata huchomoki.
Jithamini uthaminiwe. Inawezekana akakuacha leo na kesho ukapata mwingine. Sidhani umeishiwa market kihivyo kiasi kwamba akuhenyeshe kiasi hicho, na wewe ukubali.
 
Sasa madhila yote hayo halafu soon unaolewa naye!
Kwa nini mabint mkiahidiwa ndoa uwezo wenu wa kufikiri unayeyuka?
Mko mbali ugomvi kila uchao,mkiishi pamoja hata Hiyo nyumba utaitamani kweli?

Ennie mpnz ndomana nahitaji ushauri mamii

Thnx
 
we binti tafuta wimbo wa SIKILIZA- NGWEA feat.Jay Dee,FA

utakusaidia
 
............... girls get married thinking once married their man/ husband will change but the truth is they dont.

za kuambiwa changanya na zako dada Filomena

Asante
 
Last edited by a moderator:
Tatizo lenu hapa ni kule kuka wachumba kwa miaka mingi amekuzoea umechuja thamani yako ungekuwa mke angekuwa na hofu maana uchumba unaweza kuvunjika muda wowote kwa hiyo pima mahusiano yenu hayo halafu chukua hatua
 

Asante sana kwa ushauri..,. God bless u
 
Pole sna.ila waswahili wanasema.dalili za mvua nimawingu basi hapo hakuna future inakubidi umuombe mungu akupatie mwezi unaendananae kuliko wewe kumbadilisha.ukisubiri subiri utakuja kujuta humeshaharibu mfumo mzima wa maisha yako.mtu hujilekebisha mwenyewe na mungu wake.
 
Piga chini huyo jamaa hatakufaa kabisa kuwa mmeo
 

Ni mapenzi tu double R ninakazi nzuri najitosheleza...
 
Siku 3 za weekend unaona nyingi, vipi kuhusu 'hadi kifo kiwatenganishe'?

Dhumuni la uchumba ni kuchunguzana, umeshamjua chukua hatua mwenyewe.

Usifikiri atabadilika, maana kama kashindwa kuwa 'at his best' wakati wa uchumba; unategemea akishakuweka ndani ndio ataboreka?

Kumbuka ni maisha yako, na beneficially wa kwanza baada ya Mungu ni wewe na sio mashosti au wazazi au mtu mwingine. Ni bora ukosee kwa yule anayejitahidi kuficha mapungufu yake kuliko huyo asiyejali hisia zako tangu mwanzo.

Siku njema.
 
Ameshaona hauwezi kumwacha,ila hakuna mtu anaeweza kumbadilisha mtu zaidi ya mtu kuamua kubadilika,
 
Si wewe umbadilishe,ila yeye mwenyewe akubali kubadilika......huwezi kumbadilisha mtu hata siku moja,kama ni mlevi,mgovi,mnyanyasaji u better liv with tht..jambo muhimu unalotakiwa kujua ni "some dreams were'nt meant to come true"........run before its to late.
 
Hatuaminiani na nikienda sehem ntakuwa naulizwa muda wote narudi saa ngapi na kununiwa juu wakati yeye anaenda popote haijarishi kanambia au lah....

umesema mnaishi mikoa tofauti, huwa anajuaje kama umekwenda sehemu? Au huwa unajuaje kama kanuna wakati mnaishi mikoa tofauti? Au mkitembeleana wikiendi baada ya kusalimiana mmoja wenu anakwenda kutembea sehemu?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…