Sasa shosti hapo unataka ushauri gani tena,wakati umeshasema hata weekend ukienda mnagombana?sasa uko tayari mgombane maisha yote mtakayo ishi au mmalizane sasaivi na ujipange upya?
au likua unataka kusikia stahmili wanaumewengine ndio walivyo zidisha maombi? lakini akili kichwani mwako ila kama ulosema ndio alivyo basi hapo ukiolewa na yeye ujue umekoga vumba.............
sidhani kama atakufaa, kama maisha yenu kabla ya ndoa yapo hivyo.. Mkiingia ktk ndoa itakuaje? Fikisha hili jambo kwa wazee na uwaambie umeamua nini.. Kama ni heshima tayari kashajivunjia mwenyewe na ya kwako pia.
Akikuta namba ya baba mkwe wake mtarajiwa ana mind kwa kuwa tu mi mwanaume.Na wanaume ndivyo tulivyo: mtuhumiwa mimi lakini anayefanyiwa upelelezi bibie.
Kuna aina nyingi za mapenzi. Mapenzi yenu ni ya kugombana-gombana. Mkikaa muda mrefu bila kugombana hamjisikii sawa. Ugomvi ni sehemu ya mapenzi yenu. Kama uamini, chunguza sababu zinazowafanya mgombanae kama ni za maana.
Uchumba au kutambulishana si ndoa dada kumbuka. Binafsi nadhani pamoja na kumpenda na hatua mlizokwisha chukua bado na wewe yakupasa ujipende na hiyo ni pamoja na kuwa na mtu anayekupenda na anayekuheshimu
Mara nyingi tunaingia kwenye matatizo ya mapenzi kwa kudhani mwenzetu atabadilika, mwisho wake inakuwa majuto ukiwa tayari uko ndani.
Mimi nadhani Mungu kakuonyesha aina ya mwanamme unayetaka kuolewa naye mapema sasa amua kuvaa au kuvua
.eti "najitahidi sana kufanya kila atakacho hata kama ni cha kunionea ambavyo hamna mwanamke ambaye angemvumilia wakati huo huo" hata kama hujafunguka zaidi yaonekana umezoea KUDHARIRISHWA na unaona ni sehemu ya maisha yako, UTU wa mtu una thamani yake dada na ndoa hujengwa kwa misingi ya amani na mapatano yaliyoridhiwa pande zote mbili, sasa kama we ni kutoa tu na hata usipokee toka kwake nakwambia ipo siku hiyo akaunti yako itaisha afu mkaachana wakati mmefika mbali, ni bora ung'atuke sasa naamnini yupo wa kukufaa ukiiendea njia sahihi: "WAWILI WASIPOPATANA HAWAWEZI KWENDA NJIA MOJA"
thnx mamiiakishika sim yako tu mnagombana anakuta nini huko!!!!!!!!!!!!
au wewe hupendi hiyo tabia yake ya kushika sim yako
by the way Long distance relationship aren't that easier
Nimekuwa na mahusiano takribani miaka 5 sasa tatizo ni huyu mwanaume wangu ambaye sasa ni mchumba kutokana na familia zote mbili zinafahamu kuhusu uchumba wetu kwa bahati mbaya tunakaa mikoa tofauti.
Kitu ambacho naomba ushauri hapa ni kuwa huyu mtu najitahidi sana kufanya kila atakacho hata kama ni cha kunionea ambavyo hamna mwanamke ambaye angemvumilia wakati huo huo amenifanya nisimwamini kwan nishamkuta na matukio kadhaa ambayo navumilia sana nikijua mwenzangu atajirekebisha sasa imefikia hatua hatuwezi kukaa wiki hatujagombana na tukitembeleana cha kwanza kushika sim yangu yaan hapo tutagombana mpaka hiyo wikiend inakuwa chungu unatamani asingekuja au nisingeenda na ameshaji engage na wasichana ambao tukiwa wote anawablock ili nisijue kinachoendelea bahati mbaya hata afanye hivo watamtafuta tu hata kwa namba nyingine wapendwa nahitaji ushauri wenu yaan naumia sana coz nimemrekebisha nimechoka na vitendo vya yeye kutaka afanyiwe anachotaka afu ye anafanya tofauti nimechoka.
Nimefikia hatua ya kuleta hapa coz cna wa kumueleza coz hataki hata hao rafiki zake niwaambie chochote kuna kaka ake nilikuwa namueleza nahisi amenichoka so naumia sana kukaa navyo naogopa kumueleza ndugu yangu wa karibu coz napenda aendelee kuheshimiwa kusiwe na chuki.
NAMPENDA NA ANALIJUA HILO
NB. Ushauri tafadhali naolewa soon na huyu mtu.
Kugombana kwa sababu ya usaliti hiyo ni serious issue sio ya ku symplify kuwa maisha yao ni ya hivyohivyo.Wangekuwa wanagombana kwa visababu vidogo sawa. Dada anapaswa atafakari mstakabali wa uhusiano wao..Kimsingi kama walivyoshauri wengine ni vema asitishe uhusiano wao. Kwa kuwa anampenda hii si hatua nyepesi kuchukua lakini kwa kupima faida/hasara za kuendeleza uhusiano huo, kuachana yaweza kuwa the best solution, at least kwa sasa.
Dada huna pa kuupeleka huu upendo wako unakostahili?NAMPENDA NA ANALIJUA HILO
Kosa kubwa sana ambalo hua mnajidanganya ni kuwa mnadhani kuwa kuna mtu anaweza kumbadilisha yoyote yuleNB. Ushauri tafadhali naolewa soon na huyu mtu.
Asante watu8
Usichokipenda usimfanyie mwenzio....
akishika sim yako tu mnagombana anakuta nini huko!!!!!!!!!!!!
au wewe hupendi hiyo tabia yake ya kushika sim yako
by the way Long distance relationship aren't that easier
Asante.... naweza nikasema tuachane hata nikiwa mbali atapanga safari muda huo huo kuomba msamaha na kusema hatorudia na hayuko tayari kunipoteza.
Huwa nasema labda anadhani na mimi nafanya ndio maana ananifanyia hivo. Anyway thnx alot
Kwahiyo unampango wa kunipiga kibuti?
Niambie kabisaa mapema nifanye yangu!!