NB. Ushauri tafadhali naolewa soon na huyu mtu.
Nahisi kama umefanywa ndondocha au akili yako haina akili....
Wanawake wengine huwa mnakera sana, ngoja sisi wanaume tuendelee kuwatumia tu hadi akili ziwakae sawa.
Kuna aina nyingi za mapenzi. Mapenzi yenu ni ya kugombana-gombana. Mkikaa muda mrefu bila kugombana hamjisikii sawa. Ugomvi ni sehemu ya mapenzi yenu. Kama uamini, chunguza sababu zinazowafanya mgombanae kama ni za maana.
Nimekuwa na mahusiano takribani miaka 5 sasa tatizo ni huyu mwanaume wangu ambaye sasa ni mchumba kutokana na familia zote mbili zinafahamu kuhusu uchumba wetu kwa bahati mbaya tunakaa mikoa tofauti.
Kitu ambacho naomba ushauri hapa ni kuwa huyu mtu najitahidi sana kufanya KILA ATAKACHO hata kama ni cha KUNIONEA ambavyo hamna mwanamke ambaye angemvumilia wakati huo huo amenifanya nisimwamini kwan nishamkuta na matukio kadhaa ambayo navumilia sana nikijua mwenzangu atajirekebisha sasa imefikia hatua hatuwezi kukaa wiki hatujagombana na tukitembeleana cha kwanza kushika sim yangu yaan hapo tutagombana mpaka hiyo wikiend inakuwa chungu unatamani asingekuja au nisingeenda na ameshaji engage na wasichana ambao tukiwa wote anawablock ili nisijue kinachoendelea bahati mbaya hata afanye hivo watamtafuta tu hata kwa namba nyingine wapendwa nahitaji ushauri wenu yaan naumia sana coz nimemrekebisha nimechoka na vitendo vya yeye kutaka afanyiwe anachotaka afu ye anafanya tofauti nimechoka.
Nimefikia hatua ya kuleta hapa coz cna wa kumueleza coz hataki hata hao rafiki zake niwaambie chochote kuna kaka ake nilikuwa namueleza nahisi amenichoka so naumia sana kukaa navyo naogopa kumueleza ndugu yangu wa karibu coz napenda aendelee kuheshimiwa kusiwe na chuki.
NAMPENDA NA ANALIJUA HILO
NB. Ushauri tafadhali naolewa soon na huyu mtu.
Kugombana kwa sababu ya usaliti hiyo no serious issue sio ya kusymplify kuwa maisha yao ni ya hivyohivyo.Wangekuwa wanagombana kwa visababu vidogo sawa. Dada anapaswa arafakari mstakanali wa uhusiano wao..Kimsingi kama wslivyoshauri wengine ni vema asitishe uhusiano wao. Kwa kuwa anampenda hii si hatua nyepesi kuchukua lakini kwa kupima faida/hasara za kuendeleza uhusiano huo, kuachana yaweza kuwa the best solution, at least kwa sasa.
akishika sim yako tu mnagombana anakuta nini huko!!!!!!!!!!!!
au wewe hupendi hiyo tabia yake ya kushika sim yako
by the way Long distance relationship aren't that easier
Kwa nini mabint mkiahidiwa ndoa uwezo wenu wa kufikiri unayeyuka?