Naomba ushauri pls pls......... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba ushauri pls pls.........

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mwana Mpotevu, Feb 20, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Wanajamvi
  Nilikuwa na Mpenzi wangu ambaye tumekuwa katika mapenzi kwa muda mrefu sanaa, ni karibu miaka sita. katikati ya uhusiano wetu alipata ujauzito na tuna mtoto mmoja ana miaka minne lakini hatujaoana. kuanzia mwaka jana tabia za huyo mpenzi wangu zimekuwa zikibadilika sana na inaonekana kama amekuwa na kiburi kwa kiasi kikubwa na hakuna tena mapenzi kama zamani. Kutokana na hali hiyo na jitihada za kuokoa penzi letu ninavyoona linazidi kwenda kombo, nimeamua kuanzisha uhusiano na dada mwingine ili ikiwezekana nije nifunge naye ndoa huku nikiangalia mwelekeo wa yule wa kwanza pia kama atabadilika na kurejea kwenye mstari kama zamani au la.

  Uhusiano wangu mpya una kama mwaka mmoja kasoro, Nilimwambia ukweli huyu mpenzi wangu mpya kwamba nina mtoto toka kwa mpenzi wangu wa awali ambaye naona kama mahusiano yanakwenda kombo. Kwahiyo tumeingia katika mapenzi huku akijua kuwa nina mtoto mmoja na yeye akaniambia ana mtoto mmoja alizaa miaka sita iliyopita na mtoto huyo anaishi na dadake kwa sasa.

  Katika siku za hivi karibuni, huyu mpenzi wangu mpya amefanya kitu ambacho ndio kimenisukuma kuomba ushauri hapa jamvini. Amemuandikia mpenzi wangu wa awali ujumbe kwenye FB (inbox) akimwambia kuhusu mimi kuwa na uhusiano na mdada mwingine (hakutaka kujitaja kwamba ni yeye lakini description alizozitaja za huyo mdada ni wazi alikuwa anajitaja yeye mwenyewe). Na mbaya zaidi amemwambia mambo mengi kuhusu mimi na yeye na pia amemwambia namna (huyo mpenzi wangu mpya) alivyokuja kwangu na vitu alivyovikuta na hata ramani ya vyumba vyangu ilivyo huku akidai kahadithiwa na mpenzi wangu mpya yote hayo (lakini ukweli ni yeye mwenyewe mwandishi wa msg ndie huyo mpenzi wangu mpya).

  Mwisho akamshauri eti aachane kabisa na mimi maana sitaweza kumsaidia lolote katika masiaha yake na aangalie maisha mapya. Mimi nilionyeshwa kwa macho yangu hiyo msg na gf wangu wa mwanzo na jinsi ilivyoandikwa sikuwa na shaka nikajua fika kuwa aliyeandika ni yuleyule mpenzi wangu mpya maana ameandika mambo ya ndani sanaaaaa ambayo si rahisi mtu zaidi ya sie wawili kujua.

  Nilipojaribu kumuuliza yule mpenzi wangu mpya kuhusu ujumbe ule, akakana na kusema kuna siku alikutana na rafiki yake mmoja akamdokeza kuhusu uhusiano wetu, na akasema huenda huyo rafiki yake ndio aliyeandika hayo yote na akawa akijiapiza kuwa huyo rafiki yake eti anataka kusababisha uhusiano wetu mimi na yeye ufe. Nashindwa kuamini sana kwa jinsi mambo yaliyo kwenye ule ujumbe yanavyoeleza maana ni mambo ya ndani sana kiasi kwamba sio rahisi kwa mtu kumwabia rafiki yake mambo hayo.

  Najikuta nimechanganyikiwa nini lengo la huyu mpenzi wangu mpya kuandika jambo kama lile kwa mpenzi wangu wa zamani. Sijawahi kumdokeza kwamba nataka kumuoa lakini tumekuwa katika mapenzi muda sasa na ukweli natafuta mtu wa uhakika nitayetaka kumuoa. Naomba ushauri wenu huyu mtu wa pili ananifaa kweli na nini lengo lake kuandika mambo yetu kwa mpenzi wangu wa zamani??

  Naombeni msinishambulie kwa kuwa na wapenzi wawili maana nimewapa scenario iliyonifanya niingie katika uhusiano na huyu wa pili baada ya yule wa kkwanza kubadilika kitabia, sasa huyu wa pili naye ananichanganya nashindwa kumuelewa sasa.
   
 2. mdoe

  mdoe JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 436
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo wa pili anagombania kushika main position. Unadhani anafurahia kukaa kwenye standby? Anachofanya usimlaumu. Ni katika harakati za kushika namba moja.
   
 3. double R

  double R JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 1,355
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  Hayo mambo ya kawaida kwa wake wenza. chagua mmoja uanze upya. ila nina walakini na huyo wa pili, mara nyingi mwanamke akishazaa mwanaume yoyote atakayeonesha harufu ya kuoa humng'angania kisawasawa hata kama hampendi. Huyo mliyezaa naye anaweza akawa anakupenda nahisi angekuwa anatafuta sababu muaachane hiyo ilitosha kabisa kusema "it's over"
   
 4. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Fanya Home work yako kwani hakuna kosa kama kosa la kukosea kuoa mtu asiyestahili. Ukiona anayefaa endela na huyo ukiona hawafai wote. Achana nao Kuanza upya si ujinga usioe only because una please mtu utakuja juta sana huko mbeleni. Ndoa ni for life wala huwezi kuja jisahihisha baadae, ikisha toka imetoka
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Thanks Double R, tatizo huyu wa kwanza amebadilika sana hadi nakata tamaa, anadiriki hata kuanzisha kitu kama mradi bila kunishirikisha hata kidogo na nikimuuliza anasema kila mtu ana mambo yake binafsi. Sio kwamba ningemkataza isipokuwa kuniarifu tu ingetosha na zamani hakuwa hivi. Hiyo ndio ikanifanya hata kutafuta ustaarabu mpya pamoja na kuwa tuna mtoto, lakini nashukuru sana kwa ushauri wako
   
 6. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Asante Mihayo kwa ushauri na nimejitahidi kufanya home work hadi kichwa kinauma maana huyu wa pili kitendo chake cha kumuandikia yule wa kwanza ndo kikanikatisha tamaa kabisa maana sijui nia yake nini
   
 7. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  hiyo njia anayotumia ndio inanipa shaka kama ina heri ama inalenga kuleta shari zaidi
   
 8. E

  Edo JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Inanikumbusha jamaa yangu mmoja aliyesema akina dada siku zote waambie uongo kwa kwenda mbele, ukijidai kuweka wazi kila kitu ndio matatizo haya yaliyokukuta ! Sasa we tulia maana wote wawili wanaijua ishu, we kaa angalia reactions za kila mmoja, wewe unakua kama jaji wao hapo ndo mahali pa wewe kupata sifa!
   
 9. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  uwezi ukasummarize?
   
 10. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  kwa wenye tabia za madenge kuandika mistari ya bongo fleva kwenye mtihani ni ngumu kusoma, na hata wakisoma hawaelewi maana wamezoa njia za mikato
   
 11. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Ni kweli inawezekana kumwambia kwangu ukweli huyu dada wa pili ikawa imeniponza maana kaamua kufanya mambo yasiyoeleweka kabisaaaaa
   
 12. m

  mkazamjomba Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sioni hata mwenye kustahili ndoa kama anaanza kutoa siri hafai tafuta mwenye kifua kaka
   
 13. RR

  RR JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,719
  Likes Received: 206
  Trophy Points: 160
  Anakusaidia kumwondoa huyo wa kwanza ili yeye peke yake....si una mpango wa kuoa? Chezea kuolewa wewe!
   
 14. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Kaazi kweli kweli!
  Sasa huzuni yako kumbe yule wa 'zamani' bado yuko kwa picha? Mjini kugumu sana jamani, kha!
   
 15. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Uko kwenye mtanziko mkubwa..ushauri wa kwanza - tulia punguza kabisa mawasiliano na huyu wa pili ili uone reaction yake,usifanye papara.Kwa Huyu wa kwanza jishughulishe na mtoto wako basi, acha aendelee na maisha yake kama ambavyo amekudokeza.

  Hakuna jambo baya kama ku-deal na watu wasiojali feelings zako...hawajali kama vitendo wanavyovifanya vinakuumiza au la.Tulia mkuu..mambo mazuri hayataki papara
   
 16. LD

  LD JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Inawezekana huyo wa kwanza anakuona unamzingua tu, ndio maana anaona ajianzishie miradi ili awe na uwezo wa kujikimu kimaisha yeye na mtoto wake. Kwa haraka haraka naweza kusema wewe ndio huna mapenzi ya kweli kwake kwa sababu hujawa mvumilivu.

  Je ni hatua gani umechukua kumshauri na kuongea juu ya hicho unachokisema kabadilika? Je wewe ulipoanzisha uhusiano mwingine ulimwambia? Na je kama vile wewe ulivyo na uhusiano na mtu mwingine yeye anao uhusiano na mtu mwingine zaidi yako?

  Umemshauri na kumuonya kwa muda gani hata ukaamua kumchanganya kwenye uhusiano? Umemwambia kwamba tabia zako mbaya siwezi kuwa na wewe ila nina mwanamke mwingine?

  Mbona yeye alipoona huo utumbo wa huyo binti, hakufanya ushari wala kutukana, wala kukutukana wewe akakuonesha?

  Think!!!!! Mi naona wewe ndio hujielewi hata kidogo. Huyo mama mtoto wala hana makuu, itakuwa kakusoma kakuona waru waru akaamua ajiimarishe kimaisha tu.

  Kama vipi mweleze ukweli umuache alee mtoto wake, na wewe uendelee na huyo mshari wako. Tena kwa taarifa yako huyo binti wa pili hana hana roho ya kulea mtoto ambaye hajamzaa........asingeweza kukuanika hivyo kwa mama mtoto wako. Ahiii angalia manake mie wanaume Vigeu geu na wasio na msimamo wa maisha katika mahusiano nawachukia na kuwaogopa kama Malaria :(
   
 17. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0

  mpendwa LD umeongea ,maneno ya msingi sana,ubarikiwe,isipokuwa kwa hako ka red tu,du,tumekukosea nini?
   
 18. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  asante kwa maneno yako mazuri nayaheshimu. sikuwa na nafasi ya kusema kila kitu hapa maana ningechukua nafasi kubwa hata kusoma ungeshindwa. lakini nimetoa mfano mmoja tu wa mambo anayonifanyia huyo mpenzi wangu wa awali, lakini kuna mengi ikiwa ni pamoja na hata kufukia kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki yangu na niligundua hilo na akaomba radhi. yako mengi lakini pamoja na yote hayo bado nimekuwa mvumilivu mwaka wa sita huu hadi ninapoona kama huko tunakoelekea si shwari na umri wa kuoa unazidi kuyoyoma ndipo nikaona niangalia upande mwingine. Nimeshakaa naye several times na kuongea naye, tuki-solve kitu leo, after sometime kinarejea upya hadi najikuta nachoka. hadi kufikia kuanzisha uhusiano mpya nimevumilia mengi sanaa toka kwake lakini nimefikia kukata tamaa
   
 19. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  asante mkuu nitakaa chini na kujipanga upya kisha kuchukua hatua
   
 20. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kuanza upya si ujinga!
   
Loading...