Naomba ushauri, niende kozi gani kati ya hizi?

Jan 22, 2021
7
3
Mimi nimechanguliwa TIA (Human resource) na NIT (Procurement and logistics management)
Naomba ushauri wenu kwa wenye uzoefu ni confirm wapi
 
Nenda NIT, hiyo ni fani ya afisa Manunuzi! Tanzania ni nchi inayoendelea hivyo manunuzi huwa hayaishi, alafu ukiwa baadhi ya sehemu wale unakofanya manunuzi unapata bonus kwa kawaungisha.

Naishi jirani afisa manunuzi wa Taasis moja hivi, ana miaka 2 tu tangu atoke chuo, ameshajenga ya mbele na amenunua prado! Nenda huko aisee!

NB: Hata hivyo kama una Interest na kuwa HRO basi nenda huko TIA, ukatimize doto zako!
 
Mimi nimechanguliwa TIA (Human resource) na NIT (Procurement and logistics management)
Naomba ushauri wenu kwa wenye uzoefu ni confirm wapi
Ningekuwa mimi ningechagua NIT, na sababu ni kwamba siwezi soma HR.Kwanza naangalia namba ya vyuo vinavyotoa hizi kozi za Human Resources ni nyingi.kwahyo kama ni jambo la ajira ujipange kwenye ushindani japo wanasema kila mtu na nyota yake.Procurement and Logistics management inaweza isiwe kozi pendwa lakini binafsi kwa machaguo yako inaweza kukulipa hapo badae.

Jambo la muhimu chagua kile moyo wako utapenda au fanya hivi angalia description za kila kozi, changanua contents zake.Then,chagua kozi itayokizi mipango yako.

Kingine unaweza zingatia ubora wa sehemu(chuo) husika unapoenda kusomea hiyo kozi japo sio la muhimu sana
 
Ningekuwa mimi ningechagua NIT, na sababu ni kwamba siwezi soma HR.Kwanza naangalia namba ya vyuo vinavyotoa hizi kozi za Human Resources ni nyingi.kwahyo kama ni jambo la ajira ujipange kwenye ushindani japo wanasema kila mtu na nyota yake...
Mkuu mimi pia nina mtazamo kama wako, nimejaribu kufocus suala ajira baada ya chuo na maruprup ya hapa na pale! Fani ya HR inatolewa na vyuo vingi sana na mpaka sasa ni moja ya fani ilojaza joblee wengi sana mtaani!

Pia katika baadhi ya Halmashauri wamekuwa wakichuliwa watendaji wa mitaa na kata na kubadilishwa kuwa maofisa utumishi, lakini kwa upande wa Maofisa manunuzi hilo jambo si rahisi!
 
Nenda NIT, hiyo ni fani ya afisa Manunuzi! Tanzania ni nchi inayoendelea hivyo manunuzi huwa hayaishi, alafu ukiwa baadhi ya sehemu wale unakofanya manunuzi unapata bonus kwa kawaungisha...
Hata kuwa Hr nayo inalipa,mtu hawezi ajiriwa mpaka hr ahusike tena ukiwa kwenye maviwanda basi kila siku ukiingiza muajirwa mpya unachako mfukoni
 
Hata kuwa Hr nayo inalipa,mtu hawezi ajiriwa mpaka hr ahusike tena ukiwa kwenye maviwanda basi kila siku ukiingiza muajirwa mpya unachako mfukoni
Sawa ila kwa upande HR anaeyezipata sana ni Boss wa Idara, lakini kwa watu wa manunuzi usijeshangaa ukavuta mgao wa mabati kama kule morogoro!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom