Naomba ushauri niache kazi au niendelee nayo

wasikupoteze wewe.... jiamini na achana na hiyo kazi.. mungu ndiye anayejua maisha yako yataishaje.. huwezi jua kupitia kulala hapo yakaibuka mengine.. achana nayo na tulia na ndoa yako.. hope kazi utapata tu!
 
Nionavyo mimi wa kulitatua hilo tatizo ni wewe na mume wako tu, hakuna mwingine. Hebu kaeni chini mzungumze vizuri, hebu jaribu kumshirikisha kwenye hiyo hofu yako kuhusu maisha baada ya kuacha kazi,
Jadilianeni kwa makini nini/kazi gani ufanye ambayo itakua na afya na kutoathiri mapenzi yenu, nafikiri ukimsikiliza vizuri unaweza kua na maamuzi sahihi ya kufanya.
 
Yaani bado hujamfuata mmeo tu?? Sikiliza we shemeji huyo mume anakupenda ndo maana anakuambia ukweli, kaa chini mjadili mueleze upo tayari but mmpange mtaishije baada ya hapo, we unafikiri kujipikia, kujifulia nk. eti mwenza yuko kazini mchezo!
 
Mume ndie aliyekusomesha hadi ukafikia kupata kazi?! If no, nakushauri piga kazi, heshimu jinsi wazazi/walezi wako walivyotimiza wajibu wao kukusomesha na wewe ilikuwa haki yako usomeshwe
 
Its very easy, mwambie mwenzi wako akutafutie 5M. akikukabidhi asiulize unafanyia nn, ila ww jipange na cha kuifanyia itakuzalishia hiyo laki 4/5 uipataye monthly.
 
Nimeishi muda mrefu bila kazi, maisha yalikua magumu mno, ndio maana nilikubali kufanya hii kazi licha ya kuwa na masharti magumu

kwa hili sikushauri uache kazi, ila nnachokushauri ongea na mumeo mkumbushe jinsi mlivyotaabika kipindi huna kazi, na umuombe akuvumilie ukiwa unaendelea kutafuta kazi nyingine, na ukazane kutafuta nyingine tena sikuhizi ni rahisi kazi zote lazma utaziona zimetanganzwa mitandaoni na hata kuomba unaomba online kwahiyo jitahidi kufatilia iko siku utabahatisha, huku ukiendelea kumuomba Mungu ampe mumeo uvumilivu na akupatie kazi nyingine kwa haraka
 
hii shule itakuwa ya taasisi ya kidini

alafu mambo ya kusema huoni kama utapata kazi tena unayatoa wapi?

kwamba unaijua kesho yako
 
Kazini wanajua wananipa ruhusa jmos narudi jpili jion lakini mume wangu haitaki kazi ya hivi
mmeo anaona unampa show time.. .,' mwambie mmeo awe anakuja shule umpetpet hku unaangalia wap utaweza pata kaz nyngne au mmeo akusaidie kutafta ili umtoe wacwac....
 
Nimeishi muda mrefu bila kazi, maisha yalikua magumu mno, ndio maana nilikubali kufanya hii kazi licha ya kuwa na masharti magumu
mmeo nae hatumii akil ameona saiv kunavijsent kidgo ameshalzika atumie akil kuna maisha baada ya ndoa maisha magumu nahyo ndio challenge mojawapo ya ndoa kaachin mueleweshane maisha yalvyo aache ulimbukeni kma ataweza kuhudumia familia ipasavyo mckilze ila baadae mtajutia hyo nafac kunamsemo unasema acha kaz kma umepata kaz!!alamsiki!!
 
Mshika mawili moja humponyoka... Kazi ya masharti magumu hivyo bado unaipenda?? Kwa nini usipanue mawazo ukatafuta hata biashara yako binafsi ujiajiri?
 
Kwa ujumla kuna maisha baada ya kazi. Kazi usiache kuanza kabla ya kupata kazi nyingine. Jitahidi kupitia magazeti yatakusaidia kukubadilisha au kupata wazo jipya la kuongeza kipato ukiwa hapohapo ulipo kikazi angalia fursa zinazokuzunguka
 
Back
Top Bottom