Naomba ushauri ndugu yangu kapata Kesi ya Kujeruhi

EL ELYON

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
1,563
1,886
Wakuu mmebarikiwa Sana na Mungu wa Mbinguni hakuna laana.

Ndugu yangu anatuhuma za kesi ya KUJERUHI ambayo anasema ye hakuhusika Ila kuna rafiki yake ndiye kahusika.

Kwani wakati tukio linatendeka ye hakuwepo Huko alikuwa wilaya nyingine NDIPO jamaa akachomwa kisu cha mgongoni sasa nduguze wamefungua kesi ambayo itasomwa tarehe 25 mwezi ujao.

Hapa naomba ushauri wa kumsaidia yule ndugu hasa nahitaji ushauri wa kisheria na wa kawaida tu.

Asanteni.
 
Athibitishe kama hakuwepo eneo siku ya tukio.

Namna ya kuthibitisha ni kwa kutumia Cyber report kwamba siku ya tukio simu yake ilikuwa inasoma eneo gani?
 
Athibitishe kama hakuwepo eneo siku ya tukio.

Namna ya kuthibitisha ni kwa kutumia Cyber report kwamba siku ya tukio simu yake ilikuwa inasoma eneo gani?
Mkuu,kuhusu ithbati kwa kutumia simu ili kutambua kua mtuhumiwa hakua eneo hilo,

Je kutakua na uhakika gani wa nani alikua anaitumia hiyo simu ya mtuhumiwa kwa wakati huo?
 
Mkuu,kuhusu ithbati kwa kutumia simu ili kutambua kua mtuhumiwa hakua eneo hilo,

Je kutakua na uhakika gani wa nani alikua anaitumia hiyo simu ya mtuhumiwa kwa wakati huo?

Sasa hapo ni kubet tuu. kwani hao wanaosema jamaa ndio kafanya tukio wana evidence gani?

Pili mtoa mada anasema aliefanya tukio ni jamaa uq ndugu yake. Sasa huyo mwenye kesi kwanini asiwe shaidi ya mahakama kuwa kosa hakufanya yeye liyefanya ni fulani
 
Back
Top Bottom