Naomba Ushauri: Namchukia ila nimempa mimba

Ricardo Damiano

Senior Member
Nov 4, 2011
103
79
Habari za jioni ndugu na wadau wa jukwaa hili maridhawa,

Nia ya kuandika uzi huu ni kuomba ushauri juu ya maisha yangu ya sasa ambapo nategemea mtoto na dada mmoja ambaye kiukweli ni basi tuu ila sikuwa na future naye na ni vile tamaa za mwili nikajikuta nimempa mimba, kiukwel kutoa mimba sitaki kufanya hivyo na pia huyu dada amekwishakua na mtoto mmoja tayari na mwingine.

Swali langu ni; Je huyu mtoto hata akizaliwa nitakuwa na mapenzi nae kweli maana hivi sasa sitamani hata hio mimba ajifungue, yaani kiukwel huyu dada namchukia lakini ndio hivyo.

Nisaidieni ushauri

Natanguliza shukrani.
 
Mtoto lazima umpende tu, na usijaribu kumtelekeza cuz utakuja kujuta baadae, msee ile mimba amebeba yeye sio wewe, ww jukumu lako ni kumpa matunzo tu tena pia sio kila siku, so wewe mbona huna mzigo hapo? au tatizo liko wapi?
 
Ulichokitafuta umekipata sasa.

Nakushauri leo hiyo mimba pia mtoto akizaliwa onesha mapenzi kwake sababu ni wako Huyo.

Tafakari chukua hatua
 
Mtoto lazima umpende tu, na usijaribu kumtelekeza cuz utakuja kujuta baadae, msee ile mimba amebeba yeye sio wewe, ww jukumu lako ni kumpa matunzo tu tena pia sio kila siku, so wewe mbona huna mzigo hapo? au tatizo liko wapi?
tatizo ni kwamba sikuwa tayari kuanza future na mwanamke ambaye tayari ana mtoto na mwanaume mwingine na mwanaume huyo akiwa angali hai
 
Mtoto atakaye zaliwa anaweza kuwa "Nyerere, Nelson Mandela, Akawa mtu muhimu sana kwenye maisha hata mkombozi wetu juu ya uchumi na hali ngumu ya kaisha"? Usiizime ndoto ya mafanikio yake mtoto kungali mapema hivi
hili ndilo nikilfikiriaga linanitia moyo..maana mimba ina miez 6 sasa..na nilitaka kuitoa tangu ina mwez mmoja..na nimekuwa nikitamani kuitoa ever since
 
  • Thanks
Reactions: Luv
tatizo ni kwamba sikuwa tayari kuanza future na mwanamke ambaye tayari ana mtoto na mwanaume mwingine na mwanaume huyo akiwa angali hai
Hahaha... Wewe jamaa bado haujawa na point,
mbona ndio fasheni ya skuizi hiyo? Unampa mimba demu anakaa kwao, wewe unakuwa unatuma matumizi maramojamoja kwaajili ya mwanao, na haina uhusiano wowote na mapenzi yenu, tena unaweza ukamtema alafu ukawa unatunza mtoto tu baaas... Umeelewa? Sio lazima mtu ukimpa mimba ndo uishi nae,
mfano mzuri fanya kama alivyofanyiwa kwenye mtoto wake wakwanza
 
Mtt atakuja kubadili hisia zako mkuu hamna kitu kinaleta faraja kwny mahusiano km mkishakuwa na mtt
 
Suala la kujiuliza kwanza wewe pekee ndie uliekuwa na uhusiano nae? subiri mtoto azaliwe halafu kaangalie DNA kama wako lea mtoto wako na kama wa mwenzio hapo utaamua nini la kufanya. Kuna watu husingiziwa wizi kumbe wala sio wizi bali walipita eneo wakati tukio likitokea ndio wao huonekana wahusuka wa wizi.
 
Hahaha... Wewe jamaa bado haujawa na point,
mbona ndio fasheni ya skuizi hiyo? Unampa mimba demu anakaa kwao, wewe unakuwa unatuma matumizi maramojamoja kwaajili ya mwanao, na haina uhusiano wowote na mapenzi yenu, tena unaweza ukamtema alafu ukawa unatunza mtoto tu baaas... Umeelewa? Sio lazima mtu ukimpa mimba ndo uishi nae,
mfano mzuri fanya kama alivyofanyiwa kwenye mtoto wake wakwanza
Upo tayari na wewe kufanya hivi kwa utakayekuwa umezaa nae?

hebu muwe na mnatumia akili, vipi mzazi wako wa kiume angefanya hivi kwa mama yako?

unajua jinsi gani mwanamke anateseka kulea mtoto peke yake? unajua jinsi mtoto anavyokuwa mnyonge anapokuwa yupo mbali na mzazi mmoja ilhali huyo mzazi wake yu hai.

Acheni kujifikiria nyie tu wala kumfikiria mwanamke kuwa unamkomesha, kwa maamuzi hayo anayeteseka ni mtoto.

Kama unaona huna future na mwanamke mwambie kabisa "kwa sasa jitahidi usipate ujauzito maana bado sijajipanga kulea ngoja tujipange kwanza" hapo hata likitokea la kutokea unaweza kulaumu.

Maamuzi mengine mtu uwe unawaza vipi kama dada yangu ndio anafanyiwa hivi
 
Suala la kujiuliza kwanza wewe pekee ndie uliekuwa na uhusiano nae? subiri mtoto azaliwe halafu kaangalie DNA kama wako lea mtoto wako na kama wa mwenzio hapo utaamua nini la kufanya. Kuna watu husingiziwa wizi kumbe wala sio wizi bali walipita eneo wakati tukio likitokea ndio wao huonekana wahusuka wa wizi.
hili ni kweli mkuu tho nipo certain mimba ni yangu..
 
Upo tayari na wewe kufanya hivi kwa utakayekuwa umezaa nae?

hebu muwe na mnatumia akili, vipi mzazi wako wa kiume angefanya hivi kwa mama yako?

unajua jinsi gani mwanamke anateseka kulea mtoto peke yake? unajua jinsi mtoto anavyokuwa mnyonge anapokuwa yupo mbali na mzazi mmoja ilhali huyo mzazi wake yu hai.

Acheni kujifikiria nyie tu wala kumfikiria mwanamke kuwa unamkomesha, kwa maamuzi hayo anayeteseka ni mtoto.

Kama unaona huna future na mwanamke mwambie kabisa "kwa sasa jitahidi usipate ujauzito maana bado sijajipanga kulea ngoja tujipange kwanza" hapo hata likitokea la kutokea unaweza kulaumu.

Maamuzi mengine mtu uwe unawaza vipi kama dada yangu ndio anafanyiwa hivi
aliambiwa but bado imetokea na nililisisitiza kabisa staki mtoto ila nivile sijui sikufikir kabisa kuhusu mpira..ndio maana nimejikuta namchukia huyu dada maana ni kama makusudi
 
  • Thanks
Reactions: Luv
aliambiwa but bado imetokea na nililisisitiza kabisa staki mtoto ila nivile sijui sikufikir kabisa kuhusu mpira..ndio maana nimejikuta namchukia huyu dada maana ni kama makusudi
Sasa hayo makusudi mmeyafanya wote, wewe hukutumia mpira na yeye alikuwa siku za hatari mkavuna mlichokipanda.

Hakuna kuchukiana pendaneni kama mwanzo.

Kwani ulivyomtongoza ulimwambia umempenda au umemtamani!!?

tena mumshukuru Mungu mnapata mtoto, je mngepata maradhi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom