Naomba ushauri na mawazo kwenye kilimo na ufugaji

bwegebwege

bwegebwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2010
Messages
1,037
Points
1,195
bwegebwege

bwegebwege

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2010
1,037 1,195
Waheshimiwa habarini za kazi!!

Baada ya kutumika serikalini n akwenye mashirika mengine nimeweka mkakati wa kujiajiri ifikapo 2015 na nimedhamiria kujikita katika KILIMO NA UFUGAJI!
KILIMO
Katika kilimo nataka kujishughulisha na mazao yafuatayo
1. Mahindi na Mpunga
2. Mihogo
3. Matunda ( Maembe, Mananasi, Mapapai)
4. Pilipili (Hoho, Pilipili Kali (Pilipili ndefu na pilipili mbuzi)
5. Mboga (Nyanya, Vitunguu, Carrots)
6. Uyoga
UFUGAJI
Katika sualal la ufugaji natarajia kujishughulisha na ufugaji wa:-
1. Ngombe wa Maziwa
2. Mbuzi wa Maziwa (wanaozaa mapacha)
3. Nguruwe
4. Kuku wa kisasa (Nyama na Mayai)
5. Kuku wa Kienyeji
MAANDALIZI

Mpango wangu ni kuanza operations ifikapo January 2015, lakini nimejiwekea malengo ya kuanza maandalizi (mfano kutafuta mshamba, kufanya utafiti, kuandaa zana na maeneo ya kazi, kuimarisha mtaji etc) kuanzia January 2013 hadi Dec 2014.
Kwa sasa nimeanza kukusanya taarifa muhimu na "kujipanga" kwa ajili ya utekelezaji huo. N akwa kuwa nipo katika mchakato huu naomba msaada wa mawazo kwa wakle ambao tayari wapo kwenye shughuli za namna hii (iwe ni taarifa za mahitaji, wapi pa kupata msaada wa kitaalamu, contacts za wahusika au hata kama kuna mtu Mwenye documented project sample ya related project anisaidie ili nianze kujipanga). Najiandaa pia kufanya ziara kati ya March na May 2013 kenye maeneo mbalimbali ambako kunafanyika miradi kama hii (miradi midogo na ya saizi ya kati) ya watu mmoja mmoja au vikundi ilki kujipa elimu kwa vitendo!! Naomba wenye uzoefu wawasisiane name kwa email ya SELUDM2012@gmail.com au wani-PM humu tuweze kujuzana! Watakaotoa maoni kupitia thread hii nao pia nitawashukuru! Ahasanteni
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,529
Points
2,000
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,529 2,000

Karibu sana kwenye club ya wakulima

Tafuta eneo la kutosha kabisa ili liweze ku-accomodate hivyo vyote, vikiwa pamoja vitapunguza gharama.Hivyo nilivyo weka wino mwekundu nina hakika vinaweza kukaa pamoja.Hilo la kwanza, pili ni vizuri usiwe mbali na shamba lako litakapo kuwepo, pia na umbali wa soko toka shambani kwako. Maji ni kigezo muhimu sana.

Ziara kwa wanaofanya kilimo kama hicho unachotaka kuanza ni muhimu sana, na inabidi ufanye nyingi sana. Anza na mazao ambayo soko lake ni la ndani kwanza. Ukipata nafasi tembelea soko mjinga la kisutu ili uone mboga wanazopenda Wahindi.

Si vibaya ukifuga nyuki na samaki pia.
 
Asante mkuu! Nitazingatia
 
ROKY

ROKY

Senior Member
Joined
May 4, 2011
Messages
180
Points
195
ROKY

ROKY

Senior Member
Joined May 4, 2011
180 195

Ushauri mzuri sana huo.
Hapo kwenye blue, naomba utujuze kama una utaalam kuhusu ufugaji wa samaki, na soko la samaki (tilapia) kwa kwa Dar, na Morogoro.
Asante.
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,529
Points
2,000
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,529 2,000
Ushauri mzuri sana huo.
Hapo kwenye blue, naomba utujuze kama una utaalam kuhusu ufugaji wa samaki, na soko la samaki (tilapia) kwa kwa Dar, na Morogoro.
Asante.
Soko la samaki ni kubwa sana, ili upate data za ukweli waulize jamaa walio kitengo cha Fao pale Kinguruila Moro (nitakupa kwa pm simu zao), mimi nilikwenda na nikapata darasa la saa sita, ila kwa Moro soko la samaki sio kubwa kwa sababu mito mingi kule Moro ina samaki, na Wandamba/Waluguru/Wapogoro/Wambunga hawali samaki wengine nje ya Kamabale, kitoga na kibua teheeeeee. Sato aka Tilapia wana soko sana Dar. Nimeanza na kambale kama 500 hivi, ndio nawaangalia. Ili ubobee ktk hili, nashauri nenda mwenyewe pale FAO, jamaa wako vizuri sana, utafundishwa hadi kufuga samaki wa jinsia moja.

Pia ukiweka mifugo mingine ( isipokuwa swine kama uwezo ni mdogo) ktk shamba moja kama nilivyoshauri utapata faida haraka. Kuku akinya, mbolea yake ni muhimu sana kwa bwawa la samaki, pia ni muhimu kwa mboga kama mchicha,ambao utawalisha kuku wale wale ili watoe mayai bora zaidi na hivyo hivyo ukiwa na ng`ombe wa maziwa watatu wanne hivi. Yaani ecosystem fulani inazaliwa.
 
Asante sana mtaalam, nitajipanga niwatembelee huko Mrorgoro (FAO) hivi karibuni.
 
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
7,045
Points
1,225
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
7,045 1,225
Na mimi nahitaji Mbuzi anayezaa mapacha lakini awe wakienyeji.
 
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
7,045
Points
1,225
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
7,045 1,225
Soko la samaki ni kubwa sana, ili upate data za ukweli waulize jamaa walio kitengo cha Fao pale Kinguruila Moro (nitakupa kwa pm simu zao), mimi nilikwenda na nikapata darasa la saa sita, ila kwa Moro soko la samaki sio kubwa kwa sababu mito mingi kule Moro ina samaki, na Wandamba/Waluguru/Wapogoro/Wambunga hawali samaki wengine nje ya Kamabale, kitoga na kibua teheeeeee. Sato aka Tilapia wana soko sana Dar. Nimeanza na kambale kama 500 hivi, ndio nawaangalia. Ili ubobee ktk hili, nashauri nenda mwenyewe pale FAO, jamaa wako vizuri sana, utafundishwa hadi kufuga samaki wa jinsia moja.

Pia ukiweka mifugo mingine ( isipokuwa swine kama uwezo ni mdogo) ktk shamba moja kama nilivyoshauri utapata faida haraka. Kuku akinya, mbolea yake ni muhimu sana kwa bwawa la samaki, pia ni muhimu kwa mboga kama mchicha,ambao utawalisha kuku wale wale ili watoe mayai bora zaidi na hivyo hivyo ukiwa na ng`ombe wa maziwa watatu wanne hivi. Yaani ecosystem fulani inazaliwa.
Kaka hivi Kambale wanapendwa kweli???

Si ungepanda japo Perege.
 
Bosco Ntaganda

Bosco Ntaganda

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
576
Points
225
Bosco Ntaganda

Bosco Ntaganda

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
576 225
Endelea kutupa taarifa kadiri unavyo piga hatua ndugu. Hakika umechagua fungu jema, Kama mnataka mali mtayapata shambani...
Nami niko njiani, nataka kufanya Kilimo & Ufugaji pia. Kua maskini ukiwa Tanzania ni DHAMBI KUBWA MNO!!
 
matumbo

matumbo

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Messages
7,204
Points
1,250
matumbo

matumbo

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2011
7,204 1,250
Kama una buku sitini sema nikuuzie, usafiri juu yako.
malila unafahamu dawa nzuri ya kuulia magugu shambani??
Na ya kuulia wadudu shambani??

Au sehemu naweza kupata ushauri mzuri wa kilimo kwa hapa dsm.
 
Kunta Kinte

Kunta Kinte

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2009
Messages
3,684
Points
1,500
Kunta Kinte

Kunta Kinte

JF-Expert Member
Joined May 18, 2009
3,684 1,500
Mkuu kama kuna taarifa zingine za ziada ulizo nazo kuhusiana na wazo hili share na mimi tafadhali nami pia nipo interested
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,529
Points
2,000
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,529 2,000
Kaka hivi Kambale wanapendwa kweli???

Si ungepanda japo Perege.
Ukifika pale TAZARA dsm jioni utakuta Kambale ndio wanatamba, kama utapita Ruvu darajani kwenda Chalinze kushoto pale, ukienda FAO kinguluira, kifaranga cha Sato/Perege ni Tsh 30/ lakini cha kambale ni Tsh 150/. Achana na Kambale ukimpata na ugali mchana ameungwa na tetele !!!!

Tatizo la kambale ni kwamba ktk mabwawa ya kujengwa hawazai, muda wa market size ni mrefu zaidi kuliko perege, ila wanaweza kuishi ktk mazingira magumu sana kuliko perege.

Perege wana growth rate kubwa na wako popular kwa sababu wanaweza kufugwa sehemu kubwa ya nchi. Perege wa pilot ninao, sasa nataka kufanya polyculture baada ya majaribio kufanikiwa. Hawa kambale nataka kwa ajili yangu mwenyewe na marafiki wachache.
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,529
Points
2,000
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,529 2,000
malila unafahamu dawa nzuri ya kuulia magugu shambani??
Na ya kuulia wadudu shambani??

Au sehemu naweza kupata ushauri mzuri wa kilimo kwa hapa dsm.
Nenda pale ofisi za kilimo Tazara ili upewe orodha ya magugu na dawa ifaayo kwa kila gugu. Hawa wa njiani wanaweza wasikupe dawa mwafaka. Ngoja nampigia dogo SKU atupe ushauri. Huwa natumia kazini mara chache sana.
 
Kubota

Kubota

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Messages
533
Points
250
Kubota

Kubota

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2012
533 250
Waheshimiwa habarini za kazi!!

Baada ya kutumika serikalini n akwenye mashirika mengine nimeweka mkakati wa kujiajiri ifikapo 2015 na nimedhamiria kujikita katika KILIMO NA UFUGAJI!
KILIMO
Katika kilimo nataka kujishughulisha na mazao yafuatayo
1. Mahindi na Mpunga
2. Mihogo
3. Matunda ( Maembe, Mananasi, Mapapai)
4. Pilipili (Hoho, Pilipili Kali (Pilipili ndefu na pilipili mbuzi)
5. Mboga (Nyanya, Vitunguu, Carrots)
6. Uyoga
UFUGAJI
Katika sualal la ufugaji natarajia kujishughulisha na ufugaji wa:-
1. Ngombe wa Maziwa
2. Mbuzi wa Maziwa (wanaozaa mapacha)
3. Nguruwe
4. Kuku wa kisasa (Nyama na Mayai)
5. Kuku wa Kienyeji
MAANDALIZI

Mpango wangu ni kuanza operations ifikapo January 2015, lakini nimejiwekea malengo ya kuanza maandalizi (mfano kutafuta mshamba, kufanya utafiti, kuandaa zana na maeneo ya kazi, kuimarisha mtaji etc) kuanzia January 2013 hadi Dec 2014.
Kwa sasa nimeanza kukusanya taarifa muhimu na "kujipanga" kwa ajili ya utekelezaji huo. N akwa kuwa nipo katika mchakato huu naomba msaada wa mawazo kwa wakle ambao tayari wapo kwenye shughuli za namna hii (iwe ni taarifa za mahitaji, wapi pa kupata msaada wa kitaalamu, contacts za wahusika au hata kama kuna mtu Mwenye documented project sample ya related project anisaidie ili nianze kujipanga). Najiandaa pia kufanya ziara kati ya March na May 2013 kenye maeneo mbalimbali ambako kunafanyika miradi kama hii (miradi midogo na ya saizi ya kati) ya watu mmoja mmoja au vikundi ilki kujipa elimu kwa vitendo!! Naomba wenye uzoefu wawasisiane name kwa email ya SELUDM2012@gmail.com au wani-PM humu tuweze kujuzana! Watakaotoa maoni kupitia thread hii nao pia nitawashukuru! Ahasanteni

Mheshimiwa nakupongeza kwa kuamua kujichimbia kwenye kilimo wakati ukiendelea kufaidi pensheni yako! Nilivyokuelewa unataka kujiajiri kwenye Kilimo/ufugaji! Naamini mchango wangu wa mawazo kama utakuwa umechelewa kwako utawafaa wanaJF wengine!

Kwa kuwa unajiajiri unapaswa kufanya kibiashara zaidi upate faida zaidi ili kipato kisikatike! Kwanza awali ya yote nakubaliana kuwa hakuna lisilowezekana duniani na tunashauriwa tuepuke kusema kwamba 'jambo hili haliwezekani'! Hata hiyo orodha yako ndefu ya mazao na mifugo inawezekana ni vigumu kuitekeleza! Naomba tu nikushauri yafuatayo ili usije kuingia kwenye mazingira ambayo huwapa kuchanganyikiwa wastaafu wakaishiwa pesa na kuishiwa nguvu mapema sana.

Ndugu yangu orodha yako imenifurahisha imenionyesha kuwa wewe ni mkereketwa hasa wa kilimo na unashauku kubwa ufanye kitu kikubwa. Mimi ninakuunga mkono iwapo dhumuni la uwekezaji wako huo ni kutengeneza kitega uchumi cha utalii (touristic attraction) yaani Agricultural Tourism! Kulinagana na eneo ulilopo kama ni ukanda wa watalii unaweza kuzoa pesa kwani watalii wengi pia hupenda kutazama jinsi gani tunasitawisha mazao na wengine hawajawahi kuyaona! Unaweka uzio kisha unajitangaza watalii wakija wanalipia. Nchi nyingi wanafanya hivyo. Na ndiyo hapo tu ninaafiki wazo la wachangiaji wengine kwamba uongezee na nyuki na samaki!

Pia wazo lako hili ni murua sana iwapo umedhamilia kuanzisha kituo cha mafunzo ya kilimo ambapo utakuwa na mkusanyiko mkubwa wa mazao na mifugo. Hili napo itabidi ujiulize iwapo watanzania wako tayari kulipia mafunzo ya kilimo maana hadi sasa sijaona mfanowe Tanzania!

Lakini tukija kwenye upande wa uwekezaji ili upate faida itakayokufanya uendeshe maisha yako kama zamani ninaingiwa na wasiwasi sana! Kama dhumuni ni kuzalisha kwa ajili ya faida ninawasiwasi sana! Kwa ujumla inategemea na malengo yako na madhumuni yako! Mimi ninajichimbia kwenye eneo moja tu hapa la uzalishaji wenye tija. Orodha uliyokuja nayo hapa ni ndefu sana kwa mtu aliye serious anaetaka kuzalisha kibiashara kwa faida na kipato ili awezekuishi kwa furaha na maendeleo! Haijalishi utastaafu ukiwa na pesa nyingi kiasi gani jua kuwa hiyo pesa utaitandaza kwenye hiyo miradi yote hivyo ufanisi wa mtaji utapungua tofauti na kama ambavyo ingekuwa iwapo ungejimbia mtaji wako kwenye mazao machache na mifugo aina chache tu!

Utaalamu na uzoefu unaonyesha kuwa kadri unavyozidisha mazao tofauti (enterprise) mara nyingi ufanisi katika kila enterprise moja moja hupungua na gharama za uendeshaji huongezeka sana. Kama ukizidisha sana basi inashauriwa usizidi mchanganyiko wa mazao matatu labda na mifugo aina mbili au tatu hivi! Kwa sababu kuzalisha kitu ambacho hujawahi kuzalisha kunahitaji kujifunza mambo mengi sana ambayo huyajui! Unapoingia kwenye uzalishaji inapokuwa ni mara ya kwanza wewe ni kipofu tu, kuna mengi huyajui, sasa utajifunza vitu vingi kiasi hicho kwa wakati mmoja? Halafu bado upate faida? Linapokuja suala la kulima au kufuga watu wa kawaida hudhani ni kutafuta mbegu na kupanda tu, au ni kununua mifugo na kujenga mabanda tu na kuku wa kienyeji wataokota panzi ni hapo utakaposhangaa hata kuku wa kienyeji usipowaendea vizuri huwa wanadunda! Ukishaingia kwenye shughuri yenyewe unakutana na mambo ya kujifunza kwa hasara kubwa! Sasa utapata mafunzo kwa hasara kwenye mazao yote hayo na mifugo yote na ufugaji wa samaki na nyuki ukabaki salama kweli?

Nina mifano mingi nikupe mmoja, rafiki yangu alivutiwa na kilimo cha mihogo baada ya kupiga mahesabu na kuona kinafaida kubwa sana. Akaenda kulima mihogo ikastawi! Mwezi wa Ramadhani ukafika akaenda kuvuna na wanunuzi, mihogo ikatoka mikubwa sana, wafanya biashara wazoefu walipoioa ile aina ya mihogo pale pale wakampa pole! Kila mhogo alioung'oa ulipovunjwa ndani kuna ringi ya nyuzi nyuzi! Yaani ile mbegu aliyotumia ilikuwa haifai eneo lile inatoa nyuzi nyuzi! Walimuelekeza mbegu nzuri kwa eneo lile naye alikiri kuwa alipata shule kwa gharama kubwa! Hali iko hivyo kila tunapoingia zao jipya sasa fikiria una mazao 13 usiyoyajua na mifugo aina 8 usiyokuwa na uzoefu nayo!

Utahitaji umakini sana kujua zao gani linamchango mkubwa na faida kubwa na lipi linanyonya mengine, na mifugo kadharika! Unapokuwa na mazao mengi sana na aina nyingi za mifugo mara nyingi ufanisi unakuwa mdogo sana utajikuta unautaalamu wa kila zao na mfugo kwa juu juu tu! Kuku wa kienyeji pekee yake wanatabia za ajabu ajabu nyingi sana ambazo usipojua kuzidhibiti uzao hauongezeki. Ukijisambaza kwenye miradi mingi (mazao na mifugo) kwa mara moja utaisambaza pesa yako halafu taratibu utaanza kugundua miradi mingine inakusumbua kuiendesha na utaanza kuitelekeza! Kwa ufupi orodha hiyo ni ndefu sana tusitafune maneno haitekelezeki isipokuwa kama ni kwa maonyesho tu ya watalii au kufundishia lakini siyo kwa uzalishaji wenye faida ya kweli!!

Kama ingelikuwa ni kijana anaeingia kwenye shughuri hii angeshariwa aanze kidogo kidogo na kuendelea kujipanua na hatimae angepima iwapo angeendelea kujitanua hadi awe na mchanganyiko mkubwa hivyo! Kwako wewe kama mstaafu jaribu kujipima mwenyewe! Ndiyo maana kwa kuona kwamba unaonekana kupenda mchanganyiko mkubwa wa miradi ukashauriwa ufuge na nyuki na samaki pia! Mheshimiwa ukifanya hivyo utatuachia cha kujifunza duniani kuwa mtaka yote hukosa yote! Tafakari sana!

Samahani sana kwa maelezo marefu saa zingine mimi nami mweeeee!! Heshima kwako Mkubwa Malila nipo kijana wako hapa!!
 
Forum statistics

Threads 1,296,632
Members 498,713
Posts 31,254,290
Top