Foxhunters
Senior Member
- Nov 25, 2019
- 123
- 67
Ndugu zangu, habari ya jioni. Ninaomba ushauri wa kisheria. Mimi nakabiliwa na kesi ya (madai) ya kubumba ambayo mdai alishinda kesi na mahakama ikaamuru mdaiwa (mimi) nilipe deni ndani ya siku 30, na hakukuwa na mjadala baada ya hukumu.
Siku 30 zilipita bila kulipa chochote kwa sababu sikuwa na hela ya kulipa.
Sasa nimeletewa barua ya kuitwa shaurini mahakamani kama mhukumiwa kuwa kwanini mahakama isichukue hatua dhidi yangu?
Naomba ushauri, namna gani nifanye ili nisiingie kwenye matatizo zaidi. Lengo langu ni kujichanganya ili nilipe deni husika. Shida iliyopo ni muda, nikipata miezi minne ninaweza kupata hela ninayodaiwa na kuilipa yote.
Nifanyeje juu ya shauri nililoitiwa mahakamani? Ushauri tafadhali, sina uzoefu na mambo haya ya kesi na mahakama.