Msaada kwenye kesi yangu ya Madai

Dom2

Member
Jul 15, 2021
72
99
Habari za leo ndugu zangu,

Nimemfungua kesi ya Madai ya kumdai mdaiwa wangu jumla ya Tsh 5,874,500/= tangia Tarehe 17.03.2023 katika Mahakama ya Mwanzo Dodoma.

Hukumu ya kesi imetoka tarehe 04/04/2023 baada ya mtuhumiwa kukiri. Hakimu kamuamuru anilipe hela hiyo ndani ya miezi mitatu, kwa maana tarehe 04/04-4/7/2023. Muda ulipita na Mdaiwa hakulipa chochote.

Nikarudi Mahakama tarehe 10/07/2023 kuripoti kuwa sijalipwa. Wakanielekeza niadike barua ya kukaza hukumu, nikaandika nikawakabidhi.

Mpaka sasa sijapewa taarifa yoyote na nakala yangu ya hukumu pia hawajanipa. Je, nifanye nini kupata haki yangu? Na kipi kinafuata baada ya hatua hiyo?

Naomba sana Wataalamu wangu muongozo wenu wa Kisheria.

Nawasilisha.
 
Hupaswi kuwa na presha kuhusu hilo,
Kukazia hukumu pakikamilika tafuta dalali wa mahakama, tafuteni vitu vyake, tangazeni kwenye gazeti mmpe siku 14, zikiisha madalali wafanye kazi yao.
Kama hana kitu ingia gharama mfunge hata siku 100 tu hakika atakulipa na gharama zote zilizotumika
 
Asante sana kiongozi
 
"Hukumu Kuu iheshimiwe,haya Mambo ya kukazia hukumu ya hukumu Kuu ni ubabaifu ti kwa Wananchi watafuta haki zao kwenye Vyombo vya utowaji haki!! Utakuta kwenye kukazia hukumu unazungushwa kuliko hata kwenye kesi ya msingi iliokupa Tuzo!!
 
Hupaswi kuwa na presha kuhusu hilo,
Kukazia hukumu pakikamilika tafuta dalali wa mahakama, tafuteni vitu vyake, tangazeni kwenye gazeti mmpe siku 14, zikiisha madalali wafanye kazi yao.
Kama hana kitu ingia gharama mfunge hata siku 100 tu hakika atakulipa na gharama zote zilizotumika
Akikazia hukumu upande wa pili utakuja na mapingamizi,na mtaanza tena kesi upya! Wwe nenda na hukumu yako kwa kamanda wa police wa mkoa mpe na uchakavu asimamie haki yako haraka iwezekanvyo na utaipata nakuambia!!
 
Habari za leo ndugu zangu,

Nimemfungua kesi ya Madai ya kumdai mdaiwa wangu jumla ya Tsh 5,874,500/= tangia Tarehe 17.03.2023 katika Mahakama ya Mwanzo Dodoma.

Hukumu ya kesi imetoka tarehe 04/04/2023 baada ya mtuhumiwa kukiri. Hakimu kamuamuru anilipe hela hiyo ndani ya miezi mitatu, kwa maana tarehe 04/04-4/7/2023. Muda ulipita na Mdaiwa hakulipa chochote.

Nikarudi Mahakama tarehe 10/07/2023 kuripoti kuwa sijalipwa. Wakanielekeza niadike barua ya kukaza hukumu, nikaandika nikawakabidhi.

Mpaka sasa sijapewa taarifa yoyote na nakala yangu ya hukumu pia hawajanipa. Je, nifanye nini kupata haki yangu? Na kipi kinafuata baada ya hatua hiyo?

Naomba sana Wataalamu wangu muongozo wenu wa Kisheria.

Nawasilisha.
Wape hela watalegeza!!
 
Akikazia hukumu upande wa pili utakuja na mapingamizi,na mtaanza tena kesi upya! Wwe nenda na hukumu yako kwa kamanda wa police wa mkoa mpe na uchakavu asimamie haki yako haraka iwezekanvyo na utaipata nakuambia!!
Nakala ya huku nayo hawajanipa ni mwezi wa 4 wananizunguusha tu.
Au niende TAKUKURU?
 
Usiende Takukuru utapoteza muda wako,hao hawaingiliani kwenye maamuzi labda ni order kutoka juu! Wwe Cha kufanya nenda kalalamike ngazi inayofuata! Kama shauri lako liko Mahakama ya mwanzo nenda kalalamike kwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ukiwa pamoja na vielelezo vyako OG!!
 
Kesi ya madai inapoteza sana muda. Kabla ya kwenda mahakamani, ulitakiwa kuingia mkataba kwanza na polisi ili wamkamate huyo mpuuzi kwa kesi ya utapeli (ambayo ni kesi ya jinai).
Labda walikopeshana kupitia Mikataba ndiyo maana kawa na power ya kushinda kwenye Madai! Sasa Kama kuna Mkataba hapo police kuingia kwenye madai itakua ngumu kidogo!!
 
Usiende Takukuru utapoteza muda wako,hao hawaingiliani kwenye maamuzi labda ni order kutoka juu! Wwe Cha kufanya nenda kalalamike ngazi inayofuata! Kama shauri lako liko Mahakama ya mwanzo nenda kalalamike kwa Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ukiwa pamoja na vielelezo vyako OG!!
Asante sana.
Hilo la TAKUKURU nimeligusia kwa kua hawataki kunipa nakala yangu ya Hukumu ndo maana,
Hilo unalionaje?
 
Sababu za kutokupa wao wanasema nini!? Au wanasingizia mtandao uko chini!!?? Maana nakala ya hukumu ni haki yako kupewa, uwe umshinda kesi au hauja shinda kesi nilazima upewe Kama utaiomba!!
 
Wanadai kila siku mashine mbovu na pia hawana karatasi.
Wakati mwingine wanataka hela
 
Akikazia hukumu upande wa pili utakuja na mapingamizi,na mtaanza tena kesi upya! Wwe nenda na hukumu yako kwa kamanda wa police wa mkoa mpe na uchakavu asimamie haki yako haraka iwezekanvyo na utaipata nakuambia!!
Huo utaratibu wa hivyo labda upo somalia au Afghanistan!!ila kwa Tz hapa hilo haliwezekani kabisa.Na toka lini tena baada ya kukazia hukumu kuna kesi tena ya kuendelea?kazi kubwa ni mlalamikaji kutambua mali anazomiliki mdaiwa na hapo ndipi huwa kuna kazi nzito.
 
Nikishindwa kujua mali zake nini kitafuata kwa mdaiwa?
 
Yaani hizi kesi za madai bawana. Mi nilijua ukishashinda kesi ndo imetoka. Kumbe kunamambo ya kukazia hukumu. Hapo ndo utazungushwa uzunguke. Mara faili halipo, mara nakala ya hukumu bado haijamaliza kichapwa...yaani vurugu mechi. Nilikuwa na kesi ya madai ya Tsh. 230,000 nikaamua kuachana nayo tu.

Mleta uzi kama unataka jambo lako liende, mtafute hakimu upenyeze rupia.
 
Nimeamini bongo kunawatu uwa wanaongea vitu viwasivovijua kabisa.
Tuambie wwe unachojua kuhusu utekelezaji wa Hukumu! Kwa Nini watu wengi wameshinda kesi zao lakini utekelezaji wa hizo Tuzo ni kazi ngumu sana!? Hata juzi juzi hapa kuna Judge alikua ana staff akakumbushia jinsi utekelezaji wa Hukumu yake ulivyokua mgumu,na akasema hadi hukumu yake ilichwanachwanwa na Waziri Mkuu mstaafu tena mbele yake!!
 
Back
Top Bottom