Naomba ushauri: Mama mkwe amemtafutia mke wangu mchepuko

Naomba ushauri: Mama mkwe amemtafutia mke wangu mchepuko

madala mujipa

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
1,421
Reaction score
864
Amani kwenu,

Nina jamaa yangu mpaka hivi sasa dunia anaiona chungu na hajui achukue uamuzi gani dhidi ya mkewe na mkwewe.

Jamaa ameoa mwanamke ambae tayari alishaolewa na kuzaa mtoto mmoja ila kutokana na maisha kuwa ya tabu mume aliondoka kuelekea Mozambiq kuchimba madini na hakurudi tena mpaka jamaa yangu alipojitwisha majukumu ya kuoa.

Tatizo linalomsumbua jamaa yangu ni pindi alipooa aliamua kwenda kuishi na mke wake nyumbani kwao lakini pale kwao ikatokea sintofahamu na dada wa jamaa yangu ikabidi waende wakapange chumba, kule mama mkwe ikawa kila asubuhi lazima aje ashinde pale home kwa gia ya kujifanya anacheza na wajukuu na jioni anabeba chakula.

Kupita kama miezi sita tangu ule mchezo uanze mama mkwe akatoa ushauri kwanini wasihamie kule nyumbani yaani ukweni sababu nyumba ipo na nafasi na yeye mama mkwe atapunguza msafara wa kuja pale daily, jamaa yangu akashauriwa akakubali wakahamia ukweni sasa baada ya kuingia pale jamaa yangu ndio ameanziwa visa vya kuweza kuua mtu.

Jamaa yangu yeye ni dereva wa daladala sasa siku moja alipata udhuru akarudi nyumbani akakuta mlango wa chumba chake umefungwa na mama mkwe yupo pale barazani anafanya shughuli zake jamaa kuuliza akaambiwa mke ametoka akapiga simu haikupokelewa jamaa akaondoka siku nyingine akarudi tena hali ni ile ile jamaa akamuuliza mama mkwe kwani mama zuberi akiondoka haachi funguo.

Akajibiwa haachi basi jamaa jioni ikabidi angushe mtiti, kumbe pale kuna jirani anauona mchezo mzima ikabidi amg'ate sikio jamaa yangu ya kwamba kuna jamaa huwa anaingia pale na mama mkwe anawafungia kufuli kwa nje mpaka wanapomaliza shughuli zao na hawakuanza leo inavyoonekana mkwe anampenda mwizi zaidi kuliko mkwe halali.

Sasa mpaka muda huu jamaa amechanganyikiwa na mama mkwe amesema jamaa akitaka ahame yeye mwanawe abaki pale na mke ana mpenda na anafikiria watoto wake.

Naomba tumsaidie ushauri maana ameathirika kisaikolojia.
 
Mama na mwana lao moja, aondoke akayaanze ya peke yake ataendajw kuishi kwao na mwanamke, nyie wanaume nyieeee, halafu eti unasema ameathirika kisaikolojia aiseee, mpe pole
ukitegwa huwa hujui pole nitamfikishia
 
Bado anasubiri ushauri?

"....matatizo mengi huwapata watu kwa sababu ya kuchelewa kufanya maamuzi..."
 
Duuuhhhhh mbigu na aridhi zitanisamehe .... Kuna watu hawasiltahili kuishi hapa duniani.

Yaaaan jamaaa achoshwe na kaziii alafu aje achanganywe na MWANAMKE na mama mkwe .

Anyway sijui kwenu nyinyi mnaamini TendA wema uende zako..

Ila mimi huwa naamin ,Haki IPO mbiguni ,Kuna watu wanakupa maumivu makali ambayo majeraha yake hua yanadumu ,,WATU WANAMNA HIII UNAPOPONA JERAHA SIO KUWACHEKEA TENA..
 
Kalogwa sio bure. Wahi katika maombi
 
Mama mkwe na mwanawe.


c356cb8d6261e4293f8fe7512657c7ed.jpg
 
Mistake ilianzia pale alipokuwa anazichekea root za mama mkwe kuja kwake daily

Mistake ya pili ni kuhamia ukweni

Mistake ya tatu kuoa mke wa MTU japo inaweza isiwe na mashiko sana

Sasa kutenda kosa kunakupa nafasi ya kurudi nyuma na kupanga mashambulizi upya

Kama hakuchukua maamuzi ya hapo Kwa hapo ni jambo jema sasa dawa ni moja tu arudi akae na ndugu zake wa damu na marafiki wa karibu hawa wahenga watakuwa na ushauri mzuri kuliko sisi

Mchanga wetu una asilimia moja tu kwenye kutatua tatizo zima

Aombe msamaha Kwa ndugu zake alipokosea wawe nae pamoja maana mpaka ukaenda kuishi ukweni ndugu zake wasitie neno lazima kuna walakini


Conclusion
Mama mkwe ni Malaya ndiyo michezo yao nahisi na binti huwa anamfungia mama yake huku akisikilizia mama yake anavyopambana na mikuyenge ya vijeba
 
Ujinga huu si aondoke huko mwanamume gani unaishi kwa wakwe uboya wako ndio unakutesa kapange nyumba anza kivingine
 
Hilo la kuishi kwa mkwe halijanibariki kabisaa, pili baada ya kuambiwa hayo alifanya uchunguzi au ndo kalibeba ka lilivyo!!!
Waondoke hapo kwa wakwe kwanza ndo atafute suluhisho!!!!
 
Amani kwenu

Nina jamaa yangu mpaka hivi sasa dunia anaiona chungu na hajui achukue uamuzi gani dhidi ya mkewe na mkwewe

Jamaa ameoa mwanamke ambae tayari alishaolewa na kuzaa mtoto mmoja ila kutokana na maisha kuwa ya tabu mume aliondoka kuelekea mozambiq kuchimba madini na hakurudi tena mpaka jamaa yangu alipojitwisha majukumu ya kuoa

Tatizo linalomsumbua jamaa yangu ni pindi alipooa aliamua kwenda kuishi na mke wake nyumbani kwao lakini pale kwao ikatokea sintofahamu na dada wa jamaa yangu ikabidi waende wakapange chumba,kule mama mkwe ikawa kila asubuhi lazima aje ashinde pale home kwa gia ya kujifanya anacheza na wajukuu na jioni anabeba chakula

Kupita kama miezi sita tangu ule mchezo uanze mama mkwe akatoa ushauri kwanini wasihamie kule nyumbani yaani ukweni sababu nyumba ipo na nafasi na yeye mama mkwe atapunguza msafara wa kuja pale daily,jamaa yangu akashauriwa akakubali wakahamia ukweni sasa baada ya kuingia pale jamaa yangu ndio ameanziwa visa vya kuweza kuua mtu

Jamaa yangu yeye ni dereva wa daladala sasa siku moja alipata udhuru akarudi nyumbani akakuta mlango wa chumba chake umefungwa na mama mkwe yupo pale barazani anafanya shughuli zake jamaa kuuliza akaambiwa mke ametoka akapiga simu haikupokelewa jamaa akaondoka siku nyingine akarudi tena hali ni ile ile jamaa akamuuliza mama mkwe kwani mama zuberi akiondoka haachi funguo

Akajibiwa haachi basi jamaa jioni ikabidi angushe mtiti, kumbe pale kuna jirani anauona mchezo mzima ikabidi amg'ate sikio jamaa yangu ya kwamba kuna jamaa huwa anaingia pale na mama mkwe anawafungia kufuli kwa nje mpaka wanapomaliza shughuli zao na hawakuanza leo

inavyoonekana mkwe anampenda mwizi zaidi kuliko mkwe halali

Sasa mpaka muda huu jamaa amechanganyikiwa na mama mkwe amesema jamaa akitaka ahame yeye mwanawe abaki pale na mke ana mpenda na anafikiria watoto wake

Naomba tumsaidie ushauri maana ameahathirika kisaikoloji
Mwache aende zake bhana,huyo mama Mkwe amejifungulia kiwanda na ww unaking'ang'ania cha nn? Beba wanao anza mbele
 
Halafu aache mambo ya kijinga kuishi ukwenj,binafsi ukweni nitashinda tu hata kulala silali bora niende lodge
 
Hilo la kuishi kwa mkwe halijanibariki kabisaa, pili baada ya kuambiwa hayo alifanya uchunguzi au ndo kalibeba ka lilivyo!!!
Waondoke hapo kwa wakwe kwanza ndo atafute suluhisho!!!!
Alifanya uchunguzi na akagundua ni kweli
 
Pole yake' bora aondoke tu apo amna chake tena atakuja kulishwa limbwata bure
 
Mistake ilianzia pale alipokuwa anazichekea root za mama mkwe kuja kwake daily

Mistake ya pili ni kuhamia ukweni

Mistake ya tatu kuoa mke wa MTU japo inaweza isiwe na mashiko sana

Sasa kutenda kosa kunakupa nafasi ya kurudi nyuma na kupanga mashambulizi upya

Kama hakuchukua maamuzi ya hapo Kwa hapo ni jambo jema sasa dawa ni moja tu arudi akae na ndugu zake wa damu na marafiki wa karibu hawa wahenga watakuwa na ushauri mzuri kuliko sisi

Mchanga wetu una asilimia moja tu kwenye kutatua tatizo zima

Aombe msamaha Kwa ndugu zake alipokosea wawe nae pamoja maana mpaka ukaenda kuishi ukweni ndugu zake wasitie neno lazima kuna walakini


Conclusion
Mama mkwe ni Malaya ndiyo michezo yao nahisi na binti huwa anamfungia mama yake huku akisikilizia mama yake anavyopambana na mikuyenge ya vijeba
Hitimisho linachekesha japo si wakati wake
 
Back
Top Bottom